Nchi inahitaji utekelezaji, ziara tulishazichoka au ni kupoteza muda

Nchi inahitaji utekelezaji, ziara tulishazichoka au ni kupoteza muda

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Serikali ya CCM imekuja na style mpya ya wakuu waliomo serikalini au tuseme serikali iliyoundwa na CCM inastyle ya kupanga ziara ,mkae mkielewa hakuna cha ziara wala matembezi ni namna ya kula hela kwa njia ya kulipana posho.

Wananchi wanahitaji maendeleo mambo ya ziara yamepitwa na wakati, huu ni wakati wa kidigital na barcodes, Raisi au kiongozi anatakiwa awepo ofisini. Ufunguzi na mafunguzi hata meya au mkuu wa wilaya husika anaweza kuhudhuria na kuwakilisha serikali.

CCM na viongozi wenu mnatupotezea muda kama maendeleo yanaletwa na ziara mbona tungelikuwa mbali sana, unafanya ziara unaondoka watu wanamega. Hakuna faida za kuwa na wakuu wa Mikoa, wilaya, majimbo shehia maana serikali ipo mpaka vijijini lakini bado utasikia watu wanatoka wanakotoka eti wanaenda kufungua au kuangalia mradi, toa estimate time to complete the project, time ikifika unaulizia,haukumalizwa unapata faida kwa mkandarasi kukulipa.

CCM mnaila nchi kwa ziara zisizo na tija.
 
Mwache mama yetu jamani. Tena inavyoonekana anapenda matembezi kweli kweli. Pengine ndiyo fasheni yake ya uongozi. Anajaribu kuonyesha njia na kuonekana. Kujiimarisha. Watu wamzoee na kumtambua. Kuwa yeye ndiye rais na Amiri Jeshi Mkuu. Naamini atakuja kutulia huko mbele ya safari kwa sababu hata hizi safari zitamchosha.

Kwa sasa ngoja atembelee na afike Kanda zote za nchi yetu kujitambulisha na kufahamika. Na ni wananchi hawa hawa ndiyo atarudi kuwaomba kura 2025. Na kusema kweli safari hizi ndiyo nafasi yake ya kujionea miradi mikubwa ya maendeleo inavyokwenda; na kuwa karibu na wananchi. Rais anayekaa ofisini tu sidhani kama anaweza kuwa na uhalisia wa kinachoendelea kwa anaowaongoza.

 
Aahahhhaaa unajua wanadamu mna staajabisha sana..! Si nyi juzi mlisema Mama aache kuteua teau aje kwa wananchi azione kero? Sio nyie? By the way kufanya ziara ndio ufuatiliaji wa utekeleza wa mipango ya maendeleo.

Ninachofurahi Mhe. Raisi wetu yupo very systematic.. Tazama kaanza ziara za nchi jirani kusaini mikataba yenye tija, within the process anapanga timu yake imara itakayomsaidia kuendeleza kazi na kuondoa makando kando ya msimu ulopita, at the same time anarejesha uhusiano wa nchi yetu na mataifa, saivi ameanza ziara kufuatilia utekelezaji na uendelezwaji wa miradi ya maendeleo. Big Up sana my President..!!

Mwacheni Mama afanye kazi. Binadamu tupo kama kinyonga, tena kinyonga ana afadhali maana hubadili brangi yake akihisi hatari au akiona hali tofauti..
 
Mataga ndio wanafurahi kuona viongozi wa serikali kuu wanazunguka zunguka kama Kigwangala badala ya kukaa ofisini kwao.
Aahahhhaaa unajua wanadamu mna staajabisha sana..! Si nyi juzi mlisema Mama aache kuteua teau aje kwa wananchi azione kero? Sio nyie? By the way kufanya ziara ndio ufuatiliaji wa utekeleza wa mipango ya maendeleo...
 
Aahahhhaaa unajua wanadamu mna staajabisha sana..! Si nyi juzi mlisema Mama aache kuteua teau aje kwa wananchi azione kero? Sio nyie? By the way kufanya ziara ndio ufuatiliaji wa utekeleza wa mipango ya maendeleo...
Binadamu atakwambia kukosoa ni haki yake. Hajui kwenye ziara hizo hizo kuna kazi kubwa inayofanyika.
 
Back
Top Bottom