Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Nchi kumi za kutembelea katika kipindi cha miaka mitano

Ukiachana na kwenda Dubai kibiashara ambayo naona ndo wengi huenda, Dubai kuna vivutio gani wazee. Hapa nilipo nawaza kwenda Rwanda kutalii au Dubai kuona mandhari tu.
Kwa ambao mshafika nipeni maelekezo hasa hasa Dubai, sehemu za bei nafuu za kufikia, taratibu za visa na mengine. Mtu asije akasema vijana wa sasa hivi ni wavivu wa kutumia mtandao 😂😂 mtandaoni sielewi naona information ni nyingi kuliko bichwa langu.
 
Nina mpango pia wa kutembelea Dubai Desemba hii.

Kwa taarifa nilizozipata ni utalii wa mandhari zaidi na biashara. Sifahamu sehemu za kufikia kwa majina lakini gharama zake ziko vizuri tu chini ya USD 50 unapata hoteli nzuri. VISA ni online na unaipata kwa USD 100 hivi.

Unachotakiwa kufanya ni kufanya booking na Emirates then kuna kipengele cha kupata online VISA ambayo itatolewa moja kwa moja kwako ukiwa tayari na taarifa zote na umefanya mchakato wa sehemu ya kufikia.

Kila la heri Mkuu, kama tayari ushaenda weka uzoefu wako hapa.
 
Hongera sana Mkuu, nimelipenda wazo lako.

Mipango yangu ni kusafiri nchi za Afrika Mashariki kwanza (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC).

Na baadae niende Southern Africa nianze na Eswatini, Namibia, Lesotho, Angola, Zimbabwe, Zambia na Malawi.

Kwa nchi za North Africa nitahakikisha mwaka huu na ujao nimefika Egypt, Morocco na Tunisia.
 
Hivi kwenda South kwa lengo la kutembea kuna complications zipi? kwa sisi ambao hatuna vipato vya maana.
 
Ndiyo, mtu anayesafiri kwa basi kuhusu complications mipakani hiyo ndo nataka kujua zaidi.
Sawa kabisa, sina uzoefu na hilo suala.. lakini inawezekana kukawa na gharama na pesa ambazo maafisa wa mipakani wanaomba kutoka kwa wageni.

Kwa sababu unatumia bus inaweza kuwa kusiwe na vizinga vingi.

Nimesafiri nchi za Afrika Magharibi hayo ndio mambo yao hasa ukitumia usafiri wa Taxi au bus. Watakulazimisha ulipie kadi ya yellow card na chanjo za yellow fever, meningits n.k., pia wakati mwingine wataomba tu fedha bila sababu yoyote.
 
Back
Top Bottom