PostGE2025 Nchi ina viongozi wasio na aibu wala hofu ya Mungu

PostGE2025 Nchi ina viongozi wasio na aibu wala hofu ya Mungu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ngengemkenilomolomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
316
Reaction score
549
Wakuu
Hii nchi sasa inaongozwa na viongozi wasio na aibu wala hofu ya Mungu.

kama wanazo akili basi wanalazimika kuziacha nyumbani ili wamfurahishe mkuu wao.

Kwanza nimemsikiliza Gerson yan ni utumbo mtupu kaongea yani unawapongeza waandishi wa habari kwa kuandika habar za kusifia tuu nchi yao huku watu wanakufa bila hatia, watu wanatekwa na nyie kama mamlaka hamfanyi kitu.

Halafu leo unawasifia kwa kutohoji chochote, unawasifia kwa kutouliza why watu wanakufa, why rushwa imetawala, why watu wanatekwa ili muendelee kuiba, kupora, kuteka na hata kuua.

Yaani kwa kifupi ni kwamba nyie ndo wenye mamlaka ya nani aandike nini na nini kisiandikwe.

Pili nimemshangaa sana Nchemba anawezaje kwenda kuangalia mali ambazo zinaweza kuwa restored badala ya kwenda kuziona familia zilizopoteza wapendwa wao ambao ndo wameondoka hivo hawatorudi kamwe.

kitendo cha kufanya hizo mali kuwa priority kinathibitsha kwamba ripoti ya CNN ilikua ya kweli tena ukweli mtupu na kwa kufanya hivo anathibitsha kwamba sio aina ya kiongozi ambaye Tanganyika inamtaka,ni kiongozi wa hovyo na ndo maana Magu alimuweka pembeni
kapewa uwaziri mkuu kama asante baada ya kuidhinisha pesa nyingi kutoka bila kuhoji wala kusita

Mwisho wa yote Mungu wetu hasinzii, hakawii wala hawahi ipo siku haya yote yatawarudia tena kwa gharama kuwa

Mungu ibariki Africa
Mungu ibariki Tanganyika
 
Back
Top Bottom