Tunajua kwamba hata Magufuli anaposema "Nitajenga barabara" haimaanishi kwamba yeye ndiye mwenye hela au kwamba atakuwa saiti akijenga. Anatumia vyombo vilivyopo kujenga barabara n.k.
Tundu Lissu amefanikiwa kwa ushawishi wake na umahiri mkubwa wa kujenga hoja zinazowafanya waliopo madarakani kuamka usingizini na kuanza kutekeleza mara moja maono ya Lissu kwani wanajua ndio matakwa ya wananchi. Kwa hili, Lissu amefanikiwa kufanya aliyoshindwa kufanya Magufuli kwa miaka mitano:
1. Walimu 13,000 ambao serekali imetangaza kuwapa ajira mpya wiki juzi
2. Wamachinga ambao Magufuli kawaambia si lazima tena kulipia elfu 20 kupata kitambulisho wiki jana
3. Kuanzia mwezi huu mshahara kima cha chini serekalini umepanda
4. Watu kujisikia huru tena na kuthubutu hata kumkosoa Rais hadharani
5. Chama cha Mapinduzi kutambua kuwa hakijafanya wanayotaka wananchi na kwamba matatizo ya msingi ya wananchi hayajaguswa
6. Lissu ameifanya CCM kugundua kuwa ni chama kisichopendwa na wengi na hakina hati miliki ya siasa za Tanzania
7. Kwamba hakuna mtu anayeweza kuuwa upinzani na harakati za kisiasa isipokuwa wanachi wenyewe.
8. Serikali kugundua kwamba kujaribu kuuzima upinzani ndio kuufanya uwe imara na wenye nguvu zaidi
9. Watu wameelewa kuwa vyama vya upinzani ni muhimu hata kama chama tawala kinaongozwa na "malaika".
10. Kwa mara ya kwanza baada ya kuwa anawafokea tu kwa miaka 5, watanzania wamemwona mgombea urais wa CCM akiongea nao kwa kuwabembeleza, haya ni mafanikio makubwa kwa Lissu ndani ya mwezi mmoja tu.