Nchi za Jumuiya ya Ulaya ni janga kuu la maendeleo la nchi za Afrika

Nchi za Jumuiya ya Ulaya ni janga kuu la maendeleo la nchi za Afrika

Joined
Aug 20, 2021
Posts
24
Reaction score
18
Najaribu sana kufikiria, je Afrika utapataje maendeleo endapo Kila kitu ambacho tunachotaka kufanya cha maendeleo yetu ulaya inapinga, inatoa vijisababu vya ajabu ajabu mpaka unakosa majibu Nia Yao ni nini hawa jamaa.ninachokiona hawa wazungu hawana mpango mzuri na watu wa Afrika.

Haiingii akilini, rejea bwawa la umeme la Ethiopia, bwawa la Nyerere pale rufiji walivyo yapinga kwa visingizio vya mazingira na kuhalibu makazi ya wanyama wa mwituni, na sasa wameingia kwenye bomba la mafuta ghafi la Uganda na Tanzania kwa visingizio vilevile vya uchafuzi wa mazingira,hivi kati ya wao na sisi ni nani anaechafua mazingira zaidi!?

Ninani anae miliki maviwanda makubwamakubwa yanayotoa Moshi Moshi angani muda wote kama sio wao, watuache tutengeneze Afrika tunayoitaka sisi,ukoloni mamboleo kwa sasa hauna nafasi.ni swali la kujiuliza je tuendelee kuupokeo ukoloni wao mamboleo au tuwakatalie?

Ni swala la uamuzi tu

4bv50069dbb8a61l4um_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom