Nchi zinazoongoza kwa kuleta watalii hapa nchini, karibu zote ziko kwenye "lockdown" Je, tutavuka na tukivuka tutakuwa katika hali gani?

Nchi zinazoongoza kwa kuleta watalii hapa nchini, karibu zote ziko kwenye "lockdown" Je, tutavuka na tukivuka tutakuwa katika hali gani?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Nimesoma gazeti la The Citizen la siku ya leo ambapo gazeti hilo limegusia athari za ugonjwa wa corona katika sekta ya utalii hapa nchini hasa kwa mkoa wa Arusha.

Katika habari hiyo,gazeti limegusia madhara machache yaliyojitokeza mpaka sasa ambapo ni pamoja na fleet za tourist vehicles kuwa grounded,hotel kubwa na maarufu ya jijini Arusha ya Palace yenye vyumba 200 kukosa wateja kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 8 tangu ianze kutumika,flight za kimataifa kupungua, n.k.

Madhara mengine ni taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa kampuni moja maarufu ya kitalii ya jijini Arusha kuwa imewapa likizo ya lazima wafanyakazi wake kutokana na kufutwa kwa safari nyingi.

Vile vile,Afisa mmoja wa Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC),amesema bila kutoa ufafanuzi kuwa mikutano kadhaa imefutwa.

Hayo yote tisa,kumi ni kuwa,gazeti limetaja nchi zinazoongoza kwa kuleta watalii hapa nchini:Marekani (ikiwa ndio inaangoza), Uingereza, Ujeruman, Ufaransa na Italia.

Kama unafuatilia vyombo vya habari, utagundua karibu nchi zote hizo sasa ziko au ndio zinaingia kwenye lockdown kutokana na janga hili la ugonjwa wa corona.

Swali la msingi hapa ni je,ikiwa utalii unachangia asilimia 25 ya mapato ya nchi huku hali ikiwa ndio hio, kwa mwendo huu tutavuka, na tukivuka, tutakuwa kwenye hali gani?

Tukumbuke hili gonjwa ndio kwanza linashika kasi katika mataifa hayo kama ilivyo katika mataifa mengine duniani na hata likidhibitiwa, athari zake ni wazi zitachukua muda kutoweka.

Hapa ndio umuhimu wa hoja ya Msigwa kulitaka Bunge kujadili gonjwa hili na madhara yake na kuishauri serikali angali mapema unapoonekana.

Wacha tuone hali itakuwaje.

The Citizen Tanzania (@TheCitizenTZ) | Twitter
 
Nakumbuka kauli ya Mkuu kwa wahanga wa mafuriko wakati wao wanafurika huko, nyinyi limeni kisha mje muwauzie kwa bei, huenda bado mkuu anaamini Corona pia ni fursa kwetu tupige pesa utalii nk ukirejea kauli ya mental polepole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hawa watu wako radhi tufe kwa sababu ya hela tena ya utalii, hawana utu kabisa, hawatujali wananchi tuliowaweka madarakani, ila kwakua huu ugonjwa hauchagui na naomba Mungu uanzie kwa wakubwa na walivyo na maradhi ya kisukari na ukimwi!?
 
Mkuu sio siri tena,hakuna watalii,hoteli na kampuni nyingi hakuna kazi na zimefungwa,kwanzia porini mpaka mjini.wafanyakazi wengi wamerudi hawana kazi
 
Wananchi wa nchi gani wamewaweka madarakani?si anasema alisukumiziwa ikulu?
 
Mkuu sio siri tena,hakuna watalii,hoteli na kampuni nyingi hakuna kazi na zimefungwa,kwanzia porini mpaka mjini.wafanyakazi wengi wamerudi hawana kazi
Mbali na madhara ya kiuchumi, ni wazi kutakuwa na madhara mengi ya kijamii yatoyotokana na hali hii.
 
Nashauri ,Seriiali inatakiwa ibane matumizi. Misafara ya ma VX V8 iondolewe kabisa.
Mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wakiwa na safari moja wapande gari moja. Mawaziri wakiwa na safari moja ya kuzindua Choo cha shimo cha shule ya nyangarakata wapande Coaster moja.
Hii nchi uchumi ukiyumba wafanyakazi wa chini na watu wote maskini wataumizwa sana.

Nashauri pia Wateule wote wa serikali wakatwe mishahara kwa 25% asiyetaka aachie ngazi Mara moja.Mbona Kuna vyama vinajiendesha kwa michango ya waliopata ubunge !? Kumbe hata serikali inaweza kufyeka mishahara ya wateule kwa 25% na kuweza kufidia pengo la fedha za watalii.

Vinginevyo wataumizwa watu wasioweza kupata hata mlo mmoja kwa siku.
Tuone sasa wale wanaojiita wazalendo kupitia mgongo wa Dola kama watasaidia kitu gani kuonyesha uzalendo wao.
Tunawataka wakuu wa mikoa na mawaziri wakijirokeza na kutangaza kuwa wanatoa 25% ya mishahara yao kuchangia serikali wanayoona iko damuni na wanaipenda kwa uzalendo wa kweli sio unafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wafanyakazi wa utalii wameshazoea upungufu wa watalii, ndio maana kuna high na low season, sasa hivi ni low season, high season inaanza mwezi wa 6.
 
yaani ukiwapata wao ni asubuhi na mapema bendera nusu mlingoti. maana hawawezi kwenda kutibiwa nje wenyewewe wameshafunga mipaka.
mkuu hawa watu wako radhi tufe kwa sababu ya hela tena ya utalii, hawana utu kabisa, hawatujali wananchi tuliowaweka madarakani, ila kwakua huu ugonjwa hauchagui na naomba Mungu uanzie kwa wakubwa na walivyo na maradhi ya kisukari na ukimwi!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuvuka sisi tutavuka, maana mpaka sasa bado hakuna ambukizo la bongo kwa mbongo yoyote. Wote 6 waliogundulika wamekuja nayo, hapa kwetu haiambukiziki.
P
Mbona uko kinyume mada, issue hapa Ni nchi tunazotegemea watalii ziko locked wewe unaleta siasa zako ...

Naona karma ya Kabendera inaanza kukurarua na bado utakufa mdomo wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuvuka sisi tutavuka, maana mpaka sasa bado hakuna ambukizo la bongo kwa mbongo yoyote. Wote 6 waliogundulika wamekuja nayo, hapa kwetu haiambukiziki.
P
Hoja hapa ni namna gani tutavuka kiuchumi ikiwa utalii utaendelea kuporomoka sambamba na sekta nyingine.
 
FDA wanadai inaweza kuchukua miezi 18 au zaidi kuthibiti korona, ngoja tuone kama wataalamu watagundua chanjo mapema na kuitumia au watu watajenga kinga na kusababisha ugonjwa kutokomea...yote yanawezekana hasa Mungu Mwenyezi anapokuwa ameamua kwamba hili janga lisiendelee
 
Nashauri ,Seriiali inatakiwa ibane matumizi. Misafara ya ma VX V8 iondolewe kabisa.
Mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wakiwa na safari moja wapande gari moja. Mawaziri wakiwa na safari moja ya kuzindua Choo cha shimo cha shule ya nyangarakata wapande Coaster moja.
Hii nchi uchumi ukiyumba wafanyakazi wa chini na watu wote maskini wataumizwa sana.

Nashauri pia Wateule wote wa serikali wakatwe mishahara kwa 25% asiyetaka aachie ngazi Mara moja.Mbona Kuna vyama vinajiendesha kwa michango ya waliopata ubunge !? Kumbe hata serikali inaweza kufyeka mishahara ya wateule kwa 25% na kuweza kufidia pengo la fedha za watalii.

Vinginevyo wataumizwa watu wasioweza kupata hata mlo mmoja kwa siku.
Tuone sasa wale wanaojiita wazalendo kupitia mgongo wa Dola kama watasaidia kitu gani kuonyesha uzalendo wao.
Tunawataka wakuu wa mikoa na mawaziri wakijirokeza na kutangaza kuwa wanatoa 25% ya mishahara yao kuchangia serikali wanayoona iko damuni na wanaipenda kwa uzalendo wa kweli sio unafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Good thinking
 
Kukosekana kwa Watalii Thailand kumesababisha Nyani waliokuwa wakitegemea chakula kutoka kwa watalii kuingia mjini.

Back
Top Bottom