Nchini Namibia, mshahara wa security guard ni mkubwa kuliko wa profesa UDSM

Nchini Namibia, mshahara wa security guard ni mkubwa kuliko wa profesa UDSM

Nchi ya Namibia imefanya mambo makubwa sana, mpk unajiuliza Tanzania tulikosea wapi siye? Nadhani tumefika hapa kwasabb ya siasa chafu na uongozi mbovu. Namibia ina rasilimali gani za kuizidi Tanzania hadi wao wawe mbali kiasi hiki?
1. Wazee wanalipwa.
2. Walemavu wanalipwa.
3. Matibabu kwa wazee, wajawazito na watoto ni bure.
4. Elimu mpk chuo kikuu ni bure.
5. Barabara zao zimepigwa ile lami ya ukweli, hakuna uchakachuaji.

Njoo kwa upande wa mishahara ya watumishi ni kufuru. Mlinzi (security guard) analipwa vizuri kuliko maprofesa wa vyuo vikuu barani Afrika. Mapolisi na walimu wana mishahara mikubwa kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya.

Hapa kwetu ni 5% tu ya watumishi wa umma ndiyo wanalipwa 1.5M ama zaidi kwa mwezi. Hii siyo mishahara, ni posho.

View attachment 3014523
Hakuna uajabu wowote,Namibia ni Nchi Tajiri wa Madini na wako chini ya Milioni 2,huwezi linganisha na Tanzania yenye over 65mln people,kubwa kieneo na Rasilimali za kutunga unga.
 
Nimesoma maelezo ya wengi mpo kwenye idadi ya watu hicho sio kigezo wenzetu ni waadilifu na mali za umma hata wangekua wengi bado maisha wangewatengenezea wasio kuwa nacho hakuna kwa Nchi za SADC Tanzania ni moja ya Nchi yenye mali nyingi sana ila watu wake wanapata tabu tuu wanaonufaika ni wachache...
 
Siri kubwa ni hii Serikali za nchi hizo zinamiliki na kufanya biashara za rasilimali za nje ndio chanzo cha kupata pesa za surplus mpaka kulipa wazee na kuweka huduma za bure .

Nchi zote kama nchi uchumi wa madini basi serikali ni anafanya biashara yeye ndio maana wanakuwa na pesa nyingi , rejea dubai kweny mafuta kuanzia mwaka 90 mpaka sasa ni mafuta .

Sasa serikali ya Afghanstan inauza mafuta kweny nje na kuingia pesa kibao kwa siku , siku chache utasikia wanawake wanalipwa mishahara ya bure , elimu bure mpaka chuo , ukioa unapewa pesa za bure ....

Acheni kudanganywa eti muwape wawekazji halafu wakipata trill 1 nyie mnapewa Bill kadhaa ....Ukitaka nchi ipate maendeleo serikali iwekeze na kufanya biashara mtaishi kama wafalme .

China kweny biashara serikali inashika karibia 60% ya biasharaza zote .

Pesa za kodi huwezi kuendelea hata siku moja kwa sababu hata walipa kodi wengi ni janja sana wanakimbia ...Nchi zote kama za Asia serikali zao ndio zinamiliki uchumi na wana viongozi wazalendo.

View attachment 3014528
Tanzania tuna mashirika yetu toka enzi ya mwalimu wamepewa mandate ya kufanya hayo unayoeleza lakini matokeo yake wameua ,kumbe ulitaka Serikali iendelee kuwachekea? Bora Kugawana na wenye uwezo kuliko hasara ya Moja kwa Moja.

Jambo Moja usilolijua ni kwamba Watanzania sio na Wala hawajawahi kuwa waadilifu ni wezi,wenye tamaa na wafitini plus uvivu na ubinafsi.

Ni wachache hufanya mambo Kwa maslahi ya Umma nao hupigwa vita maana ni wachache,hata ukisema zitungwe sheria Kali wanaosema hivyo ni wale ambao wanatafuta nafasi wakipata hawatungi ,then unategemea nini?

Mwisho ni 20% tuu ya mashirika yote Duniani yanamilikiwa na Serikali so usiongee kana kwamba hiyo ndio alfa na omega wakati sio kweli.
 
Hakuna uajabu wowote,Namibia ni Nchi Tajiri wa Madini na wako chini ya Milioni 2,huwezi linganisha na Tanzania yenye over 65mln people,kubwa kieneo na Rasilimali za kutunga unga.

Kila siku mitanganyika inaambiwa TZ ni tajiri sana dunia nzima inatuonea wivu, kumbe ukitoa tanzanite madini ya kutengeneza pete hamna kingine chochote cha maana kisichopatikana nchi zingine tena kwa wingi kuliko bongo. Watanganyika walijazwa ujinga sana.
 
Ni kwa sababu kwa kiasi kikubwa mfumo wa biashara Namibia unaendeshwa na serikali na kutengeneza faida kubwa
 
Kila siku mitanganyika inaambiwa TZ ni tajiri sana dunia nzima inatuonea wivu, kumbe ukitoa tanzanite madini ya kutengeneza pete hamna kingine chochote cha maana kisichopatikana nchi zingine tena kwa wingi kuliko bongo. Watanganyika walijazwa ujinga sana.
Ni ujinga wa Watanzania Kwa sababu hawana maarifa na ni washamba wasio na exposure.

Namibia ni Tajiri wa Uranium,Gas na Maarufu Kwa Uvuvi hapa Africa on top of vivutio vya Utalii.

Pia juzi tuu hapo wamegundua Mafuta zaidi ya mapipa Bilioni 10,watakuwa namba 3 Kwa reserves hapa Afrika nyuma ya Libya na Nigeria.

Mpaka hapo watagawana sana madola Hadi wawe wanalalia Namibia yafanya ugunduzi mkubwa wa mafuta wa zaidi ya Mapipa Bilioni 10. Yajiandaa kujiunga na OPEC
 
Siri kubwa ni hii Serikali za nchi hizo zinamiliki na kufanya biashara za rasilimali za nje ndio chanzo cha kupata pesa za surplus mpaka kulipa wazee na kuweka huduma za bure .

Nchi zote kama nchi uchumi wa madini basi serikali ni anafanya biashara yeye ndio maana wanakuwa na pesa nyingi , rejea dubai kweny mafuta kuanzia mwaka 90 mpaka sasa ni mafuta .

Sasa serikali ya Afghanstan inauza mafuta kweny nje na kuingia pesa kibao kwa siku , siku chache utasikia wanawake wanalipwa mishahara ya bure , elimu bure mpaka chuo , ukioa unapewa pesa za bure ....

Acheni kudanganywa eti muwape wawekazji halafu wakipata trill 1 nyie mnapewa Bill kadhaa ....Ukitaka nchi ipate maendeleo serikali iwekeze na kufanya biashara mtaishi kama wafalme .

China kweny biashara serikali inashika karibia 60% ya biasharaza zote .

Pesa za kodi huwezi kuendelea hata siku moja kwa sababu hata walipa kodi wengi ni janja sana wanakimbia ...Nchi zote kama za Asia serikali zao ndio zinamiliki uchumi na wana viongozi wazalendo.

View attachment 3014528
Silaha kubwa ya maendeleo ni uzalendo wa hali ya juu kwa wananchi na viongozi pamoja na sheria kali za kudhibiti wizi wa mali za umma.

Katika kipindi cha ujamaa, serikali ilifanya biashara, viwanda karibu kila mkoa, lakini leo vipo wapi hivyo viwanda? Serikali kufanya biashara bila uzalendo na sheria kali, basi ni kuwatajirisha viongozi tu!

Kuna siku nilikuwa nafuatilia makala fulani, kwamba nchini Botswana, rais ndiye anasimamia mauzo ya madini nje ya nchi. Mwisho wa siku tunaona Botswana ikipiga hatua kwa sababu viongozi wanauzalendo na kuwakumbuka wananchi! Vipi viongozi wa bongo ndiyo wawe wanasimamia uuzaji wa madini nje ya nchi?
 
Ni ujinga wa Watanzania Kwa sababu hawana maarifa na ni washamba wasio na exposure.

Namibia ni Tajiri wa Uranium,Gas na Maarufu Kwa Uvuvi hapa Africa on top of vivutio vya Utalii.

Pia juzi tuu hapo wamegundua Mafuta zaidi ya mapipa Bilioni 10,watakuwa namba 3 Kwa reserves hapa Afrika nyuma ya Libya na Nigeria.

Mpaka hapo watagawana sana madola Hadi wawe wanalalia Namibia yafanya ugunduzi mkubwa wa mafuta wa zaidi ya Mapipa Bilioni 10. Yajiandaa kujiunga na OPEC

Watanganyika wasome haya waache kujiona special na kujidanganya kwa utajiri hewa. Tunawaambia kila siku TZ haizalishi wala haingozi kwa reserve ya kitu chochote cha msingi kuanzia mafuta, gas, madini, maji, ardhi, kilimo chochote kile nk nk.

cc johnthebaptist
 
Aisee! Kweli. Kama gesi ya Mtwara migodi yote ya madini nchi hii ingewndeshwa na serikali kwa ufanisi tungekuwa mbali sana. Hapo hatujaweka utalii, uvuvi na bandari zetu.
Rais tuliyenae nae anaturudisha nyuma na kulitia taifa Hasara...Yaani kuongozwa na mwanamke kitaifa ni dhambi mpaka mbinguni....Magufuri alitutendea vibaya sana kufa akatuachia huyu mwanamke....Yaani Raisi anateua mpaka waliokwisha Fariki???
 
Kama kulipa likizo ya mwaka ambayo ipo kisheria mtumishi kulipwa mara moja kila baada ya miaka 2 imekuwa shida ije kuwa mishahara! Uliza watumishi wa halmashauri wenye likizo juni ambao tayari wamelipwa! Leo tarehe 12/6. Hapa ndiyo inakuja Ile dhana kwamba ALL ANIMALS ARE EQUAL BUT OTHER ANIMALS ARE MORE EQUAL. (Animal farm).
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Nchi ya Namibia imefanya mambo makubwa sana, mpk unajiuliza Tanzania tulikosea wapi siye? Nadhani tumefika hapa kwasabb ya siasa chafu na uongozi mbovu. Namibia ina rasilimali gani za kuizidi Tanzania hadi wao wawe mbali kiasi hiki?
1. Wazee wanalipwa.
2. Walemavu wanalipwa.
3. Matibabu kwa wazee, wajawazito na watoto ni bure.
4. Elimu mpk chuo kikuu ni bure.
5. Barabara zao zimepigwa ile lami ya ukweli, hakuna uchakachuaji.

Njoo kwa upande wa mishahara ya watumishi ni kufuru. Mlinzi (security guard) analipwa vizuri kuliko maprofesa wa vyuo vikuu barani Afrika. Mapolisi na walimu wana mishahara mikubwa kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya.

Hapa kwetu ni 5% tu ya watumishi wa umma ndiyo wanalipwa 1.5M ama zaidi kwa mwezi. Hii siyo mishahara, ni posho.

View attachment 3014523
Niliposoma title ya uzi wako, nikadhani na UDSM nayo ipo huko unakoilinganishia na vya huko..!!
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Beba juice zako za Azam peleka Namibia uone kama mifumo yao itakuruhusu kuuza. Au nenda jaribu kufungua store ya kuuza bidhaa za chakula kutoka nchi tofauti na South Africa uone kama utaweza. Au nenda Kusini mwa nchi uone kina nani wanamliki ranch za mifugo, au nani wanamiliki kampuni za uvuvi.

Vyote vikubwa vinafanywa na makaburu, na wao raia wao wanatamani huu mfumo wa kuitegemea South Africa na makaburu wake ukome. Kila nchi na mabaya yake.
 
Serikali ikifanya biashara lazima iwe na pesa.......

kwa mfano NHC imeundwa tokea enzi za nyerere lakini hadi leo shirika hilo halina maendeleo yoyote
TANESCO ndio shirika lenye kuleta skendo za ufujaji pesa rejea eskrow acc, richmond...

DART Ni kichaka cha kupiga pesa

TPDC, hamna la maana wanalolifanya

SIDO hamna la maana ktk kuwezesha wajasiriamali ktk kumiliki na maendeleo ya viwanda vidogo kuwa vikubwa

NHIF ni kichaka cha upigaji pesa

TTCL ni heri waifute tu

Tanzania tuna upungufu wa watu wenye nia njema ya maliasili za taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja, wengi wapo kujilimbikizia mali wenyewe na wapo tayari kuona shirika au kampuni ya serikali ikifanya vibaya lakini wao ndio wanufaike
nchi inahitaji sheria ngumu kama zile za china ili wote tuwe wazalendo

japo hakuna chama cha upinzani sahihi cha kuchukua madaraka kwa sasa lakini ccm ilipaswa iwekwe pembeni waje wengne wenye mawazo mbadala na sio hawa walafi wa madaraka
 
Back
Top Bottom