Wakati nchi wafadhili kama Ujerumani inazuia mikutano ya hata watu 2, kufunga kila aina ya mikutano ili kupambana na Corona sisi tunahimizana kukutana na kuendeleza maombi.
Italy ambako ukatoriki na maombi ni sehemu ya maisha yao wamezuia kila aina ya mikutano sisi tunahimizana kuendeleza maombi. Saudi Arabia ambako mtume ndio kwao wamezuia kila aina ya ibada sisi tunahimizana maombi na kuendelea kukutana kama vile hakuna kinachoendelea.
Tumefunga taasisi zote za elimu ili kuzuia mikusanyiko ila bado tunakutana kanisani kuhimizana maombi, sasa shule tulifunga za nini kama mikusanyiko ya aina hiyo hiyo bado ipo, watoto wataenda kanisani, watachanganyikana na wenzao na kama kuna ugonjwa bado wataambukizana.
Wanaotufadhili na kutulisha wamechukua hatua, tunasubiri tatizo liwe kubwa halafu tukimbie tena kwenda kuwaomba msaada wa kibinadamu.
Lets wait and see.