Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Hapa najiuliza kwa nini mwendazake akuuweka wazi mkataba wa bandari ya bagamoyo ili nasi tuuone ulivyo wa ovyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeulizia swali zuri na la kitaalam. Kwa jinsi alivyokuwa anapenda sifa,angeuweka wazi ingependeza. Pili,nadhan alitaka kuonyesha umma ni jinsi gani awamu iliyopita ilikuwa haifai Kama ambavyo na yeye anavyokosolewa in absentia!!! MWOSHA HUOSHWA!!;
 
Mara kwa mara tumekua tunazungumzia ujasusi wa kiuchumi ! Je nyumbani mmewekeza kweli huko??

Sababu tunayaona hayo kwa watu huku uzalendo huanzia chini na hasa ulinzi wa nchi huanzia kwa mtu mmoja mmoja na huu ndio uzalendo halisi ..

Tanzania uzalendo tafsiri yake ni kuipenda Serikali ya CCM haijalishi nani yuko madarakani...

Asilimia 90% ya mabalozi wetu balozi za nje ni either Majasusi au wale waambata wao ila je wanafaidishaje nchi na ujasusi au ndio wanavuta familia zao ziende kula maisha kwa chances walizotengeneza?
 
Siamini mimi binafsi kama taifa la nje linaweza kuwa na uwezo wa kuingilia mambo binafsi ya nchi nyingine, hao mabeberu kweli tunawasingizia vingi, adui yetu ni tamaa ya viongozi wetu wenyewe, huyo mzungu akitaka uranium aje tukae chini tuzungumze bei tutanufaika vipi simple, lakini kunitisha sijui kitu gani naachana nae, hizi rasilimali tunazitumia haraka haraka kwa kiherehere chetu ndio maana tunazitoa hovyo mwishowe hatuoni manufaa yake kwa wananchi., akigoma mzungu mmoja atakuja mwingine shida iko wapi mali haiozi chini ya ardhi.
Mataifa ya nje khasa mataifa makubwa wana uwezo mkubwa wa kuingilia mataifa madogo kwa njia mbalimbali.

Njia mojawapo ni ya ujasusi.

Mwaka 2016, niliongelea hili suala la ujasusi wa kiuchumi na kiteknolojia kupitia hapa: Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari
 
LOOoo, unachosha sana na mizunguko isiyokuwa na maana aiseee!
Para mbili tatu zingetosha kabisa kueleza kitu.

Haya, 'source' yako ya haya mambo ni ipi?

Haya mambo ya kukazania 'Mabeberu,.... mabeberu' kila wakati na kusahau kuwasilisha habari muhimu ya taarifa inazingua sana.

Sasa sijui hapa kijadiliwe kipi, mabeberu, au njia tunazoweza kuzifanya tunufaike na hizi mali zetu?

Utanisamehe kama nitakukwaza kwa haya niliyoandika, lakini ukweli nimekwazwa na njia yako ya uwasilishaji wa habari yenyewe, ambayo nadhani ni habari muhimu.

Andiko la Hovyo kabisa nililopata kusoma!

Embu jaribu kusoma hii, pole pole utapata maana.

 
Mataifa ya nje khasa mataifa makubwa wana uwezo mkubwa wa kuingilia mataifa madogo kwa njia mbalimbali.

Njia mojawapo ni ya ujasusi.

Mwaka 2016, niliongelea hili suala la ujasusi wa kiuchumi na kiteknolojia kupitia hapa: Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari

Unaonekana ni mzuri wa kusoma vitabu vya kijasusi, ana kuangalia filamu za kijasusi. Sasa ukipandwa na hizo hisia ndio unatengeneza habari za kufikirika kama hizi. Toka wakoloni wameondoka katika nchi hii, ni lini hao mabeberu wamewahi kurudi kuchukua rasilimali zetu kwa njia za kijasusi, bila kuingia mkataba na hawa hawa viongozi wetu wezi wa kura? Acha story za kwenye vijiwe vya wachovu, huenda kuna mahali huko mtaani huwa unawapigia hizi story, na wanakuona unajua mambo kumbe ni muhuni tu.
 
Wajinga kama wewe wamebaki wachache, hawajaondoka na ardhi, kwa nini usitengeneze ramani yako! Kauli ya mabeberu ni ya kuficha udhaifu wako na aliitumia jiwe kuficha mapungufu yake!
 
WIN WIN SITUATION ndio mpango mzima sio WanaCCM wahongwe Nchi iingizwe kwenye umasikini na Madeni ya kutisha
 
Namuunga mkono mtoa mada,tatizo kubwa ni tamaa walizonazo viongozi wetu. Wazungu/Wachina wanapo taka kutuibia, kuna viongozi wetu wakubwa hupiga pesa ya pembeni ili kuhakikisha hao mabwana wanapata mkataba nafuu wa kutuibia. "Washaurini wakubali asilimia 10-15, mkifanikisha hili kuna billioni 5 cash zenu kama shukrani kwa kufanikisha huu mkataba" Hapa ndipo viongozi wengi huldanganyika na kusaini mikataba ya ajabu. Hata sisi tunao walaumu ni vigumu sana kukataa kitita hicho cha pesa.
 
Unaonekana ni mzuri wa kusoma vitabu vya kijasusi, ana kuangalia filamu za kijasusi. Sasa ukipandwa na hizo hisia ndio unatengeneza habari za kufikirika kama hizi. Toka wakoloni wameondoka katika nchi hii, ni lini hao mabeberu wamewahi kurudi kuchukua rasilimali zetu kwa njia za kijasusi, bila kuingia mkataba na hawa hawa viongozi wetu wezi wa kura? Acha story za kwenye vijiwe vya wachovu, huenda kuna mahali huko mtaani huwa unawapigia hizi story, na wanakuona unajua mambo kumbe ni muhuni tu.
I'm humbled.

Huwa wapenda sana personal attacks lakini nilikwishakusamehe mara 70.

Hicho kitabu si cha kijasusi.

Mwandishi amezunguka dunia na akafika hadi Zanzibar ndipo akapata wazo la kuandika Hicho kitabu, great.

Mimi si mtu unaenidhania kabisa ila nashukuru Mungu nimesoma.

Lakini nahisi pia ukinifuatilia nina uwezo wa kuona mbali ila si kwa ramli.

Sasa soma uzuri na uelewe sijamtaja marehemu JPM katika mada yangu ila mada yazungumzia jinzi ilivyo ngumu kuzuia rasilimali zetu kuchukuliwa kwa njia yoyote ile.

Kwani nchi za mabeberu tayari wana ramani yote ya Afrika na ukanda huu ambao ndo una nchi hizo tatu ndo unoangaliwa zaidi.

Pamoja na hayo zote twapaswa kutulia na kuona jinsi historia inaweza kuandikwa kisha, kufutwa na kuandkwa upya.

Kitendo hichi chatokezea hapa Tanzania.

Ila kwa sasa relax au chill na punguza jazba tuendeleze kasi ya maendeleo.
 
Nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ni nchi muhimu katika mstakabali mapinduzi ya viwanda barani Ulaya na Marekani.

Mwaka 2020 Uingereza walitangaza kuachana na magari yatumiayo mafuta ya diseli na petroli kufikia mwaka 2030 na wameazimia kuanza kutengeneza magari zaidi yatumiayo betri.

Hata hivyo tayari magari yatumiayo betri tayari yanatengenezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Nchi za kibeberu au maadui wa maendeleo hawawezi kuiruhusu Tanzania iendelee kwa kuwa na viwanda vyake .

Pia Tanzania ina malighafi zote kutengeneza hata seti za televisheni, vioo vya madirisha na balbu.

Kuna mambo matatu makuu ambayo sisi binadamu twapaswa kufahamu.

Mambo hayo ni technical know what, technical know how and technical know why.

Darasani mwalimu hutufundisha kuhusu somo la jiografia, kisha kuingia ndani kufanya tathmini kutumia kifaa maalum cha Compass kwa kutumia ramani na hiyo ni technical how.

Pale uanzapo kujiuliza hii Compas imetengezwa vipi ndipo unapoingia kwenye technical know why.

Mabeberu wanakuambia kuwa Afrika kuna dhahabu tatu ambazo ni Tanzania, Angola na Congo DRC.

Mabeberu wanaendelea kuziangalia nchi tatu ambazo nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ambazo wana malengo ya muda mrefu hadi miaka 50.

Katika nchi hizo ni Tanzania ambayo wao mabeberu wana uwezo wa kuingia na kujichotea maliasili watakavyo.

Kutokea bandari ya Lobito iliopo Benguela kupitia Lusaka, Lubumbashi ni ukanda maalum ulojaa madini, mafuta na madini ya uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi na mabomu ya nyuklia na mitambo yake.

Lango kuu la kuingia kwenda huko ndani au (interior) na kutokea ni Bagamoyo na ni njia rahisi kuliko kuzunguka Cape Town.

Ila mabeberu hao wakadai kuwa watakuja kwa mazungumzo na ikiwa mazungumzo yatashindikana basi watatumia mbinu zozote kuhakikisha wanafanikiwa azma yao.

Wazungu hao wanasema kuwa Tanzania ni nchi ya kuingia na kutokea Afrika kupitia Bagamoyo. Pia wanasema kuwa asilimia 60 ya biashara ya meli kuanzia mwaka 2050 itakuwa ndani ya bahari ya Hindi na hiyo ndio itakuwa Ocean of the future.

Hivyo, meli yaweza kutoka bandari ya Lobito kupitia Dar-es-Salaam hadi mfereji wa Suez bila shida na kwa uharaka zaidi.

Na hivyo ndivyo mfalme Leopold wa pili wa Belgium alivyokubaliana na wakoloni wa kijerumani kujenga reli ya kati ambayo ingesafirisha bidhaa zote za malighafi kutoka katikati ya Tanzania na Afrika kuelekea bahari ya Hindi.

Mfalme huyo alikuwa akivuna zao la mpira na kulisafirisha kwenda Ulaya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama matairi ya magari, baiskeli na zingine yaani alikuwa "supplier" mkubwa.

Waafrika wengi sana raia wa Congo walikufa wakivuna zao hilo na wengine kukatwa mikono kwa kushindwa kufanya hivyo.

Bahari ya Hindi ni bahari ilojaaliwa kila aina ya maliasili kuanzia mafuta, gesi asilia na uranium. Leo hii twashuhudia jinsi magaidi wa kupandikizwa nchini Msumbiji wakitumika kama kivuli cha wizi wa maliasili hizi zinazoibwa usiku na mchana.

Mwandishi Robert Kaplan katika kitabu chake cha Monsoon - "The India Ocean and Future of American Power" anaitaja bahari ya Hindi kama New Great Game kama ndo njia ya China ikitumia meli zake kubwa za mafuta kusaka maliasili hiyo ndani ya bahari ya Hindi.

Lakini safari hii upo uwezekano mkubwa wa vita ndani ya bahari hiyo baina ya nch iza kibeberu yaani Marekani na China.

Kaplan anaelezea muungano wa nchi za Marekani, China na India katika bahari ya Hindi katika kufanya biashara, kuzuia vitendo vya utekaji meli yaani Piracy, kulinda njia za usafiri wa meli na kuitikia wito wa majanga ndani ya bahari hiyo.

Bila shaka kelele za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni moja ya vielelezo vya mpango wa nchi za kibeberu.

Mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ulofumuliwa na hayati John Magufuli haukuwa mkataba uloweka maslahi ya taifa mbele na ulikuwa ni wa miaka 99.

Mkataba huo pia haukuwa unaruhusu maendelezo yoyote ya bandari zingine kama bandari ya Dar-es-Salaaam, Tanga, Zanzibar.

Hiyo ni kwasababu Bagamoyo ndo lango kuu la kuingiza na kutoa rasilimali zote zinatoka ndani ya Tanzania na maliasili zingine zinazotoka ndani ya Congo DRC na Angola.

Kwa vile nchi za kibeberu tayari wana ramani ya Afrika na sehemu zilipo maliasili basi Tanzania pamoja na Angola na Congo DRC na wanafahamu kuwa sasa hivi ujazo wa Uranium na madini mengine umefikia kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuvunwa, basi sisi hatuna ujanja.

Tanzania tunapaswa kueleza wazi msimamo wetu na pia kueleza ni nini tunataka kwani mali tunayo.

Tanzania haina budi kulinda ukanda wa bahari ya Hindi hadi Msumbiji kuhakikisha usalama wake hauingiliwi kirahisi. Serikali pia inawajibika kueleza msimamo wake kuhusiana na mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Lakini si kuanza kuzunguka mbali na kuanza mijadala ya kupoteza muda huku tayari wenzetu wachache wamekaa tayari na mabeberu na wamepanga nini kinachofuata.

La sivyo tunakubali kuwa sie ni waangalizi tu wa rasilimali tulozikalia na tupo tayari kuzigawa bure au kwa ujira kiduchu.
HIZI STORY ZILIKUWA ZA MIAKA YA 60, ETI WAZUNGU WANAIONEA WIVU TANZANIA..MFYUUUU!

FUNGENI MIPAKA NA VIWANJA VYA NDEGE NDIO UJUE NANI ANAMHITAJI MWENZIE.

WEWE UNA AKILI ZA KIMAGUFULI LICHA YA WAZUNGU KUMUWEKEA BETRI KWENYE MOYO ILI ASIFE ILA BADO ALIKUWA ANAWATUKANA..magofool!
 
I'm humbled.

Huwa wapenda sana personal attacks lakini nilikwishakusamehe mara 70.

Hicho kitabu si cha kijasusi.

Mwandishi amezunguka dunia na akafika hadi Zanzibar ndipo akapata wazo la kuandika Hicho kitabu, great.

Mimi si mtu unaenidhania kabisa ila nashukuru Mungu nimesoma.

Lakini nahisi pia ukinifuatilia nina uwezo wa kuona mbali ila si kwa ramli.

Sasa soma uzuri na uelewe sijamtaja marehemu JPM katika mada yangu ila mada yazungumzia jinzi ilivyo ngumu kuzuia rasilimali zetu kuchukuliwa kwa njia yoyote ile.

Kwani nchi za mabeberu tayari wana ramani yote ya Afrika na ukanda huu ambao ndo una nchi hizo tatu ndo unoangaliwa zaidi.

Pamoja na hayo zote twapaswa kutulia na kuona jinsi historia inaweza kuandikwa kisha, kufutwa na kuandkiwa upya.

Kitendo hichi chatokezea hapa Tanzania.

Ila kwa sasa relax au chill na punguza jazba.

Ni wapi kwenye post yangu nimemtaja JPM, au unajishuku? Hivi Richard umetuchukulia sisi humu jukwaani ni kama hao wa kwenye vijiwe vya alkasusu? Ramani ya dunia hii ni kitu adimu, mpaka useme kuna mtu anayo as if ni kitu adimu sana? Mimi hapa nina ramani ya dunia nzima, na rasilimali, viwanda, majengo mbalimbali ndani vya dunia hii. Je hiyo ni ishara kuwa nataka kwenda kuchukua utajiri wa maeneo hayo? Nimekuuliza wakoloni wameondoka hapa nchini miaka 60 iliyopita, ni lini wamewahi kurudi kuchukua madini yetu kijasusi bila kuingia mikataba na viongozi wetu? Richard achana na hizi hekaya kama za mtu aliyechanganyikiwa.
 
Mauzo ya madini enzi za mkoloni, wakati ule bado walikua wanamuamini Mungu na 10% waliyoturudishia ilikua kama zaka
Mkuu at least mjerumani ametuachia reli,madaraja n.k,muingereza alipoingia alichota tu mali zetu,hamna alichotujengea yule selfish
 
Namuunga mkono mtoa mada,tatizo kubwa ni tamaa walizonazo viongozi wetu. Wazungu/Wachina wanapo taka kutuibia, kuna viongozi wetu wakubwa hupiga pesa ya pembeni ili kuhakikisha hao mabwana wanapata mkataba nafuu wa kutuibia. "Washaurini wakubali asilimia 10-15, mkifanikisha hili kuna billioni 5 cash zenu kama shukrani kwa kufanikisha huu mkataba" Hapa ndipo viongozi wengi huldanganyika na kusaini mikataba ya ajabu. Hata sisi tunao walaumu ni vigumu sana kukataa kitita hicho cha pesa

Tatizo ni lilelile umaskini na kupenda 10%
 
Back
Top Bottom