Nchi wafadhili wamezuia kila aina ya mikutano sisi nchi masikini tunahimizana kuzidisha maombi

Italy hawamjui shetani au Saudi Arabia hawajui corona? Waliowaletea dini na kuwafundisha kumjua shetani wamechukua tahadhari, nyie wakalili dini ndio mnamjua shetani kuliko waliomtunga?
Mtu ameumbwa kuabudu, na mtu aspomwabudu Mungu muumbaji ni lazima ataabudu sanamu hiyo ni lazima, hata wewe kipo unachokiabudu, iwe ni kaburi la mababu au ushirikina nk


Ukiona hivyo, jaribu kuheshimu dini za wenzio, shauri wafanye namna gani maombi Yao kama unavyofanya wewe
 
Mkuu, 100% ya bandiko lako ni ukweli tupu,

Cha nyongeza hapo ili kupanua uelewa zaidi, ni lazima pia tujaribu kuangalia mfano wa Abednego, Shadrack Meshack, hawa watu waliandaliwa Moto kwenye shimo na wakadumbukizwa humo, lkn pia Kwa Daniel alikataa kuabudu miungu naye akatupwa kwenye tundu la Simba, Kwa Imani zao kubwa waliopona,

Je mifano hiyo haiwezi kutumika Leo Kwa watu wenye Imani kama za mashujaa hao?

Maana Kwa Daniel ilikuwa rahisi tu kwamba akubali kuiabudu sanamu ili apone, ndivyo ilivyo Leo kwamba kila kitu kisimame na kanisa lisifanye maombi ili huyu shetani aendelee kufanya yake

Hata hivyo nimekuelewa kwamba kanisa sio jengo, Bali mwili wa mtu ndio Hekaru, Asante
 
Sema wewe ndiyo labda maskini,nchi hii ni tajiri..Sisi ni matajiri
 
Wewe wa ajabu kweli ; umeambiwa kwa kuwa Kanisa Katoliki makao yake makuu yako Italy basi ndiko kuna Mungu zaidi? umeshaambiwa kwamba kutegemea cha nduguye hufa maskini acha ugojwa wa kutukuza wafadhili kwanza wanarudisha yale waliotuibia, nataka kuanza kampeni ya mataifa ya Africa zigome kulipa madeni ni hela yetu wanarudisha.
 
WHO haikatazu Maobi au sala haikatazwi,kinachokatazwa ni mkusanyiko.
India amefanya hivyo,na mataifa mengine yanaendelea kupunguza msongamano au mkusanyiko kwa siku kadha ili kupisha shari kamili.
Tatizo kubwa kwetu ni ufukara kwa watu walio wengi sehemu za mjini.
Je Magufuli akifanya lockdown yupo tiyari kugawa pesa kwa kila mwnanchi kupewa pesa inayotosha hadi Corona itokomee?
Mungu katupa mtihani mkubwa.kuongoza watu ni tofauti na kuongoza kuku.Tutumie busara ili kujenga nchi.Historia itatuhukumu.
 
Jiwe anaogopa watu wakiacha kwenda nyumba za ibada kufanywa kondoo watazidisha kumkosoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…