Hakimu Mfawidhi, Turudi kwenye misingi na taratibu za kiafya hasa kipindi hiki cha gonjwa hili la mlipuko..
Ishu ya maombi ni ramli ya patapotea.. Mungu hujibu maombi ya wenye haki na wkamilifu machoni pake.. Hawa wanaotakiwa kufanya maombi ni wachafu na wananuka uvundo wa maombi
Mungu hujibu maombi ya wenye maarifa na akili hajibu maombi ya wapumbavu..
Huwezi kulikaribia shimo lenye nyoka huku ukitumainia muujiza wa maombi Kabla hujafanya juhudi za kujiepusha nalo usitumbukie
Kanisa la Kristo sio majengo.. Na madhabahu yake sio mimbari ya mawe, tofali au marumaru.. Na dhabihu zake za haki sio matoleo ya pesa za wanadamu waliojazwa choyo na ubinafsi
Kanisa la Kristo ni roho iliyopondeka na kutulia..
Madhabahu yake ni mwili safi usio na mawaa wala najisi.. Dhabihu zake za haki ni upendo, uchaji, kiasi na matendo yote yasiyomuinua shetani
Hivyo basi Kanisa ni wewe na Yule unayemwamini.. Ibada yaweza kuwa hata ndani ya familia na kila kitu kikawa sawa.. Yale makusanyiko kwa sehemu kubwa ni makusanyiko ya chui waliovaa ngozi ya kondoo... Kwa kipindi hiki HAYANA FAIDA.. TUYAEPUKE
Jr[emoji769]