Nchi inapitia wakati mgumu kuwahi kutokea. Gunia la mahindi limefika Tsh 180,000

Kama kuna kipindi mkulima anapiga hela Ni kipindi hiki imagine mchele mpya tunanunua 1800/1600 Tena mashineni,ukinunua kwa mkulima 1500 haishuki hapo, karanga kilo 3500,gunia la alizeti tulikua tunanunua 35,000 kutoka shambani nawapigia ndugu zangu juzi wananiambia gunia elfu 60000, wengine 70000 bado maharage ndo balaa tunakoelekea kilo tutauza 2500 maana kila siku yanapanda aisee sijawahi kuona mfumuko wa Bei Kama huu hasa kwenye chakula Tena msimu wa mavuno hongereni mliolima.
 
Impacts ipo Sana tuu ila hili la Bei serikali inalijua na imeamua iwe hivyo Ili wakulima wanufaike kwa jasho lao..

Hakuna kufunga mipaka.
Bei ilikua lazima kupanda kwasababu pembejeo zilipanda bei kwa kasi....mtu ametumia gharama kubwa sana katika upandaji wa mazao yake...lakin mm naona hii swala la kupanda bei halitawanufaisha sana wakulima wadogo wadogo Bali watu wenye vipato vyao vikubwa Na walioweza kulima richa ya kupanda kwa bei ya pembejeo....wakulima wengi wa hali ya chini walishindwa kulima kutokan Na mfumuko wa bei za pembejeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mtu aloshindwa kulima then unataka anufaike,atanifaikaje sasa? Kilimo sio mahindi tuu.
 
Bei sio shida, mwananchi wa kawaida asiye na kipato anaweza kumudu hiyo bei?
 
Mtoa mada ukiwa unataja bei za mazao usiache pia kutaja mkoa ulipoikuta iyo bei.

Haya tuambie iyo bei ipo masoko ya mkoa gani!?
 

Tatizo ni mvua Hakuna mkuu!! Mimi ni mkulima mkuu bajeti kuwa kubwa na mvua hakuna ndo unakuwaje sasa mkuu?
 
Kuimba kupokezana Boss. Safari hii ni zamu ya Wakulima. Mlitucheka sana ila sasa mtatusalimia kwa heshima!
 
Wapi huko ambapo mahindi yanauzwa 180k? Maana sasa hivi msimu wa mauzo.. mahindi bei ya juu sh. 700 kwa kilo

Gunia moja bei ya juu 80k
 
Kwa anaehitaji mahindi mazuri na bei poa, aje tuonger inbox japo yanazid kupanda bei
 
Binafsi nmelima mpunga mwaka huu Kwa kawaida tulilima Kwa heka ef40,000 ila mwaka huu tumelima Kwa 60,000,kuchabanga ef 30,000 ila tumelima Kwa 45,000,mbolea ef 64,000 ila mwaka huu tumeninia Kwa 150,000,kuvuna tumevuna 130,000 Kwa heka hapo umepata gunia 6 + na madawa mengine + athari za hali ya hewa kwahyo gharama za uzalishaji ni kubwa huku mavuno machache Tena ukipiga hesabu. Hakuna faida unarudisha Hela tu.tuvumilieni ndugu zetu mkiona tnafaidi njooni tulime mapori yapo mengi
 
Gunia la Mahindi kwa Tsh. 180,000 (Laki moja na Elfu Themanini) ni bei ya mkoa gani Mkuu?
 
Mkulima hanufaiki na lolote wanaonufaika ni walanguzi wala si wakulima wakulima bado ni masikini wa kutupwa
 
Kusema ukweli gharama za kilimo zimepanda sana sasa hivi... Sana. So tuendelee tu kuvumiliana
 
Wahuni watakuita sukumagang
 
Wapi huko, ambako mahindi yamefika bei hiyo ya 180,000/=.
 
We jamaa vipi?

Mwaka huu hali ya mavuno iende vizuri kwa mvua gani?
 
Wakati mbolea inauzwa 1kg shilingi elfu tatu mbona mlikaa kimya mkawaachia wakulima walalamike wenyewe. Kilimo ni gharama acha wakulima nao wafaidike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…