BestOfMyKind
JF-Expert Member
- Apr 26, 2012
- 1,350
- 1,464
Yaani watz tunavyoishi ni kama vile bado tunajifunza kuishi. Ni kama vile tupo mafunzoni yaani hata ukikosea mara mia kwa kufanya makosa yale yale utajirekebisha kwenye maisha yenyewe haya yakipita. Hatupo sirias kabisa.
Kila kitu kimepanda bei kasoro mazao ya mkulima tu yaliyo shambani. Yaani mbolea imepanda bei, gharama ya usafiri wa kupelekea mbolea shambani imepanda bei, ila bei ya mazao shambani inapangwa na dalali ambae hata jembe hajui likoje.
Katika kipindi hiki cha hali mbaya ya chakula duniani sisi kama taifa ilibidi tuingize hela nyingi kwa kuuza chakula kwa gharama kubwa huko duniani wakulima wapate fedha na serikali ipate fedha.
Baadala yake tupo tunaibiana tu, yaani dalali anamuibia mkulima, mkusanya ushuru anaiibia serikali, dalali anaibiwa na madalali wajanja zaidi. Chini ya haya yote ndo tupo sisi tulionunua mbolea ya kilo 50 kwa laki moja na nusu ili tulime tupate hela ya kuendesha maisha yetu.
Kwenye mnyororo wa uzalishaji tukishindwa kulima sisi kwasababu tunapata hasara msimu wa pili mfululizo hawa madalali watakufa njaa lakini wao hawalijui hilo.