Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 275
- 795
Now Tanzania imekuwa nchi ya ajabu sana, Kila Tv na radio habari yao ni moja tu "cheza ushinde kwa buku tu" hii inafikirisha sana. Inaamana Uchumi wetu umeporomoka sana kiasi kwamba kila mwananchi anavizia mchongo wa kamali ili kutimiza malengo.
Uchumi huru kwa wananchi hasa wa hizi nchi maskini kama Tanzania ni ule unaotokana na shughuli halisi za uzalishaji mali (tangible assets) kama kilimo, uvuvi, ufugaji,ubunifu katika ujasiriamali, viwanda, n.k kwa sababu zinaongeza thamani ya mapato halisi ya mtu na taifa na hivyo kupelekea utengamo wa bei (price stabilization)
Lakini cha ajabu badala ya chombo cha habari cha Taifa kukemea kamali nchini na kusisitiza kukuza uchumi kwa shughuli halisi za uzalishaji wao sasa hivi wanahimiza kamali inayoitwa mbungi mtonyo.
Athali za hii kitu kamali

- Jamii kukosa ubunifu katika kuzalisha mali nchini.
- Wananchi wa kuonekana ni vilaza sana maana wanachukuliwa pesa zao kizembe kwa kuhaidiwa kushinda 1 ml. Hii inaonesha namna mfumo wetu wa elimu ulivyo hovyo.
- Umaskini kuendelea kukithiri miongoni mwa watanzania kwa kuamini one day watatoboa mbungi mtonyo na baadhi ya kamali zinazochezeshwa kwenye kila chombo cha habari