Nchi za Afrika zaongoza orodha ya wanaositisha mikataba na kampuni za China

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali ya Uganda imesitisha mkataba wa Dola Bilioni 2.2 (Tsh. Trilioni 5.1) wa Kampuni ya CHEC ya China kujenga reli ya Standard Gauge Railway (SGR) ya Kilometa 273 kutoka Malaba hadi Kampala kutokana na mvutano wa kimaslahi.

Hivyo, Uganda imeingia makubaliano ya awali na Kampuni ya Uturuki ambayo ndiyo inayojenga SGR ya Tanzania ikidaiwa gharama zao zinaweza kuwa ni Dola Bilioni 1.5 hadi 1.72 (Tsh. Trilioni 3.5 hadi 4).

Huo ni mwendelezo mbaya wa mikataba ya China katika mataifa mbalimbali kwa hivi karibuni. Ghana pia ilisitisha mkataba wa matengenezo ya mfumo wa kuangalia magari.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ameagiza kupitiwa kwa mkataba wa madini uliosainiwa Mwaka 2008 akidai haridhishwi na utendaji.

Mwaka 2022, Kenya ilitisisha mkataba wa ujenzi wa SGR.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins katika utafiti wa China-Afrika wa Mwaka 2000 - 2019, China ilisaini mikataba ya 1,141 ya kutoa mikopo yenye thamani ya Dola 153.

Aidha, Mexico pia imefuta mkataba wa ujenzi wa treni ya mwendokasi.

Ethiopia nayo imefuta mkataba wa gesi, mafuta uliosainiwa Mwaka 2013.

Source: aa.com, BBC, business-standard
 
Hii imesitishwa baadaya wanaharakati kupiga kelele eti kwani Tanzania inenge km 2100 Kwa usd 2billions na Uganda itumie 2B kuke ga km 273
 
Sinohydro atatuharibia miundombinu yetu
 
Serikali ya Uganda imesitisha mkataba wa Dola Bilioni 2.2 (Tsh. Trilioni 5.1) wa Kampuni ya CHEC ya China kujenga reli ya Standard Gauge Railway (SGR) ya Kilometa 273 kutoka Malaba hadi Kampala kutokana na mvutano wa kimaslahi.

Hivyo, Uganda imeingia makubaliano ya awali na Kampuni ya Uturuki ambayo ndiyo inayojenga SGR ya Tanzania ikidaiwa gharama zao zinaweza kuwa ni Dola Bilioni 1.5 hadi 1.72 (Tsh. Trilioni 3.5 hadi 4).

Huo ni mwendelezo mbaya wa mikataba ya China katika mataifa mbalimbali kwa hivi karibuni. Ghana pia ilisitisha mkataba wa matengenezo ya mfumo wa kuangalia magari.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ameagiza kupitiwa kwa mkataba wa madini uliosainiwa Mwaka 2008 akidai haridhishwi na utendaji.

Mwaka 2022, Kenya ilitisisha mkataba wa ujenzi wa SGR.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins katika utafiti wa China-Afrika wa Mwaka 2000 - 2019, China ilisaini mikataba ya 1,141 ya kutoa mikopo yenye thamani ya Dola 153.

Aidha, Mexico pia imefuta mkataba wa ujenzi wa treni ya mwendokasi.

Ethiopia nayo imefuta mkataba wa gesi, mafuta uliosainiwa Mwaka 2013.

Source: aa.com, BBC, business-standard
Na bidhaaa za China vipi uganda wamesusia?Tanzania ndio unaweza zania uko china make kila kitu ni China
 
Back
Top Bottom