Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Lakini sasa hali imebadilika, kwani shirika moja la China lilinunua migodi hiyo miwili, na miaka michache baadaye, kijiji hicho kina mabwawa ya maji safi, mtandao wa umeme, na barabara. Licha ya hayo, shughuli za afya na elimu pia zilianza kustawika. Wachina pia waliwafundisha wanakijiji jinsi ya kukuza mahindi vizuri kwa kutumia mbolea za kikemikali. Baada ya kuwasili kwa Wachina, migodi hiyo imewaajiri makumi ya elfu ya watu, na Jacquie akawa msafishaji katika eneo la migodi, na mume wake amejifunza ustadi wa kurekebisha mashine kutoka kwa Wachina. Familia yake imejenga nyumba mpya na kununua pikipiki, watoto wake wanasoma katika shule ya msingi iliyojengwa na Wachina. Labda siku moja wanaweza kwenda nje ya milima ambapo mababu zao hawajawahi kufika.
Kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maendeleo ya migodi hiyo pia yameleta mafanikio ya kiuchumi. Mwaka jana, nchi hiyo ilichangia asilimia 76 ya uzalishaji wa madini ya kobalti duniani. Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinaonesha kuwa katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya nchi hiyo na nchi za nje imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 21, na mauzo ya bidhaa zake kwa nje yamefikia dola bilioni 12.563.
Huu ni mfano mmoja wa matokeo ya ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta za maliasili. Hata hivyo, mara baada ya kufungwa kwa Mkutano wa mwaka 2024 wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCACA, baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vimeanza tena kupotosha ukweli wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na kusema China “inapora maliasili za Afrika”, na kufanya “ukoloni wa mamboleo” barani Afrika. Kisingizio chao cha kusema hivyo ni kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, China imeagiza bidhaa nyingi zaidi za maliasili kutoka Afrika.
Lakini, kauli hiyo haina msingi wowote. Kwanza, muundo wa biashara kati ya China na Afrika unatokana na viwango vya uchumi. Nchi za Afrika bado hazina uwezo wa kuzalisha bidhaa za teknolojia ya juu na kuziuza kwa China, ila malighafi na mazao ya kilimo, hilo si kosa la China. Sasa China inazisaidia nchi za Afrika kuendeleza sekta za viwanda, na iko siku Afrika zitaweza kuzalisha bidhaa za kisasa na kuziuza kwenye soko la kimataifa. Pili, Afrika inauza malighafi kwa nchi mbalimbali duniani, kwa nini China inalaumiwa kuwa mporaji kwa kununua bidhaa hizo kutoka Afrika? Tatu, China kuwekeza na kununua sekta za rasilimali barani Afrika, kunaongeza mapato ya nchi za bara hilo, hali ambayo inaweza kuzisaidia nchi hizo kupata fedha za kujiendeleza.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya majukwaa kama vile FOCAC na “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa. Lakini hali hii haipendwi na baadhi ya nchi za Magharibi, ambazo zimefanya kila ziwezavyo ili kukashifu ushirikiano kati ya China na Afrika, kama vile kauli za China inafanya “ukoloni wa mamboleo” barani Afrika, au China inaweka “mtego wa madeni” dhidi ya nchi za Afrika. Lakini uwongo hauwezi kuwa ukweli. Kutokana na juhudi za pamoja za China na nchi za Afrika, ushirikiano kati ya pande hizo mbili utaimarika zaidi na kuleta mafanikio makubwa zaidi.