Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mwenza wa Urais wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi, amezungumza na wanahabari leo tarehe 11 Agosti 2025 katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba. Akijibu kuhusu jitihada za kudhibiti pesa haramu amesema, "Jitihada yetu kubwa sasa hivi kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kujiepusha kuwa Serikali, kwahiyo sisi sio taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu, kwahiyo wenye kazi yao wataendelea wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha haramu, sisi kama Chama Cha Mapinduzi lazima tufanye kazi ya Siasa. Maana kitu ambacho kinaharibu nchi ni Chama cha Siasa kinapo anza kufanya kazi za dola"