Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Nimesoma gazeti la The Citizen la siku ya leo ambapo gazeti hilo limegusia athari za ugonjwa wa corona katika sekta ya utalii hapa nchini hasa kwa mkoa wa Arusha.
Katika habari hiyo,gazeti limegusia madhara machache yaliyojitokeza mpaka sasa ambapo ni pamoja na fleet za tourist vehicles kuwa grounded,hotel kubwa na maarufu ya jijini Arusha ya Palace yenye vyumba 200 kukosa wateja kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 8 tangu ianze kutumika,flight za kimataifa kupungua, n.k.
Madhara mengine ni taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa kampuni moja maarufu ya kitalii ya jijini Arusha kuwa imewapa likizo ya lazima wafanyakazi wake kutokana na kufutwa kwa safari nyingi.
Vile vile,Afisa mmoja wa Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC),amesema bila kutoa ufafanuzi kuwa mikutano kadhaa imefutwa.
Hayo yote tisa,kumi ni kuwa,gazeti limetaja nchi zinazoongoza kwa kuleta watalii hapa nchini:Marekani (ikiwa ndio inaangoza), Uingereza, Ujeruman, Ufaransa na Italia.
Kama unafuatilia vyombo vya habari, utagundua karibu nchi zote hizo sasa ziko au ndio zinaingia kwenye lockdown kutokana na janga hili la ugonjwa wa corona.
Swali la msingi hapa ni je,ikiwa utalii unachangia asilimia 25 ya mapato ya nchi huku hali ikiwa ndio hio, kwa mwendo huu tutavuka, na tukivuka, tutakuwa kwenye hali gani?
Tukumbuke hili gonjwa ndio kwanza linashika kasi katika mataifa hayo kama ilivyo katika mataifa mengine duniani na hata likidhibitiwa, athari zake ni wazi zitachukua muda kutoweka.
Hapa ndio umuhimu wa hoja ya Msigwa kulitaka Bunge kujadili gonjwa hili na madhara yake na kuishauri serikali angali mapema unapoonekana.
Wacha tuone hali itakuwaje.
The Citizen Tanzania (@TheCitizenTZ) | Twitter