- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hivi kuna ukweli kuna Siku ya kupeana mimba nchini Urusi
- Tunachokijua
- Baadhi ya kurasa za Mitandao ya kijamii hutaja uwepo wa Siku hii maalumu inayotambulika nchini Urusi ambayo huwapa wapenzi nafasi ya kutafuta watoto.
Kwa mujibu wa kurasa hizo, Siku hii huadhimishwa Septemba 12 ya kila mwaka ambapo watu hukaa nyumbani pasipo kwenda kazini.
Mathalani, ukurasa mmoja wa Mtandao wa X unasema "Siku ya Septemba 12 kila mwaka, wapenzi nchini Urusi hupumzika kufanya kazi ili kupata watoto. Serikali ya Ulyanovsk hutoa pesa na zawadi zingine wa wapenzi wanaofanikiwa kupata mtoto miezi 9 baadaye"
Ni kwa mantiki hii, mdau wa JamiiCheck Mkalukungone mwamba ameomba kuthibitishiwa ukweli wake.
Ukweli wa Madai haya
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini madai haya yana ukweli.
Siku hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 kwenye Jimbo la Ulyanovsk ambapo takriban wanawake 311 walijiandikisha ambapo watoto 46 walizaliwa Juni 2006.
Katika kuendeleza siku hii, mwaka 2006 zaidi ya wanawake 500 walijiandikisha ambapo takriban watoto 78 walizaliwa Miezi 9 baadaye, Juni 2007.
Wapenzi wanaofanikiwa kupata mtoto Juni 12 ya mwaka unaofuata ambapo huadhimishwa Siku ya Urusi hupatiwa zawadi ya Gari, pesa na Jokofu kwa ajili ya matumizi yao.
Aidha, siku hii ilianzishwa na Gavana wa Jimbo hilo Sergei Morozov kama sehemu ya hamasa ya kuongeza idadi ya watu nchini Urusi.
Kwa mujibu wa takwimu za Mei 22, 2024, Urusi ina watu takriban Milioni 144 ikiwa nchi ya kwanza kwa ukubwa duniani huku ukubwa wa eneo lake ukichukua 11% ya eneo lote la nchi kavu duniani.
Idadi hii ya watu ni ndogo sana ikilinganishwa na ukubwa wa eneo hivyo mpango huu ni sehemu ya motisha ya kuongeza idadi ya watu kwenye nchi hiyo.