Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa, wanaharakati, na jamii kwa ujumla kuacha kurejea matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ili kuruhusu Tume ya Rais kukamilisha uchunguzi wake bila upendeleo.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Februari 2, 2026, akiwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshaunda Tume maalum ya kuchunguza kiini cha matukio hayo na tayari imeanza kazi. Amesisitiza kuwa kuendelea kuyazungumzia matukio hayo hadharani ni kinyume na mfumo wa kisheria na ni kutoitendea haki nchi.