Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Nchi kuwa kubwa, na dhaifu halafu kuwa na makao makuu pembezoni ni hatari sana kwa usalama wake.
Kwa nchi zetu hizi kadri unavyozidi kuwa mbali na Capital City ndivyo unavyozidi kusahaulika. Na watu waliosahaulika ni rahisi kuasi.
Hawa wameweka mji mkuu Kinshasa. Kilomita zaidi ya 2500 kufika Goma. Wangetafuta mji hapo katikati.
Msumbiji wameweka mji mkuu kwenye kona kabisa. Ndiyo maana inakuwa ngumu kudhibiti maeneo ya kaskazini. Yanaishia kudhibitiwa na waasi na sasa magaidi. Walau makao makuu yangekuwa Beira.
Pengine Nigeria wasingehamisha makao makuu kutoka Lagos wangepata shida sana na watu wa kaskazini, walio wengi.
Nchi zingine zilizoona umuhimu wa kuweka makao makuu ya nchi katikati ni Pamoja na Tanzania na hivi karibuni Indonesia.
DRC ingekuwa na Capital City katikati ya nchi ingeweza saidia kuepuka machafuko inayoyakabili miaka na miaka?