sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Kuelekea mtanange wetu dhidi ya Ndada FC, huko Nangwanda Sijaona 15/09/2018 (Jumamosi ya wiki hii).. Hebu tuangalie mbili tatu za Simba SC katika kipindi hiki cha International Break.
Kipindi hiki kimekua na faida kwetu kwani, tumeuwasha moto vilivyo kila kona. Hali hii inanifanya niwaonee huruma sana Ndada FC. Kwanini? Ungana nami;
1. Kagere alipata mazoezi ya kutosha pale timu yake ya Rwanda ilipopambana na miamba Ivory Coast. Achilia mbali na ile stori ya kumlaza na viatu beki bora duniani, Erick Bailly, jamaa aliingia kambani siku hiyo. Pia siku hiyo Niyonzima alichowafanya hao jamaa, hawatakisahau.
2. Le Capitain, Bocco alitupia kambani goli 2 dhidi ya timu yenye beki ngumu kabisa ukanda huu wa CECAFA, AFC Leopards. Kama si "ubishi" wa Amunike haya magoli yalitakiwa yafungwe nchini Uganda.
3. Ubovu wa uwanja ulimzua 'CR7 wa Uganda Okwi kufanya yake pale nchini Uganda.. Ila shughuli aliyowapa mabeki wa timu yenye wachezaji wenye uraia wa Tanzania, haikua nyepesi. Wenyewe walikiri kama uwanja ungekua vizuri, siku hiyo walikua wanaaibika.
4. Unamkumbuka Juuko Murshidi.. Huyu jamaa alimuweka kabisa mfukoni, Mtanzania pekee aliyetungiwa nyimbo na Wazungu, Samata.
5. Yule kiungo mwenye uwezo wa kufunga, kupiga pasi ndefu na fupi, anayeweza kutumia nguvu na anayeweza kushindana na viungo wagumu, Ndugu Chama alikiwasha katika timu yake ya Taifa, ya Zambia. Aliiupiga mwingi mnoo asikuambie mtu.
6. Marcel Kaheza alianza kurudisha hela yetu kwa kufunga goli ambalo tumezoea kuliona EPL pekee, sasa jamaa ameanza kuyaleta magoli sampuli hiyo Tanzania. Niseme nini Kuhusu Mo Ibrahim?! Kwa mpira alioupiga dhidi ya AFC Leopards, amempa kocha wakati mgumu sana kupanga 1st eleven.
Natanguza Pole zangu za dhati kwa Ndada Football Club.
Nikiripoti toka Kigali International Airport.. Ni Mimi sembo wa Simba TIIIIIIIIVIIIIIIIIIIIIIIIII (in George Malatu Voice)