Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Nitajie beberu mmoja tu ambaye Tanzania haina ushirika naye na ambaye tunapaswa kutokuwa na uhusiano naye kwa ubaya alionao. Taja beberu mmoja tu tafadhali
 
Ukiona mtu anatumia sana neno 'mabaleberu', uwe na mashaka naye sasa juu ya uelewa wake kuhusiana develipment na civilization dynamics za Dunia.

Sidhani kama kuna content kwenye hii mada inayopnekana inastahili kujadiliwa na great thinkers.

Imekaa kama ndoto isiyoeleweka imeanzia wapi na inashia wapi. Haina hata source wala analysis yoyote. Ni hadirhi ya kufikirika.

ECONOMY ECONOMICS

10 Countries With The Most Natural Resources

FACEBOOK

TWITTER

LINKEDIN

By

CRAIG ANTHONY

Updated Jun 25, 2019

TABLE OF CONTENTS

CLOSE

10. Australia

9. The DRC

8. Venezuela

7. The United States

6. Brazil

5. Russia

4. India

3. Canada

2: Saudi Arabia

1: China

Natural resources or commodities are the raw inputs used to manufacture and produce all of the products in the world. These resources are found in the earth including those extracted from the earth and those that have yet to be extracted. They grow naturally without any help from humans. Commodities are either renewable or nonrenewable. Renewable resources are those whose supply is infinite—such as solar power—while nonrenewable ones have a limited supply and can no longer be used once the supply is exhausted like

Tanzania na Angola are not even among the top 10.
Wewe waongelea kiujumla.

Mimi nimeongela specifics yaani maeneo husika, logistics na future economic war zone.

Lengo la hawa wakubwa ni kupunguza influence ya mmojawao yaani China kwa Afrika.

Hii ni geopolitics sasa tumeingia new era.
 
Nitajie beberu mmoja tu ambaye Tanzania haina ushirika naye na ambaye tunapaswa kutokuwa na uhusiano naye kwa ubaya alionao. Taja beberu mmoja tu tafadhali
Mabeberu wote tunao ushirikiano lakini wa kutoaminiana kwenye masuala fulani.

Hii ni kwasababu tunapokea misaada yao na wakti huohuo twazungumza vingine kuonyesha ukigeugeu wetu.

Ndo maana nchi zote za kibeberu hutazama ni kiongozi yupi awafaa wao kwa ushirikiano na asiwe hardliner au asie na chembechembe za kijamaa.

Kiongozi wa aina hiyo hatakiwi na mabeberu.

Siwezi taja nchi moja moja kwani nchi hizi zina foreign policy ambazo hazitofautiani sana.

Nchi za kibeberu ni zote huitwa imperialist powers.
 
Mkuu 'eliakeem', kwa kusoma tu kichwa cha habari ya andiko hilo, tayari nimekwishatambua ni habari ya aina ambazo kikawaida huwa sizipi uzito sana.
Lakini nakuahidi, nitatafuta muda niisome hiyo habari, baada ya hapo ntakupa mrejesho juu yake.

Bro never miss to read it. It's the evidence based article. You will wonder how this world go.
Duniani kuna mambo mengi sana.
 
Acha uongo wewe! Mikataba yote ya maliasili za nchi inafichwa hata Wabunge hawaioni. Kwanini unaandika uongo kiasi hiki? MABEBERU waliwahi kuingia nchini na majeshi yao ili kutupora rasilimali hizo? Jibu ni kwamba tuna Viongozi Wapumbavu, wezi na mafisadi ambao wakishikishwa kitu basi maslahi ya Taifa hawayajali kabisa.
Wabunge mwaka 2000 walikuja juu ili kutaka kuiona mikataba ya dhahabu au wangekwamisha bajeti yote. Mkapa alifunga safari na kufanya kikao cha siri na Wabunge wa maccm ambao nao walikuwa wamegoma kupitisha bajeti bila kuona mkataba. Baada ya kikao cha siri Wabunge wa maccm wakawageuka Chadema ná kupiga ukelele wao wa ndiyooooooo. Acha kuwa muongo kiasi hiki.
Hata hiyo mikataba tukipewa tuisome yachosha hivyohivyo na ndo twaishia kusaini bila kusoma hadi mwisho na kuelewa.
 
Acha uongo wewe! Mikataba yote ya maliasili za nchi inafichwa hata Wabunge hawaioni. Kwanini unaandika uongo kiasi hiki? MABEBERU waliwahi kuingia nchini na majeshi yao ili kutupora rasilimali hizo? Jibu ni kwamba tuna Viongozi Wapumbavu, wezi na mafisadi ambao wakishikishwa kitu basi maslahi ya Taifa hawayajali kabisa.
Wabunge mwaka 2000 walikuja juu ili kutaka kuiona mikataba ya dhahabu au wangekwamisha bajeti yote. Mkapa alifunga safari na kufanya kikao cha siri na Wabunge wa maccm ambao nao walikuwa wamegoma kupitisha bajeti bila kuona mkataba. Baada ya kikao cha siri Wabunge wa maccm wakawageuka Chadema ná kupiga ukelele wao wa ndiyooooooo. Acha kuwa muongo kiasi hiki.
Je, wakti ule awamu ya 3 na 4 si kuna mikataba ambayo ilibidi watu waende London na miji mingine ambako ndiko walisaini au umeamua kusahau?
 
Tanzania kwa sasa ni ya pili Afrika kwa kuzalisha dhahabu pekee baada ya Afrika Kusini.

Wafahamu hilo?
Ndugu yangu hiyo habari umeiokota wapi. Tanzania katila miaka ya karibuni kwenye uzalishaji dhahabu imeshuka sana.

Wazalishaji wakubwa wa dhahabu Afrika:

1. Ghana
2. South Africa
3. Sudan
4. Mali
5. Burkina Faso

From Ghana to Burkina Faso we profile the leading gold producers across the African continent.

Ghana – 142.4 tonnes. ...

South Africa – 118.2 tonnes. ...

Sudan – 76.6 tonnes. ...

Mali – 71.1 tonnes. ...

Burkina Faso – 62 tonnes.

28 Aug 2020

Home - NS Energy › ...

Top five gold mining countries of Africa from Ghana to Burkina Faso

Wakati wa uongozi wa awamu ya 5, Tanzania imeanguka kwenye ukuaji wa sekta zote za uchumi. Bahati mbaya Watanzania wengi hawaujui ukweli huu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Seven hundred years ago; and then, what happened?

Surely I have come across something like this before. Why didn't it hit me hard as it has done now?

We should read more of this!

And a massive library [emoji432]
What went wrong?
That’s the question
Mkuu watu wanaanini kuwa wazungu wanatubania vingi ila ukweli ujinga wa baadhi ya viongozi na wanaopenda kujimilikisha mali bila kuangalia maslahi ya Taifa ndio tatizo

Tunaweza kufanya mengi sana kama tutaamua kwa uadilifu na kufuata sheria madhubuti
Mwizi wa kuku anapewa adhabu kali ila anaeiba billions na kuibaka katiba anatamba
 
Sasa kwenda huko ni kuruhusu Wabunge kuiona mikataba au MABEBERU waliwapiga na kuwatisha hao walioenda ili wakubali kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Taifa? Acha KUKURUPUKA na kuandika uongo. Viongozi mafisadi na majizi na Bunge DHAIFU ndiyo chanzo cha huo upumbavu.
Je, wakti ule awamu ya 3 na 4 si kuna mikataba ambayo ilibidi watu waende London na miji mingine ambako ndiko walisaini au umeamua kusahau?
 
Ndugu yangu hiyo habari umeiokota wapi. Tanzania katila miaka ya karibuni kwenye uzalishaji dhahabu imeshuka sana.

Wazalishaji wakubwa wa dhahabu Afrika:

1. Ghana
2. South Africa
3. Sudan
4. Mali
5. Burkina Faso

From Ghana to Burkina Faso we profile the leading gold producers across the African continent.

Ghana – 142.4 tonnes. ...

South Africa – 118.2 tonnes. ...

Sudan – 76.6 tonnes. ...

Mali – 71.1 tonnes. ...

Burkina Faso – 62 tonnes.

28 Aug 2020

Home - NS Energy › ...

Top five gold mining countries of Africa from Ghana to Burkina Faso

Wakati wa uongozi wa awamu ya 5, Tanzania imeanguka kwenye ukuaji wa sekta zote za uchumi. Bahati mbaya Watanzania wengi hawaujui ukweli huu.
Nilikuwa namaanisha reserve ya dhahabu na si uzalishaji
 
Kanuni kuu ya ubepari na hasa ubepari wa kidola ni kuhakikisha kuwa kiwango cha umasikini wa kipato unaendelea kuwa Kati ya asilimia 70 na 80. Juhudi zozote za kupunguza kiwango cha umasikini chini ya hapo, popote pale Duniani ni tishio kwa ubepari na hivyo mabepari watafanya lolote linalowezekana kudhibiti mabadiliko hayo, ikiwemo kuzalisha vibaraka.
 
Sasa kwenda huko ni kuruhusu Wabunge kuiona mikataba au MABEBERU waliwapiga na kuwatisha hao walioenda ili wakubali kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa Taifa? Acha KUKURUPUKA na kuandika uongo. Viongozi mafisadi na majizi na Bunge DHAIFU ndiyo chanzo cha huo upumbavu.
Hizi nchi hazikupigi wala kukutisha ila hukuanzia mbali sana.
 
Acha ujinga wako. Nchi kama Namibia na Botswana zinafaidika sana na mikataba yao ya rasilimali kwanini isiwe Tanzania? Uongo wako peleka kwingine siyo humu.
Hizi nchi hazikupigi wala kukutisha ila hukuanzia mbali sana.
 
Kiwango cha elimu waliyokuwanayo wakati wanatutawala kilikua ni cha juu sana kulinganisha na uelewa wetu wa mambo. Wakiona udongo tu wanafahamu madini yanayopatikana katika udongo ule.

Kuna siku mmoja nilimjonyesha picha ya Tanzania sehemu yenye udongo mwekundu. Aliniambia chini ya hii ardhi kuna copper nyingi sana.
Hapa Kibondo na Kasulu zinahusika, sio kwa dongo lile jekundu.
 
Mimi nimeongela specifics yaani maeneo husika, logistics na future economic war zone.

Lengo la hawa wakubwa ni kupunguza influence ya mmojawao yaani China kwa Afrika.

Hii ni geopolitics sasa tumeingia new era.
Mistari hii mitatu inaeleweka sana, na ina maana haswa.

Andiko, kama kweli ni lako, hukulitendea haki mkuu.

Umelivurugavuruga sana na mambo mengi yasiyoendana, tena kwa sehemu tofauti tofauti katika andiko lenyewe.

Hii mistari yako mitatu hapa..., ngoja nikuongezee ushahidi wa unayoyasema:

Maongezi ya hivi karibuni, kati ya Biden na BoJo kwenye simu, huku Biden akimhimiza BoJo na wao waanzishe kitu kama kile alichokifanya Jinping, the "Belt and Road". $650 Billion ikiwa kianzio cha juhudi hizo za kumpiku Jinping.

Na pia usisahau juhudi za yule Magufuli wa U'beparin' (Trump); hata yeye alikuwa kwenye mbio hizo hizo, ndio maana akina Uhuru Kenyatta wakaitwa White House, na akina Betchell wakitaka kujiingiza na barabara ya Nai-Momba, ili kupunguza nguvu za SGR ya mchina.

Haya mambo yapo sana, lakini tunatakiwa tuwe na ufahamu nayo vizuri, tusiwe watu wa kupiga tu kelele za "Mabeberu..., mabeberu", huku hata kuelza watu waelewe inatuwia vigumu.

Maana hasa ya kutumia neno hilo mara kwa mara kunaondoa uzito wake. Inabaki kama njia ya kuwatishia watu tu... wakimbie; hata bila ya kueleza sababu za ubeberu wenyewe tunaouona ukipangwa.

Sasa sijui kama utanielewa hapa, lakini nimejaribu kujieleza kadri niwezavyo. Nitajaribu njia nyingine kama bado sieleweki.

Ndio, mambo haya yapo
 
Unaonekana ni mzuri wa kusoma vitabu vya kijasusi, ana kuangalia filamu za kijasusi. Sasa ukipandwa na hizo hisia ndio unatengeneza habari za kufikirika kama hizi. Toka wakoloni wameondoka katika nchi hii, ni lini hao mabeberu wamewahi kurudi kuchukua rasilimali zetu kwa njia za kijasusi, bila kuingia mkataba na hawa hawa viongozi wetu wezi wa kura? Acha story za kwenye vijiwe vya wachovu, huenda kuna mahali huko mtaani huwa unawapigia hizi story, na wanakuona unajua mambo kumbe ni muhuni tu.
Afu ww umezidi matusi sana hapa jamvini, alafu hunaga mambo ya maana ni upumbavu tu na kulobulobu kwenye hoja
 
And a massive library [emoji432]
What went wrong?
That’s the question
Mkuu watu wanaanini kuwa wazungu wanatubania vingi ila ukweli ujinga wa baadhi ya viongozi na wanaopenda kujimilikisha mali bila kuangalia maslahi ya Taifa ndio tatizo

Tunaweza kufanya mengi sana kama tutaamua kwa uadilifu na kufuata sheria madhubuti
Mwizi wa kuku anapewa adhabu kali ila anaeiba billions na kuibaka katiba anatamba
"Tunaweza kufanya mengi sana kama tutaamua kwa uadilifu na kufuata sheria madhubuti"

"...watu wanaamini kuwa wazungu wanatubania vingi, ila ukweli 'UJINGA' wa baadhi ya viongozi na wanaopenda kujimilikisha mali bila kuangalia maslahi ya Taifa ndio tatizo"

Hii mistari miwili na nusu inaniumizaga sana roho yangu.

Halafu unakuja humu JF, unakutana na michango ya kuchefua kabisa...; usipoangalia unakufa kwa 'stress'.

Lakini inasikitisha sana kwamba miaka yote hii 60 na zaidi sasa, inakuwa kama tunarudi kinyumenyume.
 
Back
Top Bottom