Nchimbi ataka wabadhirifu na wezi waombewe ili roho hizo za kuhujumu nchi ziwatoke!

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewataka Watanzania kuwaombea wanaofanya ubadhirifu na wezi ili roho hizo za kuhujumu nchi ziwatoke.

Amesema haiwezekani Rais Samia anahangaika kutafuta fedha ndani na nje ya nchi usiku na mchana na kuzishusha chini halafu hazitumiki kama ilivyokusudiwa, akatolea mfano wa mtu kuongeza idaidi ya manunuzi kuliko kinachohitajika bila aibu. Aliyasema hayo jana 7/6/2024 aliposimamishwa na wananchi katika mapokezi yake Korogwe-Tanga.

CCM mko serious kweli? Kuna Katiba, na Mahakama, zinafanya nini kuhakikisha sheria zinafuatwa? Kwanini tuna mhimili wa Mahakama kama kwa makusudi mnakula kwa urefu wa kamba zenu na hakuna chochote mnafanywa?

Hii ndio shida ya Rais (Mhimili wa serikali) kuwa na madaraka na nguvu kubwa kuliko wengine na yeye kuwa mteule wa viongozi Wakuu kwenye karibu taasisi zote nchini. Unatia aibu na kauli za kijinga namna hii utafikiri huna darasa hata moja kichwani.

Your browser is not able to display this video.
 
Last edited:
Angeanza yeye kwanza kujiombea. Inasikitisha sana kwa katibu mkuu wa chama tawala kutoa kauli kama hiyo iliyojaa unyonge mbele ya mafisadi. Aachie ngazi
 
Mwambieni nchimbi aache hizo!!!

Anatia hasira,magereza na mahakama zipo kwa ajili gani!!?

Mwambieni tuna mambo ya kuombea ikiwemo Pepo la ushoga liondoke nchini !hayo mengine ni mahakama!
 
iseeee!
 
Kuna mwenzao huko sijui burkina faso kala mboko za mataqor mpaka yamechanika chanika kwa upuuzi huu huu
 
Tuondoe sheria za nchi tuishi kwenye maombi. Niamini maombi yanalipa kuliko sheria za nchi, futeni mahakama boresheni nyumba za ibada.
 
Spana za Lissu hizo 😂😂😂
 
Kuombeana ni kwenye mikutano ya dini.
Serikali na vyama vya siasa siyo taasisi za dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…