GE2025 Nchimbi: CCM sio taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu, jitihada yetu kubwa ni kujiepusha kuwa Serikali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
CCM utajiepushaje kuwa Serikali wakati Mwenyekiti wako wa CCM Taifa ndiye Mtendaji Mkuu wa Serikali yaani Rais wa nchi.
 
Hakika

2030 Kura yangu unayo 😄🙏
Ukiangalia Kwa makini Jamaa pamoja na kusemwa vibaya amejitahidi sana kwakutojihusisha na ufisadi, angalau hiyo mikubwa tunayoisikia kama ni kweli. Kama sivyo Leo angekuwa billionaire Kwa nafasi alizopewa, kama wengine. Sijui kwanini Slow slow anamwona kama threat pengine anajua zaidi kuliko navyomfahamu.
Binafsi na mategemeo makubwa sana mbele ya safari kutoka kwake. Ama pengine mafisadi wameshaona Kuna hatari akipata nafasi kubwa. Nimewaza nje ya box
 
Siamini bana
CCM wanafanyaje money laundering
Kwanza kabisa unaelewa money laundering ni nini?

Tuanzie hapo kwanza. Kwa unavyoelewa wewe, monwy laundering ni nini?

Nataka tupate uelewa wa pamoja tu ili unaposema huamini kuwa CCM wanafanya money laundering, tuwe tuna uelewa wa pamoja wa money laundering ni nini.

So.

Money laundering ni nini kwa uelewa wako?

Pia, fedha haramu ni zaidi ya Money Laundering. Fedha haramu zinaweza kutumika kuingia kwenye siasa kwa donation na rushwa tu bila Money Laundering kufanyika.
 
Serikali haina cheo kinachoitwa mgombea mwenza. Mpaka sasa Nchinbi ni Katibu Mkuu wa CCM hana cheo serikalini.

Kuna contradiction katika maneno yake kwa sababu ingawa ni kweli CCM si serikali, lakininm pia, CCM kama chama tawala ndiyo inayounda serikali na serikali inatekeleza ilani ya CCM.

Ndiyo maana hakuna Waziri asiye mwanachama wa CCM.

Swali la muhimu ni hiki, kwa nini Nchimbi anakwepa wajibu kwenye suala la utakatishaji wa fedha?

Je, CCM inahusika katika utakatishaji wa fedha na Nchimbi anajua hilo na hiyo ndiyo sababu inayomfanya akwepe kujibu swali hiki moja kwa moja?
Umesema vyema, kama hana cheo serikalini anawezaje kuwazuia hao wenye power iwapo watakengeuka Incase wataamua kufanya hivyo? Hata kama ingekuwa wewe ungejibuje. Vyombo husika ndivyo vyenye dhamana na uwezo wa kudhibiti hayo na siyo yeye. Msimwonee!
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mwenza wa Urais wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi, amezungumza na wanahabari leo tarehe 11 Agosti 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba. Akijibu kuhusu jitihada za kudhibiti pesa haramu amesema, "Jitihada yetu kubwa sasa hivi kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kujiepusha kuwa Serikali, kwahiyo sisi sio taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu, kwahiyo wenye kazi yao wataendelea wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha haramu, sisi kama Chama Cha Mapinduzi lazima tufanye kazi ya Siasa. Maana kitu ambacho kinaharibu nchi ni Chama cha Siasa kinapo anza kufanya kazi za dola"

Wanafanyia mikutano ya chama ikulu, tofauti yao na serekali ni ipi? Atafute wa kuhadaa. Wao waendelee kutakatisha pesa chafu na hiyo tone tone.
 
Ukiangalia Kwa makini Jamaa pamoja na kusemwa vibaya amejitahidi sana kwakutojihusisha na ufisadi, angalau hiyo mikubwa tunayoisikia kama ni kweli. Kama sivyo Leo angekuwa billionaire Kwa nafasi alizopewa, kama wengine. Sijui kwanini Slow slow anamwona kama threat pengine anajua zaidi kuliko navyomfahamu.
Binafsi na mategemeo makubwa sana mbele ya safari kutoka kwake. Ama pengine mafisadi wameshaona Kuna hatari akipata nafasi kubwa. Nimewaza nje ya box
Nchimbi anatembea na Falsafa za mzalendo Mustafa Songambele 😄
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Serikali haina cheo kinachoitwa mgombea mwenza. Mpaka sasa Nchinbi ni Katibu Mkuu wa CCM hana cheo serikalini.

Kuna contradiction katika maneno yake kwa sababu ingawa ni kweli CCM si serikali, lakininm pia, CCM kama chama tawala ndiyo inayounda serikali na serikali inatekeleza ilani ya CCM.

Ndiyo maana hakuna Waziri asiye mwanachama wa CCM.

Swali la muhimu ni hiki, kwa nini Nchimbi anakwepa wajibu kwenye suala la utakatishaji wa fedha?

Je, CCM inahusika katika utakatishaji wa fedha na Nchimbi anajua hilo na hiyo ndiyo sababu inayomfanya akwepe kujibu swali hiki moja kwa moja?
Hata namimi nimeshangaa au haujui kama ccm ndio chama kiricho madarakani? Dr hapo kaniangusha.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mwenza wa Urais wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi, amezungumza na wanahabari leo tarehe 11 Agosti 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba. Akijibu kuhusu jitihada za kudhibiti pesa haramu amesema, "Jitihada yetu kubwa sasa hivi kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kujiepusha kuwa Serikali, kwahiyo sisi sio taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu, kwahiyo wenye kazi yao wataendelea wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha haramu, sisi kama Chama Cha Mapinduzi lazima tufanye kazi ya Siasa. Maana kitu ambacho kinaharibu nchi ni Chama cha Siasa kinapo anza kufanya kazi za dola"

Umesema vyema, kama hana cheo serikalini anawezaje kuwazuia hao wenye power iwapo watakengeuka Incase wataamua kufanya hivyo? Hata kama ingekuwa wewe ungejibuje. Vyombo husika ndivyo vyenye dhamana na uwezo wa kudhibiti hayo na siyo yeye. Msimwonee!
Hapana,

Chama kina uwezo wa kumuwajibisha mwanachama yeyote anayekiuka misingi ya chama.

Kwa mfano, chama kina kanuni dhidi ya rushwa, kiongozi wa serikali aliye mwanachama wa CCM, kama Waziri, anawajibika kufuata kanuni hizo na kuzi advance ziwe katika kanuni za serikali.

Kwa sababu serikali inatekeleza ilani ya chama.

Sasa hapo kiongozi wa chama anapataje uhalali wa kusema chama si serikali na wao kazi yao si kuzuia fedha haramu?

Ina maana CCM haina Anti Money Laundering policy kabisaa?

Na kama haina, hii ina tofauti gani na kubariki Money Laundering na kubariki kupokea pesa chafu?
 
Hata namimi nimeshangaa au haujui kama ccm ndio chama kiricho madarakani? Dr hapo kaniangusha.
Anajua sana.

Ila labda pia anajua kwamba CCM inapokea pesa chafu bila kuhoji zilipotoka, na hivyo, anaepuka wajibu wa kuhakikisha pesa wanazopokea ni safi.
 
Hii kauli ya kujiepusha kuwa serikali itachanganya watu sasa hivi.
Ana maana kwamba wao wanachotaka ni hela kutoka chanzo chochote hata kama ni wauza unga, hayo ya kuchunguza fedha za watu zilikotoka iachiwe serikali
 
Sawa,

Lakini mbona kwenye mambo mengine mengi wanajinadi chama ndiyo kinaongoza serikali? Serikali ya CCM hivi, serikali ya Samia vile. Samia kafanya hiki, CCM imefanya kile.

Kwenye hili all of a sudden chama hakitaki kuiingilia serikali?

Does CCM even have an Anti Money Laundering Policy? Even one that is just for show?
 
Kwanza kabisa unaelewa money laundering ni nini?

Tuanzie hapo kwanza. Kwa unavyoelewa wewe, monwy laundering ni nini?

Nataka tupate uelewa wa pamoja tu ili unaposema huamini kuwa CCM wanafanya money laundering, tuwe tuna uelewa wa pamoja wa money laundering ni nini.

So.

Money laundering ni nini kwa uelewa wako?

Pia, fedha haramu ni zaidi ya Money Laundering. Fedha haramu zinaweza kutumika kuingia kwenye siasa kwa donation na rushwa tu bila Money Laundering kufanyika.
Money laundering ni kuchukua fedha inayotokana na vyanzo haramu(corruption,tax avoidance,drugs,robbery,huma trafficking,terrorism etc etc ) kuingiza mfumo halali wa kibenki (financial system)
Kuna stage 3 zinatumika
Placement(kuatamisha)
Layering (conceal the source)
Integration (into legitimate financial institution)

Mkuu naomba unirekebishe
Source :Google
 
Ubuntu botho! By Mamelod Sandowns FC ya Afrika Kusini
 
Sawa,

Lakini mbona kwenye mambo mengine mengi wanajinadi chama ndiyo kinaongoza serikali? Serikali ya CCM hivi, serikali ya Samia vile. Samia kafanya hiki, CCM imefanya kile.

Kwenye hili all of a sudden chama hakitaki kuiingilia serikali?

Does CCM even have an Anti Money Laundering Policy? Even one that is just for show?
Anachotaka Nchimbi ni hela tu, hakuna kingine, mfuatilie tangu UVCCM utamuelewa vizuri
 
Back
Top Bottom