Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amewataka Watanzania kuwaombea wanaofanya ubadhirifu na wezi ili roho hizo za kuhujumu nchi ziwatoke.
Amesema haiwezekani Rais Samia anahangaika kutafuta fedha ndani na nje ya nchi usiku na mchana na kuzishusha chini halafu hazitumiki kama ilivyokusudiwa, akatolea mfano wa mtu kuongeza idaidi ya manunuzi kuliko kinachohitajika bila aibu. Aliyasema hayo jana 7/6/2024 aliposimamishwa na wananchi katika mapokezi yake Korogwe-Tanga.
CCM mko serious kweli? Kuna Katiba, na Mahakama, zinafanya nini kuhakikisha sheria zinafuatwa? Kwanini tuna mhimili wa Mahakama kama kwa makusudi mnakula kwa urefu wa kamba zenu na hakuna chochote mnafanywa?
Hii ndio shida ya Rais (Mhimili wa serikali) kuwa na madaraka na nguvu kubwa kuliko wengine na yeye kuwa mteule wa viongozi Wakuu kwenye karibu taasisi zote nchini. Unatia aibu na kauli za kijinga namna hii utafikiri huna darasa hata moja kichwani.