Kama nilivyoandika kwamba sina uhakika sana kwa maana kuna mambo mengi, na kuna hili lililonijia kichwani baada ya kufikiria kidogo kuhusu Ndege kuweza kuruka kwenye vacuum, nimefikiria kwamba ili ndege aruke ni lazima kuwe na hewa/upepo ambayo ndiyo kwa kutumia mabawa yake humuwezesha kwenda mbele hivyo ili ndege aweze kwenye mbele au kuruka ni lazima kuwe na nguvu ya msuguano kati ya ndege/mabawa na hewa/upepo, sasa kama kwenye vacuum hakuna kitu ina maana hata hewa hakuna mabawa yatawezaje kumpeleka mbele ndege? Hivyo nafikiri hatoweza kuruka kwenye vacuum, ingawaje bado sina uhakika, ninaendelea kulifikiria!