Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
Nanukuu:Hakuna Yahudi ataishi kwa amani ndani ya Middle East. Hivi vita wanavyovichokoza ndio vitasababisha anguko lao. Soon mataifa yote ya kiarabu yataamka na kutengeneza pande mbili...either uwe na wayahudi au uwe na Waislam.
Huu ni mwanzo wa vita vingi vidogo vidogo kabla ya kuja Malhama al kubra (Vita kubwa na ya mwisho ) hapa duniani.
Mtume Muhammad (s a.w) alishaeleza haya kwa undani kabisa na kukusanyika kwa mayahudi katika ardhi ya palestina hakujaja kwa bahati mbaya bali ni mpango wa Mungu katika kukifuta kizazi chote cha Mayahudi.
Ni suala la muda watu watakuja kuelewa hivi vita
"Hakuna Yahudi ataishi kwa amani ndani ya Middle East. Hivi vita wanavyovichokoza ndio vitasababisha anguko lao. Soon mataifa yote ya kiarabu yataamka na kutengeneza pande mbili...either uwe na wayahudi au uwe na Waislam".
Mkuu; Hapo kuna tatizo -TATIZO kubwa unapochanganya siasa na dini. Israeli (Myahudi) hakuna mahali popote aliwahi kusema vita yake dhidi ya HAMAS na Hezbollah ni vita dhidi ya Waislam. Ila baadhi ya Makundi ya kiislamu esp. yale yanayofadhiliwa na Iran na yenye kitengo cha kijeshi ndani yake, yanawarubuni baadhi ya nchi huru za mataifa ya Kiarabu kwamba Myahudi (Israel) anapingana (Israeli is against Islamic belief) dhidi ya Imani ya Kiislam jambo ambalo ni uzushi na ni uongo. Kwa bahati mbaya sana, yale mataifa ya Kiarabu yaliyoamini propaganda hizo yamejikuta yanashabikia na kujiingiza kwenye ugomvi ambao kiuhalisia HAUPO. e.g. Kuna kundi linalofadhiliwa na Iran lipo hapo Syria linajiita The Islamic Popular Force. Mambo ya kidini unayaunganishaje na mambo ya vita/jeshi? Yan ni kama tujiulize hivi kuna risasi na mabomu ya kiislam? Kama ni ndiyo, basi tuseme pia zipo risasi na mabomu ya kibudha, kikristo, n.k. n.k. Siku zote Tunamwomba Mungu atuepushie vita na Hatujawahi hata siku moja kumwomba Mungu atuepushie Uislam, Ukristo, Uhinduism, Ubudha n.k. n.k.
Kwa kifupi niseme tu kama angalizo kwamba HAKUNA MUNGU awaye yeyote yule (labda Shetani) mwenye mpango wa kikifuta kizazi chote cha Wayahudi au waIsraelites. HAYUPO na HATOKAA AWEPO.
Hakuna dini inayochuchumalia vita bali dini zote huzungumzia AMANI na Utengamano baina ya Wanadamu.