BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa amesema ndani ya muda huo jumla ya ajali 1,177 zilitokea huku 135 zikiwa za magari ya Serikali ambayo ni sawa na 11.5% kwa mwaka 2022
Takwimu hizo pia zinaonesha mwaka 2021 ajali zote zilizotokea zilikuwa 1,698 kati ya hizo ajali 158 zilitokana na magari ya serikali ambayo ni 9.3%. Vifo vilikuwa ni 1,245. Kati yake, ajali za magari ya serikali ni vifo 94 sawa na 7.6%
Kamanda Mutafungwa amesema ili kudhibiti ajali, elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Serikali ni muhimu kwao kwa kuwa wanapaswa kulinda uhai wao na wateja wao kwa kutambua kuwa hawako juu ya sheria na wanapaswa kutii sheria kama madereva wengine.
============================
KIKOSI cha Usalama Barabarani nchini kimetaja takwimu mbalimbali za ajali mwaka huu, kikibainisha kuwa ndani ya miezi minane ya mwanzo ajali 1,177 zilitokea huku 135 zikiwa za magari ya serikali, sawa na asilimia 11.5.
Kutokana na hali hiyo, kikosi hicho kimetoa elimu kwa madereva wa magari ya serikali na kuwataka kuacha mihemko kwa kuwa hawako juu ya sheria.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mafunzo maalum ya elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa magari ya viongozi wa serikali na wabunge jijini hapo, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa, alisema ajali hizo za magari ya serikali zimetokea kwa kipindi cha Januari hadi Agosti 2022.
Kamanda Mutafungwa alisema ili kudhibiti ajali, elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa serikali ni muhimu kwao kwa kuwa wanapaswa kulinda uhai wao na wateja wao kwa kuheshimu na kutii sheria.
Alisema madereva hao wanapaswa kujitambua kuwa hawako juu ya sheria na wanapaswa kutii sheria kama madereva wengine.
"Waache kutumia vyeo na ukuu wa viongozi wao ambao siyo madereva wa magari ya serikali kwa kuwa wameajiriwa kwa majukumu mengine na siyo udereva tu, dereva hapaswi kuwa na mihemko na anatakiwa kujiepusha na 'makandokando' yanayoweza kupelekea apoteze weledi katika kazi zake, mfano ulevi na kuheshimu sheria ya mwendokasi," alisema.
Alisisitiza wataendelea kusimamia sheria bila kumwonea dereva yeyote na atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kuwafungia au kufuta leseni.
Akizungumzia takwimu hizo za ajali, alisema ndani ya kipindi hicho, vifo vyote vilikuwa 1,038 ambapo kati yake, vifo 90 vilitokana na ajali za magari ya serikali, sawa na 8.7 huku majeruhi wa magari hayo wakiwa 211.
Katika kipindi cha mwaka 2020, Kamanda Mutafungwa alisema ajali zote zilizotokea zilikuwa 1,714 na kati ya hizo ajali 260 zilikuwa za magari ya serikali na kusababisha vifo 82, sawa na asilimia 6.5.
"Kwa mwaka 2021 ajali zote zilizotokea zilikuwa 1,698 kati ya hizo ajali 158 zilitokana na magari ya serikali sawa na asilimia 9.3. Vifo vilikuwa ni 1,245. Kati yake, ajali za magari ya serikali ni vifo 94 sawa asilimia 7.6," alifafanua.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini alisema elimu hiyo iliyotolewa kwa madereva hao ni muhimu kutolewa kwa viongozi wao huku akisisitiza sheria kuchukuliwa kwa yeyote atakayekiuka.
Chanzo: Nipashe