mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,514
- 4,042
Nimejaribu kufuatilia Kwa ukaribu wengi wa wakosoaji na wasifiaji wengi Kundi kubwa ni Vijana,na shida kubwa ya ulimwengu huu tulionao wa sayansi na teknolojia,Vijana wengi wanamiliki simu janja,wao Kila siku ni kuisema Vibaya Serikali na wengine ndio waimba mapambio Kwa wingi pia,Ila Chanzo Cha yote ni Ukosefu wa Ajira,ndio Maana Kila kijana anaona akiingia kwenye Siasa zinalipa.Mbaya zaidi Vijana wa Chama changu Tawala ni vijana ambao wengi wetu mzimu wa kuwaza Teuzi Kila siku unawatesa ...Ukiondoa Vijana wa CHADEMA ambao wao huiponda Serikali muda wote,huku wakishauri mambo ya ukweli bila kumung'unya na mwisho wa siku huja kuonekana ni lulu kwenye kusaidia Serikali ,mifano ni mingi ya Vijana walioachana na CDM na Sasa wapo CCM,wengi wao walikuwa na nafasi ndani na wengine bado wapo kwenye nafasi.
Nini kinasababisha hayaa..
Chama Cha Mapinduzi kinawatumia vijana wake kwenye mambo mengi,wasomi na wasio Wasomi hasa kipindi Cha Uchaguzi,Baada ya hapo hata hakiwasaidii kupata Ajira au chochote Kile kujiongezea kipato,na mwisho wa siku Kundi la aina hili linakuja kugeuka na Kuanza kuisema Vibaya Serikali au kusifia sifa zisizo sahihi mitandaoni na kwingineko huku baadhi ya Viongozi wakiwa hawajali Kwa lolote ilhali Vijana hao hao wa CCM Njaa zimewashika...
Viongozi wengi wa CCM baadhi yao wenye mamlaka ni wabinafsi Sana,na Wengi wao hujali mambo yao Kuliko mambo ya Watu,hasa Watanzania wenye shida.Naweza kusema Mhe.Samia ana Nia nzuri sana na Watanzania ila wengi wao waliomzunguka ndio wanamharibia na kusababisha wakosoaji kuwa wengi mitandaoni na kwingineko kadri siku zinavyokwenda.
Watu wa Chama Cha upinzani hasa CHADEMA wengi wao sio wabinafsi,wana Upendo Sana,hata Mtu wa Taasisi fulani Akiwa mwanachadema kumpigania mtu anayemfahamu wa CDM kupata Ajira ni rahisi sana Kuliko mwana CCM aliye na nafasi kubwa Mahali fulani.Hata suala na matatizo kama msiba au ugonjwa,watu wa CHADEMA huhamasika Sana kuchangiana Kuliko Wana CCM.
Mwisho na sio muhimu..
CCM kama Chama Tawala Muwasaidie Vijana Wenu wenye Sifa za Ajira kuwapa Ajira Serikalini na Kokote Kule bila hivyo Kundi kubwa litaanza nanyi lakini Mwisho wa siku litakuja kuwa kundi la kupinga pinga na hata huku ndani wengi wa Makada wenzangu ninaowafahamu Kwa ID Feki ni wengi na hata huko makundi wa WhatsApp wapo pia,utaona maandiko mengi ya Vijana hii yote ni kutaka kuonekana na Kuvizia Teuzi ambazo kimsingi ni Chache, sababu ni kukosa Ajira na ugumu wa Maisha ndio Chanzo Cha Kila mtu kuwa Mwanasiasa na Mkosaoaji Tanzania.Vijana wengi wa CCM wanachekwa Mitaani.