Nchi inabidi kuongozwa na mifumo thabiti na imara na si matamko ya wanasiasa. Wasomi tulisaidie Taifa

Nchi inabidi kuongozwa na mifumo thabiti na imara na si matamko ya wanasiasa. Wasomi tulisaidie Taifa

Serikali imeanza kuzidiwa , population inaongezeka kwa kasi na life span inaongezeka hapa Mimi natajaribu kutaka nchi iwe na mifumo sahihi na sio nchi kuongozwa kwa matamko mfano hawa watoto elfu moja wanapozaliwa kila Mwezi katika kata ya moja maana yake huko Mbele kitatokea Matatizo ya ukosefu wa shule, zahanati n.k mfano shule nyingi za mjini darasa moja wanakaa watoto 100+ badala ya 45 so wanasiasa wamepiga usingizi wa pono.
Hivyo mifumo ni mibovu!!
Aisee. Haya land. "Sijui"
 
Kila mwezi kwenye kata moja kufyatuliwa watoto 1000 ni kidogo?! Kwa hali hiyo serikali itafanya kazi nyingine zaidi kujenga madarasa na kutengeneza madawati??
Na bado hujaenda hospital ya Muhimbili, Agakhan, hospital zilizopo wilaya ya Ubungo, Ilala, Kigamboni.
 
Bad enough! Wasomi wengi wa taifa hili wamemezwa na siasa, nchi inaendeshwa kwa mihemko. Most of them they are after money, ndiyo maana wanakimbilia huko kwenye posho za 300+k a day, na mikopo ya hadi 500millions.
 
Sasa mtani tatizo la hii nchi siasa ilipewa kipaumbele tokea nchi ilipoasisiwa jambo lililofanya wanasiasa wakawa na nguvu kupindukia. Cha kufanya ni katiba mpya kuunda taasisi imara za kiutendaji na kuondoa mamlaka kubwa waliyo nayo wanasiasa kwenye utendaji wa mifumo ya nchi.
 
Back
Top Bottom