Ndaisaba Ruhoro Ameishauri Wizara ya Nishati Kuweka Fedha za Kutosha kwa Ajili ya Nishati Safi ya Kupika

Ndaisaba Ruhoro Ameishauri Wizara ya Nishati Kuweka Fedha za Kutosha kwa Ajili ya Nishati Safi ya Kupika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. NDAISABA RUHORO AMEISHAURI WIZARA YA NISHATI KUWEKA FEDHA ZA KUTOSHA KWA AJILI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

"Rais Samia ameona ni muda muafaka tuendeleze rasilimali ya Gesi Asilia ambayo MUNGU ametupatia Watanzania. Wananchi wa Ngara tunamuunga mkono Rais na timu nzima ya Wizara ya Nishati, nendeni mkaweke fedha za kutosha ili watanzania tuondokaneni na adha ya kutumia nishati chafu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Tunaposema nishati chafu tunazungumzia matumizi ya Kuni, Mkaa na Mafuta ya Taa kwenye kupikia. Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia itawafanya Watanzania, akina Mama, Wababa na Watoto wasiende maporini kutafuta Kuni na Mkaa kwa ajili ya kupikia." - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Kuna Watanzania macho yao yalikuwa yanaathiriwa na moshi maeneo kama ya Kanda ya Ziwa baadhi ya wazee vikongwe waliuliwa wakiitwa ni Wachawi kwasababu wanapikia Kuni na Matokeo ya zile Kuni ni ule Moshi wenye Kaboni na Kemikali nyingi zinaua macho yao yanakuwa mekundu, watu walipigwa mapanga kwasababu ya Nishati chafu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Naomba Watanzania waelewe, tunaposema nishati safi ni kuondokana na hii adha ya kutumia nishati chafu ambayo imegharimu maisha mengi ya watanzania. Muda ambao akina Mama walikuwa wanautumia kwenda kutafuta Kuni sasa watautumia kufanya shughuli zingine za uzalishaji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Katika uharibifu wa Mazingira, miti imekatwa sana, watu wanafanya nishati chafu kama chanzo cha biashara. Mtu amekata miti anachoma mikaa na kuharibu Misitu matokeo Dar es Salaam wanaingia adha ya ukosefu wa Maji kwasababu miti mingi ya Mto Ruvu imekatwa ambako ndipo Maji yanapozalishwa" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Nia na lengo la mradi wa LNG ni kwenda kuwaokoa Watanzania. Wizara ya Nishati wekeni fedha za kutosha ili miradi ikatekelezwe iende kuwasaidia Watanzania" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Kwa upande wa REA, Tanzania 🇹🇿 ina Vijiji zaidi ya 10,800 na kati yake Vijiji zaidi ya 10,000 vimeweza kuwashwa Umeme, vimebaki Vijiji vichache Nchi nzima. Waziri wa Nishati twende tukawashe Umeme Kijiji cha Mrusagamba ambacho tangu Mungu akiumbe hakijawahi kuwa na Umeme" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Nikuombe Waziri wa Nishati kule Ngara niongezee hata vitongoji 10 au 20 ili vitongoji vinavyotaka Umeme. Ulipokuja Ngara kwenye mradi wa Rusumo nilikuomba unisaidie kwenye mitaa 17 ya Rulenge ambayo haina huduma ya umeme kabisa, ile ni Mamlaka ya Mji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
 
Back
Top Bottom