Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Wakuu wa nchi 13 za Afrika wamekutana Abidjan nchini Ivory Coast na kufanya mazungumzo ya jinsi ya kuhuisha uchumi kutokana na athari za virusi vya corona, kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa ajira.
Mkutano huo umefunguliwa na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast aliyetoa wito kwa Benki ya Dunia kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) kuunga mkono juhudi hizo.
Maazimio ya mkutano huo yamelenga pia kuongeza upatikanaji wa chanjo kwa nchi zote za Afrika, ambapo mpaka sasa ni asilimia 3 tu ya wakazi wote wa Bara la Afrika ndio waliopata angalau dozi moja ya chanjo.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuongezeka kwa vifo duniani kumetokana na ukosefu sugu wa Chanjo pamoja na kuenea kwa aina ya Kirusi cha Delta cha Corona, ambacho mpaka sasa kimekwishasambaa katika nchi 21 barani Afrika.
Rais Ouattara ameiomba Benki ya Dunia kuzipatia nchi za Afrika angalau dola bilioni 100 za Kimarekani (sawa na Tsh. trilioni 231.9) ndani ya kipindi cha miaka mitatu ili kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na Corona.
“Huu ni wasaa mzuri wa kuonesha kuwa mshikamano ndio njia pekee ya kuleta mafanikio kwa wote na kuwa tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kurudisha mwenendo wa ukuaji wa uchumi tuliokuwa nao kabla ya kuzuka kwa janga hili na kujenga dunia yenye maendeleo,” alisema Rais Ouattara.
Kiasi hicho cha fedha, endapo kitapatikana, kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa ya Benki ya Dunia. Mkakati wa ufadhili huo unalenga kuandaa sera itakayotoa mwongozo, kufikia mwishoni mwa mwaka huu, wa miradi maalum itakayolengwa katika nchi 74 zilizopo katika Mpango huo wa Benki ya Dunia, itakayofadhiliwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Viongozi hao pia, kwa kuelewa malengo yao ya kufikia ajenda ya maendeleo, wameangazia umuhimu wa kuongeza njia za ndani na nje za kuongeza upatikanaji wa fedha kwa kuzingatia ongezeko la mahitaji ya kifedha ya Bara hili, kufikia kiasi cha dola bilioni 285 (sawa na Tsh trilioni 660.9) ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa lengo la kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, mabadiliko ya hali ya hewa na kuhuisha uchumi, wakikadiria kuwa juhudi za ndani za kutafuta kiasi hicho cha fedha zinaweza zisizae matunda yaliyokusudiwa, hivyo wameiomba Benki ya Dunia kufanikisha upatikanaji wa dola milioni 100 kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 ili kufanikisha malengo yao.
Chanzo: VOA, Benki ya Dunia