Ndege hatari 100 za IDF zafanya mashambulizi makubwa na kusambaratisha maeneo 120 yaliyo ngome kuu za Hezbollah Lebanon kusini

Nanukuu:
"Hakuna Yahudi ataishi kwa amani ndani ya Middle East. Hivi vita wanavyovichokoza ndio vitasababisha anguko lao. Soon mataifa yote ya kiarabu yataamka na kutengeneza pande mbili...either uwe na wayahudi au uwe na Waislam".
Mkuu; Hapo kuna tatizo -TATIZO kubwa unapochanganya siasa na dini. Israeli (Myahudi) hakuna mahali popote aliwahi kusema vita yake dhidi ya HAMAS na Hezbollah ni vita dhidi ya Waislam. Ila baadhi ya Makundi ya kiislamu esp. yale yanayofadhiliwa na Iran na yenye kitengo cha kijeshi ndani yake, yanawarubuni baadhi ya nchi huru za mataifa ya Kiarabu kwamba Myahudi (Israel) anapingana (Israeli is against Islamic belief) dhidi ya Imani ya Kiislam jambo ambalo ni uzushi na ni uongo. Kwa bahati mbaya sana, yale mataifa ya Kiarabu yaliyoamini propaganda hizo yamejikuta yanashabikia na kujiingiza kwenye ugomvi ambao kiuhalisia HAUPO. e.g. Kuna kundi linalofadhiliwa na Iran lipo hapo Syria linajiita The Islamic Popular Force. Mambo ya kidini unayaunganishaje na mambo ya vita/jeshi? Yan ni kama tujiulize hivi kuna risasi na mabomu ya kiislam? Kama ni ndiyo, basi tuseme pia zipo risasi na mabomu ya kibudha, kikristo, n.k. n.k. Siku zote Tunamwomba Mungu atuepushie vita na Hatujawahi hata siku moja kumwomba Mungu atuepushie Uislam, Ukristo, Uhinduism, Ubudha n.k. n.k.
Kwa kifupi niseme tu kama angalizo kwamba HAKUNA MUNGU awaye yeyote yule (labda Shetani) mwenye mpango wa kikifuta kizazi chote cha Wayahudi au waIsraelites. HAYUPO na HATOKAA AWEPO.
Hakuna dini inayochuchumalia vita bali dini zote huzungumzia AMANI na Utengamano baina ya Wanadamu.
 
Story za jaba unaleta kwa great thinker
 
Mkuu na ndiyo ukweli usiosemwa huo. Hezbollah hamas na houth wote ni matawi ya Iran na ndiyo maana yalipochokonolewa mashimo yao Panya katoka kwenye shimo lake akarusha vimondo kuelekea Israel.
 
IDF ni shida sana aisee
 
Mkuu; Hilo sikubaliani nalo kamwe. Kama ingekuwa agenda ya Wayahudi ni kuua kila chembe chembe ya Uislam mbona si wangelianza basi na kuwamaliza wale Waislam waliomo humo ndani ya nchi ya Israel ambao ni zaidi ya milioni 1.7 (18%)? Haiingii akilini eti Wayahudi waende mbali kote huko wakatafute waislam wa kuwaua ilhali wanao Waislam ready at hand hapo nyumbani kwao?
Halafu kwa sasa chokochoko iliopo ni baina ya Makundi yanayojinadi kuwa ni ya kiislam lakini ni waislam wa madhehebu ya Shia peke yao. Madhehebu ya Sunni na Ahmadiya hawajajihusisha.
Ukweli ni kwamba ikitokea siku Iran ikatetereka au ikakubali kubadilika na kuacha kuyafadhili makundi ya kiislam yaliyopo na yenye harakati za kijeshi kwa ufadhili wao (Iran) naamini huenda hapo Middle East pakatulia.
Tena; Ingekuwa ni kheri sana usimhusishe Mtume Mohammad s.a.w na yanayoendelea huko Middle East. Laiti angelikuwepo nina uhakika angekugombeza sana.
 
Mkuu na ndiyo ukweli usiosemwa huo. Hezbollah hamas na houth wote ni matawi ya Iran na ndiyo maana yalipochokonolewa mashimo yao Panya katoka kwenye shimo lake akarusha vimondo kuelekea Israel.
Na kwa sasa kinachoendelea mezani ni jinsi ya kumfanya Nyani ateme bungo.
 
Fuatilia Hezibollah wametuma nini Israel katika kukumbuka October 7 na uharibifu uliotokea Israel.
 
Ifike wakati wapige magaidi na wanaowafuga wote pamoja
Kha! We hausikii vilio kutoka pande hizo "IDF anaua wanawake na watoto"? Unadhani hao wanawake na watoto ni nini kinawaweka hapo ilhali Mwamba alitoa matangazo ya kuondoka/kupisha mtifuano? Hao ndo wanaowafuga magaidi ndo mana wanachanganywamo.
 
Show ya VVIP Itawadia au sio
 
Israel inaisaidia Serikali ya Lebanon sana, msije shangaa baada ya Vita wakaanzisha ushirikiano
Hapana mkuu, hayo mashambulizi yanaiharibu Sana nchi ya Lebanon na kuua maelfu ya raia wasio na hatia.
 
Hamna jipya hapo, ungefuatilia vita ya Hezbollah na Israel 2006, ungedhani Lebanon itafutika na kubaki jangwa kwa jinsi IDF alishambulia.

Israel aache ubabe wa kipuuzi ME, aishi vyema na jirani zake hilo ndilo suluhisho.
Majirani zake wapo tayari kuishi naye kwa amani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…