Nchi wafadhili wamezuia kila aina ya mikutano sisi nchi masikini tunahimizana kuzidisha maombi

Nchi wafadhili wamezuia kila aina ya mikutano sisi nchi masikini tunahimizana kuzidisha maombi

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
5,082
Reaction score
20,806
Wakati nchi wafadhili kama Ujerumani inazuia mikutano ya hata watu 2, kufunga kila aina ya mikutano ili kupambana na Corona sisi tunahimizana kukutana na kuendeleza maombi.

Italy ambako ukatoriki na maombi ni sehemu ya maisha yao wamezuia kila aina ya mikutano sisi tunahimizana kuendeleza maombi. Saudi Arabia ambako mtume ndio kwao wamezuia kila aina ya ibada sisi tunahimizana maombi na kuendelea kukutana kama vile hakuna kinachoendelea.

Tumefunga taasisi zote za elimu ili kuzuia mikusanyiko ila bado tunakutana kanisani kuhimizana maombi, sasa shule tulifunga za nini kama mikusanyiko ya aina hiyo hiyo bado ipo, watoto wataenda kanisani, watachanganyikana na wenzao na kama kuna ugonjwa bado wataambukizana.

Wanaotufadhili na kutulisha wamechukua hatua, tunasubiri tatizo liwe kubwa halafu tukimbie tena kwenda kuwaomba msaada wa kibinadamu.

Lets wait and see.
 
Sisi siyo wao, damu yetu ni tofauti na wao. Joto na giografia yetu inaruhisu Maombi na kufanya usafi.
Ukiumwa jitenge na watu , siku tatu Mafua yanatulia. Ona wote walioambukizwa walivyofanya.

Tumeumbwa hivyo na tuko hivyo.
We are Super race.
 
Wao watajinusuru na hili janga muda huo linatusumbua sisi, kisha watatupa misaada, nasi kwa ukarimu wetu tutawashukuru sana kwa moyo wao wa kujitoa kama ilivyo desturi yetu.
 
Hakimu Mfawidhi, Turudi kwenye misingi na taratibu za kiafya hasa kipindi hiki cha gonjwa hili la mlipuko..

Ishu ya maombi ni ramli ya patapotea.. Mungu hujibu maombi ya wenye haki na wkamilifu machoni pake.. Hawa wanaotakiwa kufanya maombi ni wachafu na wananuka uvundo wa maombi
Mungu hujibu maombi ya wenye maarifa na akili hajibu maombi ya wapumbavu..

Huwezi kulikaribia shimo lenye nyoka huku ukitumainia muujiza wa maombi Kabla hujafanya juhudi za kujiepusha nalo usitumbukie

Kanisa la Kristo sio majengo.. Na madhabahu yake sio mimbari ya mawe, tofali au marumaru.. Na dhabihu zake za haki sio matoleo ya pesa za wanadamu waliojazwa choyo na ubinafsi
Kanisa la Kristo ni roho iliyopondeka na kutulia..

Madhabahu yake ni mwili safi usio na mawaa wala najisi.. Dhabihu zake za haki ni upendo, uchaji, kiasi na matendo yote yasiyomuinua shetani

Hivyo basi Kanisa ni wewe na Yule unayemwamini.. Ibada yaweza kuwa hata ndani ya familia na kila kitu kikawa sawa.. Yale makusanyiko kwa sehemu kubwa ni makusanyiko ya chui waliovaa ngozi ya kondoo... Kwa kipindi hiki HAYANA FAIDA.. TUYAEPUKE

Jr[emoji769]
 
Kwa hiyo Kwa mawazo yenu shetani aachwe aendelee Kula uhai wa watu??

Elekeza namna maombi yafanyike mkuu, siyo kuyazuia
 
Kwa hiyo Kwa mawazo yenu shetani aachwe aendelee Kula uhai wa watu??

Elekeza namna maombi yafanyike mkuu, siyo kuyazuia
Italy hawamjui shetani au Saudi Arabia hawajui corona? Waliowaletea dini na kuwafundisha kumjua shetani wamechukua tahadhari, nyie wakalili dini ndio mnamjua shetani kuliko waliomtunga?
 
Ulichosahau ni kuwa sisi ni maskini wa vingi, ikiwemo kupanga na kuchagua. Kwa tukio la gonjwa hili na kinacho endelea, inathibitisha hatuna collective leadership, kuna mpiga kengele wa kanisani wa kuwaamsha waumini waende kanisani kumsikiliza paroko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom