Nchi za Afrika kuleta sampuli zao kuchunguzwa Tanzania

stakehigh

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
40,702
Reaction score
41,213
1615349658472.png

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kuwa kutokana na umahiri wa maabara zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zimeweza kutoa huduma ya upimaji wa sampuli mbalimbali kutoka Katika nchi tofauti za Afrika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ,Adam Fimbo katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo Dar es salaam kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo .

Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa.

"Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo.

Ameongeza kuwa Nchi hizo ni pamoja na Zambia, Lesotho, Malawi, Uganga na Kenya na kwamba hilo limewezekana kutokana na tangazwa na WHO.

Ziara hiyo ya siku tatu imehitimishwa rasmi Machi 5,2021 kwa waandishi wa habari kutembelea maabara ya Dawa na Vifaa Tiba nyongeza kwa kuangalia maabara maalumu ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo kwenye Ofisi zao leo Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza.

CHANZO: Michuzi Blog
 
Tanzania hii badala ya kwenda mbele kisayansi wao wanaturudisha nyuma enzi za mababu na magome ya miti!! haya mpeni mgonjwa wenu basi hizo dawa zenu tuone.
 
Hizo maabara zimeundwa Tanzania ?

Mie hata nadhani tumekuwa wa mwisho kuwa na maabara ya kiwango hiki. Tuna tabia tu ya kukuza mambo!!

Tunaponda mabeberu lakini tunakubali viwango vyao, elimu zao, ujuzi wao! Tuna shida!!
 
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kuwa kutokana na umahiri wa maabara zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zimeweza kutoa huduma ya upimaji wa sampuli mbalimbali kutoka Katika nchi tofauti za Afrika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ,Adam Fimbo katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo Dar es salaam kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo .

Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa.

"Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo.

Ameongeza kuwa Nchi hizo ni pamoja na Zambia, Lesotho, Malawi, Uganga na Kenya na kwamba hilo limewezekana kutokana na tangazwa na WHO.

Ziara hiyo ya siku tatu imehitimishwa rasmi Machi 5,2021 kwa waandishi wa habari kutembelea maabara ya Dawa na Vifaa Tiba nyongeza kwa kuangalia maabara maalumu ya MICROBIOLOGY inayotumika kupima vifaa tiba mbalimbali ikiwemo Barakoa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kuhitimisha ziara ya siku tatu ya mafunzo kwenye maabara za kisasa zilizopo kwenye Ofisi zao leo Dar es Salaam. kushoto Meneja wa Elimu ya Umma na Mawasiliano wa TMDA, Gaudensia Semwanza.

CHANZO: Michuzi Blog
Tumetengeneza vifaa vingine vya kupimia au bado tunapimia vifaa vya mabeberu ambavyo vinapima mbuzi na mapapai?
 
Itakuwa labda wanakuja kujifunza jinsi ya kujifukiza & kupandisha mashetani
 
​
Amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na utaratibu wa kukagua na kuthibisha umahili wa maabara mbalimbali Duniani ambapo kwa nchi za Afrika Tanzania ni moja kati ya nchi chache iliyothibitishwa kuwa na maabara zenye ubora hivyo kupelekea baadhi ya nchi za Afrika kuleta Sampuli zao kwaajili ya kuchunguzwa.

"Kuna viwango vilivowekwa na WHO ukifika hicho kiwango wanakutangaza na kukupa cheti hivyo kupelekea nchi nyingine kutaka kujifunza na kuleta Sampuli zao" amesema Fimbo.
Hawa ni wale WHO tunaowakubali au ni wale tunaowakataa ? AKA Mabeberu?
 
Hongereni sana Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

My take: Sampuli zinazozungumziwa hapa sio za kupima COVID, ni dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
 
Kuna watu yaani mawazo yao yamegandana na kufikiri kuwa kitu kizuri hakiwezi kupatikana Tanzania.
 
Mbona sisi tunapeleka sampuli Kitibiwa Kenya
 
Sarakasi zenu ndizo zinawasumbua ,hivi ninyi mna maabara bora kuliko Kenya,Afrika Kusini,Zambia,Uganda,Malawi,Ghana,Nigeria,Misri,Tunisia,Algeria na hata Senegal? Awamu hii vilaza wengi ukiwemo na wewe mtoa mada.

kwan sisi sio watu
 
Back
Top Bottom