Nchi za Afrika Mashariki inabidi zijifunze demokrasia ya kweli kutoka kwa Wakenya

Nchi za Afrika Mashariki inabidi zijifunze demokrasia ya kweli kutoka kwa Wakenya

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
This is how a small clique of families control Kenya

- Kenya's Presidents Together Before 3 of Them Came into Power

- Jomo Kenyatta (seated) served from 1963-1978.

- Daniel Arap Moi (standing) served from 1978-2002.

- Mwai Kibaki (bending) served from 2002-2013.

- Uhuru Kenyatta (sitting next to his dad) is the current President.

- Also Daniel Moi became a foster father to Uhuru Kenyatta once his old father died.

Mwai Kibaki was already Uhuru Kenyatta’s godfather.

FB_IMG_1592166549974.jpg
 
Kwahivyo hapo walikuwa wanaandikiana mkataba kwamba Jomo Kenyattta afe akiwa madarakani? Tena Moi akiwa makamu rais, sio Jaramogi wala Joseph Murumbi, alafu baada ya miaka 24 ya udikteta wa Moi wakenya wafe kwa wingi wakipigania demokrasia ya vyama vingi?

Kisha baadaye aliyechaguliwa na Moi kama mrithi, Uhuru Kenyatta, ashindwe kwenye uchaguzi pamoja na chama chao cha KANU. Tena na Mwai Kibaki ambaye unasema alikuwa 'godfather' wa Uhuru na ambaye aliunganisha vyama vyote vya upinzani dhidi ya jogoo(KANU)?

Kwenye picha mimi naona rais, mwanawe, makamu wake na waziri wake wa fedha, basi. Hivi unajua kwamba baada ya kifo cha Kenyatta ilibidi Moi asafarishwe kwenye boot la gari kutoka kwake Nakuru hadi Nairobi? Kisha wakamuapisha kwa haraka, kisa wapambe wa Mzee Kenyatta walikuwa wameapa kwamba hatakuwa rais na kwamba watamuangamiza?
 
Kwahivyo hapo walikuwa wanaandikiana mkataba kwamba Jomo Kenyattta afe akiwa madarakani? Tena Moi akiwa makamu rais, sio Jaramogi wala Joseph Murumbi, alafu baada ya miaka 24 ya udikteta wa Moi wakenya wafe kwa wingi wakipigania demokrasia ya vyama vingi? Kisha baadaye aliyechaguliwa na Moi kama mrithi, Uhuru Kenyatta, ashindwe kwenye uchaguzi pamoja na chama chao cha KANU. Tena na Mwai Kibaki ambaye unasema alikuwa 'godfather' wa Uhuru na ambaye aliunganisha vyama vyote vya upinzani dhidi ya jogoo(KANU)? Kwenye picha mimi naona rais, mwanawe, makamu wake na waziri wake wa fedha, basi. Hivi unajua kwamba baada ya kifo cha Kenyatta ilibidi Moi asafarishwe kwenye boot la gari kutoka kwake Nakuru hadi Nairobi? Kisha wakamuapisha kwa haraka, kisa wapambe wa Mzee Kenyatta walikuwa wameapa kwamba hatakuwa rais na kwamba watamuangamiza?
Kenya ipo na wenyewe, ninyi wengine wote ni wapiga kelele na wasindikizaji tu, rais ajaye lazima atatoka katika makabila mawili tu, Jaluo au Kelenjin, Raila au Rutto,

Taja rais wa Tanzania baada ya Magufuli.
 
Kenya ipo na wenyewe, ninyi wengine wote ni wapiga kelele na wasindikizaji tu, rais ajaye lazima atatoka katika makabila mawili tu, Jaluo au Kelenjin, Raila au Rutto,
Taja rais wa Tanzania baada ya Magufuli.
Mmetawaliwa na chama kimoja na sera yao ya kimaskini kwa miongo zaidi ya miine, eti na mpo hapa mkiwapa wakenya mawaidha kuhusu demokrasia. [emoji1]
 
Kenya ipo na wenyewe, ninyi wengine wote ni wapiga kelele na wasindikizaji tu, rais ajaye lazima atatoka katika makabila mawili tu, Jaluo au Kelenjin, Raila au Rutto,

Taja rais wa Tanzania baada ya Magufuli.
Rais wa tanzania si atotoka CCM tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tabiri chama Kenya km wewe mwanaume
 
Rais wa tanzania si atotoka ccm tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tabiri chama kenya km wewe mwanaume
Kwani Kenya kuna vyama vya siasa?, Kenya mnatumia makabila katika siasa hamchagui vyama. Sisi huku tunachagua chama cha siasa, ninyi huko mnachagua makabila ya siasa, Jaluo political party, Kikuyu political Party & Kalenjin Political Party. Hahahaha!
 
Kenya pia imetawaliwa na KANU tangu uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Kenya kuna vyama vya siasa?, Kenya mnatumia makabila katika siasa hamchagui vyama. Sisi huku tunachagua chama cha siasa, ninyi huko mnachagua makabila ya siasa, Jaluo political party, Kikuyu political Party & Kalenjin Political Party. Hahahaha,
Source : Wazalendo TV

KIONGOZI wa chama cha siasa cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amekosoa Bajeti kuu ya serikali na kusema, kila bajeti inapaswa kutafsiri maono, malengo na shabaha, ambazo hazijawahi kuonekana tangu Rais John Magufuli, kuingia madarakani.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, tarehe 14 Juni 2020, Zitto amesema, “tangu serikali ya Rais Magufuli, iingie madarakani, haijawahi kutimiza malengo yaliyowekwa katika bajeti zake.”


Ametoa kauli hiyo, siku tatu baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Philip Mpango, kuwasilisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2020/21.

Akichambua bajeti moja baada ya nyingine – kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2020/2021 – Zitto amesema, kila mwaka serikali imekuwa ikukusanya pungufu ya kile inachokikadiria.

Amesema, “katika bajeti ya kwanza ya Rais Magufuli (2016/2017), serikali serikali ilipanga kukusanya Sh. 29.5 trilioni. Lakini iliishia kukusanya kiasi cha Sh. 25.3 trilioni tu.

“Kushindwa kukusanya kwa kiwango hicho, kukafanya kutokufikia lengo la makusanyo hayo, kwa asilimia 14.33.Ukuzaji huu wa makisio kwa asilimia 31, ni mkubwa sana, ukulinganisha na wastani wa ukuzaji wa makisio ya bajeti wa asilimia 11 katika miaka miwili ya nyuma,” ameeleza.

Amesema, “Sababu kubwa ya serikali ya kushindwa kufikia malengo, ni kuweka makisio makubwa mno bila ushahidi wa takwimu za kutosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.

“Jambo hili lilisababisha ukamuaji mkubwa wa kodi kwa wafanyabishara, jambo ambalo lilisababisha biashara nyingi kufungwa, na hivyo kusababisha athari kubwa kwenye uchumi wa taifa hili.”

Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ilikuwa bajeti ya kwanza ya serikali ya Rais Magufuli.

“Licha ya serikali kutambua makosa yake haya ya kuweka makisio makubwa katika bajeti yake ya kwanza, bado haitaki kubadilika,” ameeleza.

Amesema, “kwa kuanza kushusha kasi ya kupandisha makisio kutoka asilimia 31 mpaka asilimia asilimia 7 mwaka 2017/18; asilimia 2 mwaka 2018/19, asilimia 2 mwaka 2019/2020 na asilimia 4 mwaka 2020/2021, tayari uchumi umeshaharibiwa kwa shughuli za uzalishaji kushuka na hivyo malengo ya makusanyo kuporomoka zaidi kuliko mwaka uliopita.”

Amesema, mwaka 2018/19 jumla ya Sh. 32.5 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya CAG, serikali ilikusanya Sh. 25.8 trilioni pekee na hivyo kutofikia lengo la makusanyo kwa asilimia 21.

Amesema, “mwaka 2019/20 jumla ya Sh. 33.1 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya Dk. Mpango, mpaka Aprili mwaka huu, makusanyo yamefikia Sh. 24.85 trilioni tu, ikiwa imebakia miezi 2 kabla ya mwaka wa fedha kuisha.”

Anasema, mpaka Aprili 2020, lengo la mapato ya kibajeti, halijafikiwa kwa asilimia 25 na kwamba makusanyo ya mapato yote ya serikali katika mwaka 2018/19, yalikuwa madogo kuliko bajeti ya mwaka uliotangulia wa 2017/18.

Kwenye uchambuzi wake huo Zitto anasema, kwa mujibu wa taarifa ya Mwaka ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kamati ya Bunge ya Bajeti, licha ya makadiro na makusanyo halisi yaliyotarajiwa, utekelezaji wa bajeti uko chini ya asilimia 70.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17, bajeti ya serikali ilitekelezwa kwa asilimia 66.5, mwaka 2017/18, asilimia 64.5, mwaka 2018/19 asilimia 68.6 na 2019/2020, ilitekelezwa kwa asilimia 62 pekee.

“Kwa ujumla bajeti zote tano za Serikali ya Awamu ya Tano, baada ya hii ya mwaka 2020/2021 kupitishwa na Bunge, zitakuwa ni jumla ya Sh. 162 trilioni. Je, fedha hizi zinaendana na hali halisi ya maendeleo ya wananchi,” amehoji Zitto.

Amesema, taarifa ya hali ya uchumi wa taifa 2019 iliyotolewa na Dk. Mpango, tarehe 11 Juni 2020, inaonyesha kuwa pato la taifa (GDP) limekua kwa asilimia 7, kama ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Hii maana yake ni kwamba, ukuaji wa uchumi haukuongezeka; bali ulibaki pale pale katika viwango vya mwaka uliopita.

Mwanasiasa huyo kijana amesema, katika miaka hiyo mitano ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali imeshindwa kutumia rasilimali fedha za nchi kuchochea maendeleo kwa wananchi wake

Source : Zitto Kabwe, ‘azitoboa ’ Bajeti 5 za Rais Magufuli
 
Kenya hakuna vyama vya siasa kuna majangili wa siasa, chaguzi ikifika wanaunganisha makundi kushindana, kundi litakaloshinda linaunda selikari na kuanza kunywa chai ya bilioni moja😂😂
 
Kwani Kenya kuna vyama vya siasa?, Kenya mnatumia makabila katika siasa hamchagui vyama. Sisi huku tunachagua chama cha siasa, ninyi huko mnachagua makabila ya siasa, Jaluo political party, Kikuyu political Party & Kalenjin Political Party. Hahahaha,
Usijiumize bure jomba, km ingelikua tunachagua makabila basi kenya kusingelikua na wabunge wahindi..
Sasa kizungu mkuti njoo pande za bongo, yani bila chama huchaguliwi..

Ea nadhani only in kenya mtu anaweza chaguliwa na kushinda kura bila chama, huku akiwa anajisimamia mwnywe tu..
Yani tz ngazi zote za juu ni ccm bana
 
Usijiumize bure jomba, km ingelikua tunachagua makabila basi kenya kusingelikua na wabunge wahindi..
Sasa kizungu mkuti njoo pande za bongo, yani bila chama huchaguliwi..

Ea nadhani only in kenya mtu anaweza chaguliwa na kushinda kura bila chama, huku akiwa anajisimamia mwnywe tu..
Yani tz ngazi zote za juu ni ccm bana
Kenya mlipiga hatua nzuri sana kuruhusu wagombea binafsi, saa nyingine tunashindwa kupata viongozi wazuri kutokana na ubabe na rushwa zilizojaa kwenye hivi vyama vya siasa. Misimamo ya vyama saa nyingine huzengua.
 
Kenya ni muungano wa Wawakilishi wa Makabila kutaka Madaraka.

Bila kuwapata akina Naj Balala na kundi lake kutoka Mombasa hutopata kura za Pwani.

Usipocheza karata zako kumpata Kalonzo au Uhuru au Martha Karua au kwa sasa huyu dogo wa Machakos hapo Central hupati kitu na hii inaenda mpaka Mai mai pia Naivasha

Akina Musalia Mudavadi nao wana uwakilishi wa baada ya JKIA Kipengele na Kajiado mpaka huku Namanga bila kuungana nao na kuahidi madaraka.

Kanda ya Nyanza huku baada ya Kisii Kuja Kurya district mpaka ziwa Victoria bila familia ile ya Kijaluo utakuwa umechimba chini.

Ujinga unaendelea vivo hivo kwa Wakalenjin hadi Malaba huko Ruto na ndugu hawakuelewi.

Nenda kwa Wasomali wa Turkana ni maujinga jinga tu.

Nini cha kuigwa hapo ni ushuzi tu.
Coalitions za kikanda na kikabila hazina nafasi Bongo

Sent from my SM-A520F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom