Ndege anaweza kupaa kwenye vacuum?

Ndege anaweza kupaa kwenye vacuum?

Kama nilivyoandika kwamba sina uhakika sana kwa maana kuna mambo mengi, na kuna hili lililonijia kichwani baada ya kufikiria kidogo kuhusu Ndege kuweza kuruka kwenye vacuum, nimefikiria kwamba ili ndege aruke ni lazima kuwe na hewa/upepo ambayo ndiyo kwa kutumia mabawa yake humuwezesha kwenda mbele hivyo ili ndege aweze kwenye mbele au kuruka ni lazima kuwe na nguvu ya msuguano kati ya ndege/mabawa na hewa/upepo, sasa kama kwenye vacuum hakuna kitu ina maana hata hewa hakuna mabawa yatawezaje kumpeleka mbele ndege? Hivyo nafikiri hatoweza kuruka kwenye vacuum, ingawaje bado sina uhakika, ninaendelea kulifikiria!
Sasa mkuu umesema vacuum ni kutokuwa na hewa hata kidogo means hamna hewa kabisa sasa huyo ndege atapaaje sehem ambapo hakuna hewa atawezaje ku kishi bila ya hewa
 
Sauti haiwezi safiri kwenye vacuum inahitaji medium ambayo itatetemesha particles zake na ziweze kuambukizana hadi kufika kwenye destination

Kwenye ishu ya ndege pale kuna Laws za motion na law of flotation.

Kwenye ile law inasema " Action and reaction equal and oposite " hiii ndio ndege huitumia sana anatengeneza action kutumia wings then anatumia reaction ya air kueleka mbele na upande anaotaka.
 
Sasa mkuu umesema vacuum ni kutokuwa na hewa hata kidogo means hamna hewa kabisa sasa huyo ndege atapaaje sehem ambapo hakuna hewa atawezaje ku kishi bila ya hewa


Kwenye Fizikia sehemu kubwa sana ni nadharia au idealization hata hiyo vacuum yenyewe ni nadharia tu hakuna anayeweza kutengeneza vacuum, hivyo hapa kinachojadiliwa ni nadharia, ni kama vile ether Wanafizikia waliamini kwa miaka mingi kuna ether ambayo Mwanga hutumia kusafiri na hiyo imekuja kuachwa kuaminiwa hivi karibuni tu, hivyo siku zote kumbuka hilo Fizikia sehemu kubwa ni idealization tu!
 
Vacuum that means nothing exists, hivyo ndege hawezi paa kwasababu hataweza kutua, so atabakia pale atakapokuwa.
 
Nackiaga vacuum vacuum
Kwan mfano wa vacuum Katika mazngira ya Kawaida Ni UPI ????
 
Vacuum that means nothing exists, hivyo ndege hawezi paa kwasababu hataweza kutua, so atabakia pale atakapokuwa.
Household vaccum.cleaner

But km.jamaa.alivyo sema juu kwama hakuna vaccum iliyo sahihi..yaan km 100% imakamilika

Ila kwa dunia ya sasa tunaita vaccum kwa zile ambazo zimeondolewa molecular gar kwa kiasi kikubwa
 
Hiwezekanai ndege kupaa kwenye Vaccuum kwa sababu kwenye vacuum hakuna hewa. Ndege hutumia hewa kutengeneza tofauti ya mgandamizo ( difference in pressure) ambayo hiyo tofauti husababisha ndege kunyanyuka juu na hapo pia hujiendesha kwa kutumia mbawa zake. Hii yote hutegemea uwepo wa hewa. Bila hewa haiwezi fanyika. Hivyo basi, chochote ili kiweze kuruka ni lazima hewa iwepo. ( upande wa roketi ni suala jingine)
 
Kisayansi atakuwa anaelea koz kwenye vavuum kuna zero gravity. Kwa ninavyokumbuka
Acha uongo, si kweli kuwa kwenye vacuum g ni zero, g ipo kama kawa, labda hiyo vacuum iwe anga za mbali (space). Shortly, vacuum has no effect on gravity.
 
acceleration due to gravity kwenye vacuum huwa ni kubwa kuliko kwengineko ajili hamna friction na hewa ama kinginecho, hivyo napingana na wanaosema ati hamna gravity kwenye vacuum
Acceleration due to gravity inategemea umbali kati ya body na USO wa dunia. Acceleration due to gravity is maximum at the earth's surface (9.8m/S²) but as you move a certain heigh away from the earth's surface the value of acceleration due to gravity decrease. Also as you move a certain distance from the earths surface toward the earths center its value decrease! We should note that the value of acceleration due to gravity can not be affected by vacuum! It's magnitude depend only on it's position from the earth's surface.
 
Acha uongo, si kweli kuwa kwenye vacuum g ni zero, g ipo kama kawa, labda hiyo vacuum iwe anga za mbali (space). Shortly, vacuum has no effect on gravity.

Mkuu mahala pekee ambapo pana G ni duniani kwamaana dunia na koti lake
Nje ya dunia hakina G

Na inasemwa ndani ya dunia hakina vacuum labda za kutengeneza ambazo sio pure 100%

Kwa msingi huo basi maana yake ni kwamba vacuum ipo nje ya dunia ambako hamma G

Hebu ninasilishe hii dhana yangu mkuu nikuelewe
 
Nackiaga vacuum vacuum
Kwan mfano wa vacuum Katika mazngira ya Kawaida Ni UPI ????
neno vacuum linamaanisha tupu/mahali ambapo hakuna kitu chochote yani no air no anything..
mara nyingi binadamu amekuwa akitengeneza utupu huo lkn sio timilifu wa asilimia mia! hivyo kwa kiwangohicho tunachotengeneza hiyo hali ya utupu tunaita tu lkn haijatimia.
kuhusu kwenye mazingira sehemu ambapo kuna vacuum hilo sifahamu lkn nijuavyo kwa hapa duniani hakuna labda huko anga za mbali..

i think you get it
 
Naona mnaongelea elementary physics

Ndege inaruka na kutua kwenye vacuum lakini it depends na engine yake. Hapa sizungumzii engine za mapangaboi... nazungumzia engines kama zile za space shuttles
 
Naona mnaongelea elementary physics

Ndege inaruka na kutua kwenye vacuum lakini it depends na engine yake. Hapa sizungumzii engine za mapangaboi... nazungumzia engines kama zile za space shuttles
Unataka kuniambia huko anga mbali ni vacuum..?
 
Naona mnaongelea elementary physics

Ndege inaruka na kutua kwenye vacuum lakini it depends na engine yake. Hapa sizungumzii engine za mapangaboi... nazungumzia engines kama zile za space shuttles
Utakuwa umeshachanganya mada mkuu, hapa kinachozungumziwa ni ndege mnyama.
Ndege obviously hawezi kuruka kwenye vacuum. Kwa lugha ya kawaida, ndege anachofanya ni kuogelea kwenye hewa, hivyo kama hakuna hewa basi hawezi kuogelea ataporomoka tu, na kama kitendo hicho kinafanyika sehem isiyo na gravity basi ataelea angani lakini si kwa kupaa!
 
Back
Top Bottom