NDANDA: Mtwara na Dar-es-Salaam wapi kwenu?

NDANDA: Mtwara na Dar-es-Salaam wapi kwenu?

Betterhalf

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
2,882
Reaction score
2,560
Jana timu ya Ndanda imefanya maadhimisho ya siku yao "NDANDA Day".
Kupitia siku hii shughuli mbalimbali hufanyika kama vile usafi n.k.
Hongereni kwa hilo ingawa nina maswali kadhaa ya kujiuliza.
1.Timu imehamisha makazi yake Mtwara?
2.Kwa nini utambulisho usifanyike Mtwara kama ilivyokuwa mwaka jana?
3.Wana Mtwara wawaeleweni vipi?
4.Mliomba ridhaa ya wana Mtwara?
5.Kwa nini msiwaombe radhi wana Mtwara kwa hili?
6.Kwa shughuli ya kutembelea wagonjwa, je hospitali ya Ligula haikustahili au haikuwa na hadhi hiyo?
Naamini Mtwara ni bora zaidi kwa kuwa tungeshawishi viongozi wa mkoa kama vile RC, ma-DC,ma-DED,Wabunge,wawekezaji na wadau wengine kuiunga mkono timu yetu.
Poleni kwa yote.
Nawasilisha.

The Great Gatsby
 
Sisi kama wana mtwara tumechukizwa sana na jambo hili...
Hii ni dharau kubwa sana kwetu na usaliti usiokubalika..wametuvunjwa moyo kabisa...
binafsi nimewasamehe na sitegemi hili kujirudia tena
 
Watendaji wa timu wajifunze kutokana na hili.

The Great Gatsby
 
Uongozi wa club uwajibike kwa hili... Mwenyewe nimejiuliza mambo mengi saaana, kwa Ndanda FC waje Dar!... Lakini yule kiongozi wao wakati anahojiwa juzi, alikuwa pale white sand, mbezi Beach kajipumzikia tu.... Sasa nahisi, kuna nguvu ya pesa ya hawa wadhamini wapya wa Boko, labda wakifanyia Dar, ni kitovu kizuri kwa media na wateja wa bidhaa zao kutangazwa....

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Ni kweli, lakini wangapi waliopo Dar wana habari na NDANDA?
NDANDA hupata heshima zaidi wakiwa Mtwara na kwenye wilaya zake kama Tandahimba,Newala,Masasi n.k. kuliko sehemu nyingine. Hali hii ni tofauti na Yanga na Simba ambazo hata wakienda Kigoma, Mwanza na kwingineko wanaweza kuvutia mashabiki.
Dharau hizi zimeanza wakati wa trials ambapo walizunguka na lundo kubwa la U20 bila ya wachezaji hata wawili wa first team(achilia mbali first eleven). Kwa hali hiyo, mashabiki waliona hiyo ni dharau na hivyo hamasa ilipungua na hivyo kukosa mapato.
Viongozi wabadilike, kama wataona inafaa.

The Great Gatsby
 
Nafikiri Ndanda vs Azam kesho...wote watakuwa ugenini.

The Great Gatsby
 
Back
Top Bottom