Nchi masikini zenye uchumi unaoyumba (unstable economy) na mfumuko mkubwa wa bei (high inflation rate), hulazimika kila mwaka kuongeza mishahara ya watumishi wake ili kujaribu kukabiliana na mfumuko wa bei. Ongezeko hilo la mishahara kwa kawaida huwa ni kiduchu lakini matokeo yake huwa ni kusababisha ongezeko zaidi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Yaani ni vicious circle.
Kipindi cha miaka 5 iliyopita tumeshuhudia mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu kuteremka sana na ku stabilize. Uko chini ya asilimia 3! Hivyo thamani ya hela yetu ilivyokuwa mwaka 2015 iko pale pale hadi sasa. Kwa mfano bidhaa nyingi muhimu zilizokuwa zinauzwa shs elfu kumi mwaka 2015 mpaka sasa inauzwa kwa bei hiyo hiyo au chini ya hiyo.
Siyo kweli kwamba promotions na annual increments za watumishi wa umma waliokizi sifa hawakupewa promotions na annual increments hizo ispokuwa kwa kwenye kipindi hicho kifupi cha uhakiki wa watumishi hewa na watumishi feki. Katika kipindi hiki cha miaka 5 zaidi ya watumishi zaidi ya laki tatu (ie zaidi ya 50% ya watumishi wote) walipata promotions zao baada ya kukidhi masharti yake. PAYE yao imepunguzwa nk. Kodi za kupanga nyumba nk hazipandi kila mwaka kama ilivyokuwa huko nyuma, badala yake zimepungua. Watumishi wa umma sasa hivi ni highly paid ukilinganisha na wengi walio kwenye private sector.
Huko tulikotoka private sector ndiyo ilikuwa inalipa zaidi. Ndiyo maana utumishi wa umma umetulia, hakuna migomo migomo tena kama tunazoziona kwenye nchi za majirani kwetu. Na serikali imeahidi kuendelea kuboresha mishahara yao kuendana na ukuaji wa uchumi wa nchi bila kusababisha mfumuko wa bei. Ndivyo zilivyofanya na zinavyofanya nchi zilizoendelea kama ulaya, marekani na uchina. Mambo haya ni ya kitaalamu. Si ya kimuhemuko wa kisiasa.
Nyie ndio mnaofurahia shida za binadam kwa sababu shida zao ndizo manufaa yenu.
Hivi Tanzanaia Chini ya Hiki chama kilichoasisiwa na mawakala wa Lusifa na ushauri wa CIA ili kuua vyama vya Ukombozi wetu yaani ASP na TANU kinafuata mfumo gani wa Maisha?
Ujamaa au Ukomunisti au Ubepari au Utumwa?
Bila shaka CCM imafuatafumo wa Utumwa .
Ukiangaliaa maisha ya watawala na watawaliwa chini ya utawala wa CCM kuna mabawana na Watwana.
Ndani ya nchi moja maskini ,nchi isiyoweza kuwalipa wafanyakazi wake mshahara umaoweza kuendesha maisha yake kwa wiki mbili lakini inawaweka watawala (Mabwana) waishi maisha ya kifahari na kujilimbikizia mali chungu nzima.
Ni mtawala gani ndani ya CCM anayeweza kutangaza mali zake mbele ya watumwa wanaowatumia kujineemesha? Jibu ni hakuna mana wanatumia ofisi kama biashara zao na makampuni yao. Ofisi za Umma zinatumiwa kuwaneesha watawala huku wafanyakazi wa chini wakiwa kama watumwa wao.
Hebu jiulize kuna Taasisi ndani ya Serikali Kuu mfanyakazi wa chini analipwa laki nne kwa mwezi ( amepanga ,anasafiri kwa bodaboda au basi kwa mshahara huo huo, hana posho ya mawasiliano, umeme analipa ,maji, anakatwa kodi na akinunua bidhaa anakatwa tena kodi kwenye kimshahara kilichobakia ,anafamilia ,anataka siku moja naye ajenge nyumba akitaka kukopa kiwango chake cha mwisho ni mil. 6 ) ; Kwenye ofisi hiyo ya umma kuna Bosi wake analipwa Mil. 7 na kuendelea (Anapewa nyumba ya serikali,anapewa gari la serikali,anapewa dereva wa serikali, analipiwa umeme na maji ,anapewa posho za mawasiliano, na ana fursa kubwa ya kupata msaada ofisi yoyote , bima yake ya afya ni daraja la juu , ana Diplomatic Passport, akiingua benki anaweza kukopa mil.500 n
k.) hawa wote wanatumia soko moja na fursa sawa kwenye ardhi, nyumba na makazi .
Yani hawa ni binadamu wawili wanaoishi kwenye dunia mbili tofauti lakini wanatambuana wakati yule wa juu anapotafuta kodi ili aendelee kula bata.
CCM Mungu anawaona. Binadamu ni binadamu na ana haki ya kuishi kama binadam kwa heshima na utu wake kuthaminiwa. Somalia hakuna Serikali lakni wasomali wanaishi maisha ya juu kuliko waafrika wa nchi zenye serikali zisizojali maisha ya wananchi wao. Serikali ni kikundi cha watu wachache wanaowakilisha umma kwenye kugawa keki ya Taifa na kutoa maamuzi kwa haki. Ukiondoa neno haki basi serikali inakua ni genge la wahalifu wanaostahili kufukuzwa madarakani.
Nchi yenye utajiri mkubwa kama Tanzania na Zanzibar kuwa na wafanyakazi wenye mishahara isiyokidhi mahitaji ya bunadam kwa mwezi mzima ni laana.
CCM kwenye kukusanya kodi na mifumo mingine ya kinyonyaji wanaiga mifumo ya Kikaburu ya kukusanya mali za umma na kuwalimbikizia watawala .
Nilishangaa kuona Mtu kama Mwinyi mwenye miaka 94 aliyetawala Zanzibar na Tanganyika na Tanzania anajengewa nyumba ya mabilioni eti ni sheria wakati wafanyakazi wao sheria haifuatwa . Mtu ambaye hawezi kuthubutu kutaja mali zake na hisa alizo nazo kwenye makampuni ya mabilionea wa ndani na nje ya nchi. Eti yeye naye ni kama mfanyakazi anayelipwa laki 4 ambaye hata akope hawezi kumiliki nyumba yenye thamani ya sh. Mil. 100 mpaka astaafu kwa miaka 35 .
Hiyo ndiyo CCM na ujamaa . Chama kinachoweka serikali ya mabilionea kwama tunavyoona kule Zanzibar wanavyotumia Silaha na vifaru kumweka mtoto wa mfalme Madarakani . Wanatumia mapolisi ambao ni watoto wa maskini kuwaua maskini wenzao ili Tajiri aingie madarakani.
Nini cha kufanya kwa Watanzania ili kuwapa waanyakazi maisha bora lakini pia unafuu wa maisha :
Kuanzisha Benki ya Nyumba kwa wafanyakazi chini ya udhamini wa PSSF na mwajiri na NHC . Maisha ni Nyumba. Wizi rushwa na kila aina ya dhulma ni kwa sababu wafanyakazi wote wanawaza kujenga . Wanapanga kwa bei kubwa , mtu analipa kodi kubwa kila mwezi . Mafano mtu anayelipwa laki nne akipanda nyumba yenye vyumba viwili na sebule analipa kodi zaidi ya laki moja na nusu kwa mwezi. Anabakiwa na 250000/ .
Hapo MwanaCCM anaona ni sawa kabisa alimradi fulani awe Rais mana ni wa dini yake au kabila lake. Ndio uhaba wa akili tulionao waafrika.
Wafanyakazi wajengewe nyumba za kuishi.
Nyumba za msajili ziwe ni nyumba za waanyakazi wapangishiwe kwa bei ndogo na wakatwe kwa miaka yote mpaka ifikie thamani ya nyumba kisha wapewe hizo nyumba .
(NB:Nendeni mkajifunze maono ya Mkombozi wa Zanzibar Maalim Seifu. Nitawashanga wazanzibari wakimchagua mtu asiyejua shida zao ,Husein Mwinyi kibaraka kama aivyokua Carl Peter.)
Mfano : walimu kila shule iwe na nyumba za shule hata kwa kulipa kodi kidogo lakini walimu watakua wanakaa karibu na shule hivyo wanapunguza gharama za usafiri n.k.
Serikali ya Mkoloni mzungu iliwajali sana waanyakazi wake kuliko hii ya Mkoloni Mweusi.
Eti hakuna migomo. Wewe ni mfia madaraka na chama.
Kigomo itatoka wapi wakati CCM imewahonga viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na wengine ni makada kwa ajili ya kuzuia maslahi ya wafanyakazi.
Lakini pia wataandamana kwenye uhuru upi wa utawala wa aina gani ?? Ni bora wakati wa Mkoloni mzungu wafanyakazi waliandamana kwa uhuru kuliko wakati wa mkoloni mweusi wa awamu ya Tano. Wakati wa mkoloni mzungu ukifika kijijini ungeona nyumba za nyasi za wakulima lakini nyumba ya bati nzuri ilikua ni ya mfanyakazi wa serikali ya mkoloni mzungu .
Nani ataandamana afukuzwe kazi na huko mtaani biashara zote zinakufa kwa kodi kubwa.