Nchi za mabeberu wana Ramani zinazoonyesha maliasili ilipo Tanzania na nchi nyingine mbili. Wao wanaamini walitukabidhi tuwatunzie lakini si zetu

Acha ujinga wewe utakosaje jazba huku ukiona madudu ya kutisha miaka nenda miaka rudi watu wanadhulumiwa, wanalawitiwa, wanauawa, wanapigwa risasi mchana kweupe, wanaporwa ubunge wao, trillions za walipa kodi zinaibiwa zinafisadiwa halafu unataka nisiwe na Jazba? Miaka 60 ya uhuru nchi inazidi kurudi nyuma kwenye kila sekta. Toa upumbavu wako hapa.
Eti unamuheshimiu Prof Assad wakati huo huo alipofukuzwa kama mbwa na jiwe hukutia neno. Acha ujinga wako!!!

Mkuu, punguza jazba, mwisho wa siku huu mjadala utaisha.

I respect Mr Assad ambae mara mojamoja huwa namsikiliza pale kijiwe cha Mnazimmoja akimwaga madini.

He has had a very distinguished career and he is well respected.

Lakini Prof Assad alisahau kwamba hii ni Tanzania ya CCM na ina namna yake ya kuendesha nchi.

Natarajia Freeman Mbowe kesho atatoa mwelekeo wa siasa za upinzani maana mfumo bado upo pale pale regardless nani ni raisi.
 
Acha ujinga wewe utakosaje jazba huku ukiona madudu ya kutisha miaka nenda miaka rudi watu wanadhulumiwa, wanalawitiwa, wanauawa, wanapigwa risasi mchana kweupe, wanaporwa ubunge wao, trillions za walipa kodi zinaibiwa zinafisadiwa halafu unataka nisiwe na Jazba? Miaka 60 ya uhuru nchi inazidi kurudi nyuma kwenye kila sekta. Toa upumbavu wako hapa.
Eti unamuheshimiu Prof Assad wakati huo huo alipofukuzwa kama mbwa na jiwe hukutia neno. Acha ujinga wako!!!
Mkuu, kunywa maji utue roho, relax.
 
Natarajia Freeman Mbowe kesho atatoa mwelekeo wa siasa za upinzani maana mfumo bado upo pale pale regardless nani ni raisi.
Nina hofu na Mbowe na chama chake...!

Sijui kama huko ndani kwao wana'sophistication' (kiswahili chake sikijui) ya kutosha na kuweza kwa mfano kupambanua na kuepuka mitego ya aina ya mambo unayoyapigia chepeo hapa..., sijui!

Umewasema CCM hapo na ubovu wao, ambayo ni kweli kabisa..., bahati yao nzuri bado wanapumulia sifa walizokuwa nazo miaka mingi iliyopita, sifa ambazo kwa namna fulani waTanzania bado wanadhani kwamba labda siku moja chama hicho kitazinduka na kuacha ubovu uliopo huko sasa.
Matokeo yake ndiyo haya ya CCM kuendelea kutawala

CHADEMA na wengine, pamoja na mlengo wa chama chao ulivyo, inabidi wajivumbue upya, waonekana kwamba wao sio njia ya kutumika tu kuja kuihujumu Tanzania. Mtu atabisha, lakini ndio hivyo, niko 'serious' juu ya hili.
 
Nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ni nchi muhimu katika mstakabali mapinduzi ya viwanda barani Ulaya na Marekani.

Mwaka 2020 Uingereza walitangaza kuachana na magari yatumiayo mafuta ya diseli na petroli kufikia mwaka 2030 na wameazimia kuanza kutengeneza magari zaidi yatumiayo betri.

Hata hivyo tayari magari yatumiayo betri tayari yanatengenezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Nchi za kibeberu au maadui wa maendeleo hawawezi kuiruhusu Tanzania iendelee kwa kuwa na viwanda vyake .

Pia Tanzania ina malighafi zote kutengeneza hata seti za televisheni, vioo vya madirisha na balbu.

Kuna mambo matatu makuu ambayo sisi binadamu twapaswa kufahamu.

Mambo hayo ni technical know what, technical know how and technical know why.

Darasani mwalimu hutufundisha kuhusu somo la jiografia, kisha kuingia ndani kufanya tathmini kutumia kifaa maalum cha Compass kwa kutumia ramani na hiyo ni technical how.

Pale uanzapo kujiuliza hii Compas imetengezwa vipi ndipo unapoingia kwenye technical know why.

Mabeberu wanakuambia kuwa Afrika kuna dhahabu tatu ambazo ni Tanzania, Angola na Congo DRC.

Mabeberu wanaendelea kuziangalia nchi tatu ambazo nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ambazo wana malengo ya muda mrefu hadi miaka 50.

Katika nchi hizo ni Tanzania ambayo wao mabeberu wana uwezo wa kuingia na kujichotea maliasili watakavyo.

Kutokea bandari ya Lobito iliopo Benguela kupitia Lusaka, Lubumbashi ni ukanda maalum ulojaa madini, mafuta na madini ya uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi na mabomu ya nyuklia na mitambo yake.

Lango kuu la kuingia kwenda huko ndani au (interior) na kutokea ni Bagamoyo na ni njia rahisi kuliko kuzunguka Cape Town.

Ila mabeberu hao wakadai kuwa watakuja kwa mazungumzo na ikiwa mazungumzo yatashindikana basi watatumia mbinu zozote kuhakikisha wanafanikiwa azma yao.

Wazungu hao wanasema kuwa Tanzania ni nchi ya kuingia na kutokea Afrika kupitia Bagamoyo. Pia wanasema kuwa asilimia 60 ya biashara ya meli kuanzia mwaka 2050 itakuwa ndani ya bahari ya Hindi na hiyo ndio itakuwa Ocean of the future.

Hivyo, meli yaweza kutoka bandari ya Lobito kupitia Dar-es-Salaam hadi mfereji wa Suez bila shida na kwa uharaka zaidi.

Na hivyo ndivyo mfalme Leopold wa pili wa Belgium alivyokubaliana na wakoloni wa kijerumani kujenga reli ya kati ambayo ingesafirisha bidhaa zote za malighafi kutoka katikati ya Tanzania na Afrika kuelekea bahari ya Hindi.

Mfalme huyo alikuwa akivuna zao la mpira na kulisafirisha kwenda Ulaya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama matairi ya magari, baiskeli na zingine yaani alikuwa "supplier" mkubwa.

Moja ya viwanda vikubwa ambavyo mfalme huyo alikuwa akiviuzia malighafi ya mpira ni kiwanda kinachotengeneza bidhaa za Dunlop.

Waafrika wengi sana raia wa Congo walikufa wakivuna zao hilo na wengine kukatwa mikono kwa kushindwa kufanya hivyo.

Bahari ya Hindi ni bahari ilojaaliwa kila aina ya maliasili kuanzia mafuta, gesi asilia na uranium. Leo hii twashuhudia jinsi magaidi wa kupandikizwa nchini Msumbiji wakitumika kama kivuli cha wizi wa maliasili hizi zinazoibwa usiku na mchana.

Mwandishi Robert Kaplan katika kitabu chake cha Monsoon - "The India Ocean and Future of American Power" anaitaja bahari ya Hindi kama New Great Game kama ndo njia ya China ikitumia meli zake kubwa za mafuta kusaka maliasili hiyo ndani ya bahari ya Hindi.

Lakini safari hii upo uwezekano mkubwa wa vita ndani ya bahari hiyo baina ya nch iza kibeberu yaani Marekani na China.

Kaplan anaelezea muungano wa nchi za Marekani, China na India katika bahari ya Hindi katika kufanya biashara, kuzuia vitendo vya utekaji meli yaani Piracy, kulinda njia za usafiri wa meli na kuitikia wito wa majanga ndani ya bahari hiyo.

Bila shaka kelele za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni moja ya vielelezo vya mpango wa nchi za kibeberu.

Mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ulofumuliwa na hayati John Magufuli haukuwa mkataba uloweka maslahi ya taifa mbele na ulikuwa ni wa miaka 99.

Mkataba huo pia haukuwa unaruhusu maendelezo yoyote ya bandari zingine kama bandari ya Dar-es-Salaaam, Tanga, Zanzibar.

Hiyo ni kwasababu Bagamoyo ndo lango kuu la kuingiza na kutoa rasilimali zote zinatoka ndani ya Tanzania na maliasili zingine zinazotoka ndani ya Congo DRC na Angola.

Kwa vile nchi za kibeberu tayari wana ramani ya Afrika na sehemu zilipo maliasili basi Tanzania pamoja na Angola na Congo DRC na wanafahamu kuwa sasa hivi ujazo wa Uranium na madini mengine umefikia kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuvunwa, basi sisi hatuna ujanja.

Tanzania tunapaswa kueleza wazi msimamo wetu na pia kueleza ni nini tunataka kwani mali tunayo.

Tanzania haina budi kulinda ukanda wa bahari ya Hindi hadi Msumbiji kuhakikisha usalama wake hauingiliwi kirahisi. Serikali pia inawajibika kueleza msimamo wake kuhusiana na mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Lakini si kuanza kuzunguka mbali na kuanza mijadala ya kupoteza muda huku tayari wenzetu wachache wamekaa tayari na mabeberu na wamepanga nini kinachofuata.

La sivyo tunakubali kuwa sie ni waangalizi tu wa rasilimali tulozikalia na tupo tayari kuzigawa bure au kwa ujira kiduchu.
Haya ni maoni yako yanayotokana na hisia na fikra. Angalau ukinipa references naweza kukuamini japo kwa asilimia chache. Ndio maana maandishi ya kuaminika hutumia rejea na kama hauna rejea ni muhimu kutangaza Disclaimer kwamba jamaani eeeh haya ni mawazo yangu tuu.

No research no right to speak. Tuwekee rejea.
 
Ukiangalia ktk angle nyingine
Maliasili hizi hapa Duniani ni za kila mtu mwenye uwezo wa kutumia achangamkie fursa
Sisi kuwa nazo ktk nchi yetu sio sababu ya sis kuendelea kuzilalia wkt tunajua hatuna ujuzi wa kuzitumia
 
rasimali zimetapakaa kila mahala duniani, ukosefu wa akili kwa WaAfrica ndio husababisha kuzidiwa akili kila siku....tuwekeze kwenye vichwa vya binadamu tuwajaze maarifa, maarifa yakitumika lazima usimame mwenyewe...
 
kama una rasirimali ardhini na huna maarifa acha wenye maarifa wazifanyie kazi....dunia ina shida na law materials nyie mmezikalia mnaleta ujuaji wa 1802 wakati dunia inataka kwenda mbele...
 
either muwe na maarifa muisaidie dunia kujikwamua au mshirikiane na wenye maarifa watumie maarifa watu waishi duniani..
 
Nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ni nchi muhimu katika mstakabali mapinduzi ya viwanda barani Ulaya na Marekani.

Mwaka 2020 Uingereza walitangaza kuachana na magari yatumiayo mafuta ya diseli na petroli kufikia mwaka 2030 na wameazimia kuanza kutengeneza magari zaidi yatumiayo betri.

Hata hivyo tayari magari yatumiayo betri tayari yanatengenezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Nchi za kibeberu au maadui wa maendeleo hawawezi kuiruhusu Tanzania iendelee kwa kuwa na viwanda vyake .

Pia Tanzania ina malighafi zote kutengeneza hata seti za televisheni, vioo vya madirisha na balbu.

Kuna mambo matatu makuu ambayo sisi binadamu twapaswa kufahamu.

Mambo hayo ni technical know what, technical know how and technical know why.

Darasani mwalimu hutufundisha kuhusu somo la jiografia, kisha kuingia ndani kufanya tathmini kutumia kifaa maalum cha Compass kwa kutumia ramani na hiyo ni technical how.

Pale uanzapo kujiuliza hii Compas imetengezwa vipi ndipo unapoingia kwenye technical know why.

Mabeberu wanakuambia kuwa Afrika kuna dhahabu tatu ambazo ni Tanzania, Angola na Congo DRC.

Mabeberu wanaendelea kuziangalia nchi tatu ambazo nchi za Tanzania, Angola na Congo DRC ambazo wana malengo ya muda mrefu hadi miaka 50.

Katika nchi hizo ni Tanzania ambayo wao mabeberu wana uwezo wa kuingia na kujichotea maliasili watakavyo.

Kutokea bandari ya Lobito iliopo Benguela kupitia Lusaka, Lubumbashi ni ukanda maalum ulojaa madini, mafuta na madini ya uranium ambavyo ni malighafi muhimu kwa utengenezaji wa betri za magari, simu za mkononi na mabomu ya nyuklia na mitambo yake.

Lango kuu la kuingia kwenda huko ndani au (interior) na kutokea ni Bagamoyo na ni njia rahisi kuliko kuzunguka Cape Town.

Ila mabeberu hao wakadai kuwa watakuja kwa mazungumzo na ikiwa mazungumzo yatashindikana basi watatumia mbinu zozote kuhakikisha wanafanikiwa azma yao.

Wazungu hao wanasema kuwa Tanzania ni nchi ya kuingia na kutokea Afrika kupitia Bagamoyo. Pia wanasema kuwa asilimia 60 ya biashara ya meli kuanzia mwaka 2050 itakuwa ndani ya bahari ya Hindi na hiyo ndio itakuwa Ocean of the future.

Hivyo, meli yaweza kutoka bandari ya Lobito kupitia Dar-es-Salaam hadi mfereji wa Suez bila shida na kwa uharaka zaidi.

Na hivyo ndivyo mfalme Leopold wa pili wa Belgium alivyokubaliana na wakoloni wa kijerumani kujenga reli ya kati ambayo ingesafirisha bidhaa zote za malighafi kutoka katikati ya Tanzania na Afrika kuelekea bahari ya Hindi.

Mfalme huyo alikuwa akivuna zao la mpira na kulisafirisha kwenda Ulaya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama matairi ya magari, baiskeli na zingine yaani alikuwa "supplier" mkubwa.

Moja ya viwanda vikubwa ambavyo mfalme huyo alikuwa akiviuzia malighafi ya mpira ni kiwanda kinachotengeneza bidhaa za Dunlop.

Waafrika wengi sana raia wa Congo walikufa wakivuna zao hilo na wengine kukatwa mikono kwa kushindwa kufanya hivyo.

Bahari ya Hindi ni bahari ilojaaliwa kila aina ya maliasili kuanzia mafuta, gesi asilia na uranium. Leo hii twashuhudia jinsi magaidi wa kupandikizwa nchini Msumbiji wakitumika kama kivuli cha wizi wa maliasili hizi zinazoibwa usiku na mchana.

Mwandishi Robert Kaplan katika kitabu chake cha Monsoon - "The India Ocean and Future of American Power" anaitaja bahari ya Hindi kama New Great Game kama ndo njia ya China ikitumia meli zake kubwa za mafuta kusaka maliasili hiyo ndani ya bahari ya Hindi.

Lakini safari hii upo uwezekano mkubwa wa vita ndani ya bahari hiyo baina ya nch iza kibeberu yaani Marekani na China.

Kaplan anaelezea muungano wa nchi za Marekani, China na India katika bahari ya Hindi katika kufanya biashara, kuzuia vitendo vya utekaji meli yaani Piracy, kulinda njia za usafiri wa meli na kuitikia wito wa majanga ndani ya bahari hiyo.

Bila shaka kelele za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni moja ya vielelezo vya mpango wa nchi za kibeberu.

Mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ulofumuliwa na hayati John Magufuli haukuwa mkataba uloweka maslahi ya taifa mbele na ulikuwa ni wa miaka 99.

Mkataba huo pia haukuwa unaruhusu maendelezo yoyote ya bandari zingine kama bandari ya Dar-es-Salaaam, Tanga, Zanzibar.

Hiyo ni kwasababu Bagamoyo ndo lango kuu la kuingiza na kutoa rasilimali zote zinatoka ndani ya Tanzania na maliasili zingine zinazotoka ndani ya Congo DRC na Angola.

Kwa vile nchi za kibeberu tayari wana ramani ya Afrika na sehemu zilipo maliasili basi Tanzania pamoja na Angola na Congo DRC na wanafahamu kuwa sasa hivi ujazo wa Uranium na madini mengine umefikia kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuvunwa, basi sisi hatuna ujanja.

Tanzania tunapaswa kueleza wazi msimamo wetu na pia kueleza ni nini tunataka kwani mali tunayo.

Tanzania haina budi kulinda ukanda wa bahari ya Hindi hadi Msumbiji kuhakikisha usalama wake hauingiliwi kirahisi. Serikali pia inawajibika kueleza msimamo wake kuhusiana na mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Lakini si kuanza kuzunguka mbali na kuanza mijadala ya kupoteza muda huku tayari wenzetu wachache wamekaa tayari na mabeberu na wamepanga nini kinachofuata.

La sivyo tunakubali kuwa sie ni waangalizi tu wa rasilimali tulozikalia na tupo tayari kuzigawa bure au kwa ujira kiduchu.
Kaka Richard, labda utumie muda kidogo ujifunze kutumia intaneti (au maktaba ya chuoni) na kujielimisha kabla ya kuposti hapa.

Historia yako si sahihi (mfalme Leopold wa Ubelgiji hakujenga reli ya kati wala hakuhusika katika ijenzi), wala jiografia yako (mzungu gani anasema Bagamoyo ni njia kuingia Afrika??? Bagamoyo ni mji mzuri ila hamna kitu kiuchumi, ni Wachina waliotaka kujenga bandari kule, si kwa sababu ya Bagamoyo lakini kama bandari ya pili ya Dar es Salaam), wala uchumi wako ( mbona nchi za kibeberu wanapata faida kubwa sana kubadilishana / kuuzana bidhaa na nchi nyingine zenye viwanda na tasnia ya huduma, ilhali faida katika biashara na nchi zenye malighafi ni ndogo??? Mfano kwa nini asilimia ya bishara ya Afrika katika takwimu ya Umoja wa Ulaya iko chini kiasi hiki kulingana na biashara na sehemu nyingine za Dunia??)

Bila shaka ni muhimu kutodanganywa katika biashara na mambo ya malighafi! Na bila shaka nchi nyingi za Afrika zimedanganywa katika biashara hiyo! Lazima ikwishe.
Lakini hakuna sababu ya kushangaa kwamba nchi nyingine wana ramani nzuri ya malighafi za Tanzania, maana data zinapatikana kote duniani, ni uwezo tu kutengeneza ramani.
Labda ujiunge na Openstreetmaps.org na ujifunze kutunga ramani mwenyewe.
 
Mkuu, mimi nimesoma historia uzuri tu na kwa undani.

Sikusema Mfalme Leopold wa pili alijenga reli ya kati (soma tena mada yangu uzuri).

Nimesema alikubaliana na Ujerumani kwamba atatumia reli hiyo kupitisha malighafi ya mpira kwenda Ulaya.

Na hiyo ilikua baada ya yeye (Mfalme Leopold wa pili ) kuitangaza sehemu hiyo ya Congo kuwa Congo Free state baada ya mkutano wa Berlin uloitishwa pale bwana Otto Von Bismark kansela wa Ujerumani alipoona mabeberu wanagombia sehemu hiyo bila muafaka.

BIdhaa kama meno ya tembo, mpira, dhahabu, uranium na hata biashara ya watumwa ambayo alikuwa akifanya na mfanyabiashara maarufu kama Tippu Tip zilikuwa zipitie njia hiyo ambayo baadae ndo ilijengwa ya reli ya kati.

Pia ukisoma uzuri historia Ubelgiji ilitawaliwa na Ujerumani katika vita ya kwanza ya dunia hivyo kulikuwa na mahusiano fulani ya kibiashara na hata nchi zingine kama Marekani ambazo zilihitaji madini kama Uranium ambayo ndo yalitumika kutengeneza bomu la nyuklia lilozipiga Hiroshima na Nagasaki.

Kumbuka Germany East Africa makao makuu yao ya kwanza yalikuwa ni Bagamoyo na baadae walipotaka kupanua shughuli zao na bandari ndo wakahamia Dae-es=Salaam.

Jasusi Henry Morton Stanley alianzia Bagamoyo kufuata njia alozipitia jasusi mwingine David Livingstone ambae alikwenda hadi Ujiji Kigoma.
 
Wenzetu wapo vizuri sana...

Cha muhimu ni kukomaa nao tuende nao sawa...
 
Historia yako haikai. Mfalme Leopold hakufanya makubaliano kuhusu reli na Wajerumani. Hakuhusika katika ujenzi huo. Reli ilifika Kigoma mwaka 1914, miezi michache kabla ya vita ya kwanza ya Dunia ilianza. Ukiona si vile, lete chanzo. Hati za miaka ile inapatika zote intaneti.

Ubelgiji "kutawaliwa" na Ujerumani wakati wa vita kuu ya kwanza? Ilitwaliwa na jeshi la Kijerumani lakini serikali na mfalme pamoja na jeshi walihamia Ufaransa. Kinyume jeshi la Ubelgiji kwenye Kongo (waliitwa Force Publique) lilishambulia koloni ya Afrika ya Mashariki, likatwaa Rwanda, Burundi na maeneo hadi Tabora.

Unataja uranium, hakika hakuna mtu aliyetafuta urani pale kongo katika karne ya 19. Tabia nururifu ya urani ilitambuliwa mwaka 1896 na Henri Becquerel, na uwezekano wa kuitumia ulionekana baada ya mwaka 1930, si kabla. Wala Tippu Tip wala wakoloni Wajerumani wala mfalme Leopold walijua kitu kuhusu urani.

Tena njia ya reli haikujengwa kwa ajili ya biashara ya Tippu Tip. Lengo kubwa ya wakaloni wajerumani lilikuwa kumaliza nafasi za Waswahili na Waarabu katika biashara ya misafara - kwa kumaliza misafara hiyo. Njia ya kumaliza misafara ya kubeba bidhaa (iliyokuwa ghali saaana) ilikuwa kujenga reli; bidhaa kutoka mashariki ya Kongo zilikadiriwa kuwa sehemu ya mizigo itakayokuja, lakini zaidi walileanga kusafirisha, tena kwa bei nafuu, mazao ya mashamba makubwa waliyopanga na pia madini mbalimbali. Pia walimaliza biashara ya watumwa tangu mwanzo.

Morton Stanley hakuwa "jasusi" - alisafiri Ujiji kama mwanahabari wa gazeti la Marekani aliyemtafuta Livingstone - na huyu Livingstone alikuwa mtu maarufu katika Ulaya na Marekani wakati ule kutokana na taarifa zake (pamoja na ziara za kuzunguka Ulaya) alipoleta habari za biashara ya watumwa. Jasusi ni mtu anayejificha na kufanya kazi kwa siri. Hao wawili hawakuficha kitu chochote. Stanley alikuwa mtu mwenye tabia mbaya aliyedharau Waafrika, Livingstone alikuwa mtu mpole aliyependwa na wengi.

Bagamoyo kwa miaka michache ilikuwa ofisi kuu ya "Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki" iliyoshindwa kutawala maeneo iliyodai kumiliki, lakini "Afrika ya Mashariki ya Kijerumani" ilianza hali halisi mwaka 1891 wakati serikali ya Ujerumani ilipochukua utawala mkononi mwake - na hao walipeleka mji mkuu mara moja Dar es Salaam.
 
Uzi mzuri, watu wanazidi kutupia rejea / reference nasi tunajifunza zaidi kuhusu biashara za kikanda na kimataifa enzi hizo za Tippu Tip, King Leopold II, Kaizer wa Prussia/ Germany mpaka wakati huu tulionao 2021.
 
Nyie acheni utoto, mabeberu mabeberu wamewahi kuja na bunduki hapa kumpora mtu madini? Si mnawaita wenyewe. Sheria ya madini 1997 wametunga wao? Mbona Nyerere aliye yaacha huko chini hawakumfanya kitu njaa zenu mnaingia mikataba mibovu halafu mnalia Lia. Wanawashangaa mjue?
 
Hapo utofautishe. Migodi ya dhahabu iliyoanzishwe wakati wa Mwingereza zilichoka katika miaka ya 60 kulingana na bei ya dhahabu na tekinolojia iliyopatikana. Kwa miaka mingi dhahabu ya Tanzania haikuwa na kivutio. Tangu kupanda kwa bei ya dhahabu na tekinolojia mpya wanachimba sasa ardhi yenye kiwango kidogo cha madini ya dhahabu ambayo wangepuuza miaka 30, au 40 iliyopita.
Hawakuja kwa bunduki, walikuja na elimu na tekinolojia. Na hapo ni sehemu moja ambako Magu alifaulu kubadilisha kitu kweli (asilimia za nyongeza katika dhahabu zililipia ujinga wa kununua ndege...)
 
Back
Top Bottom