Ndege JOHN nakupa mchongo uufanyie kazi, deal na breakfast ya vyakula vya asili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Anzisha mgahawa weka wafanyakazi wawili tafuta eneo zuri deal na breakfast ya vyakula vya asili tu. Nunua sahani 20 za udongo na Uma 20 na vijiko 20 na sufuria 5. Mazingira yawe masafi yenye maji ya kutosha na yanayovutia bila kusahau jiko kubwa la gas na friji liwepo.

Asubuhi nenda sokoni kanunue boga kubwa 1, tango 1, papai 1 parachichi 2, nyanya za buku 1, mayai ya kienyeji yawepo, Maharage na njugu, karanga kidogo, nyama utaamua wewe kama ukiinunua nusu ukakata vipande vidogo sana Safi na Mihogo vipande kidogo kidogo.

So unachofanya una wawekea mixer moja ya kibabe yaani kipande kidogo kidogo cha boga, tango, nyama zenye bamia kidogo, Maharage nusu upawa na bei yako uza 2500 tu watu Wana hela asubuhi asikudanganye mtu watu hawana hela za kujenga ila za kula wanazo na kwa sababu ya lifestyle yao wanakuwa waoga wanapenda kula Chakula tiba so ukiwakorogea vitu hivyo hukosi hela ni kufanya tu ubunifu na kusafiri unawakomba wote.

Naomba kuwasilisha.
 

Attachments

  • IMG_20211007_075310.jpg
    353.6 KB · Views: 17
  • DSC_0066.JPG
    2.6 MB · Views: 16
  • IMG_20210930_194717.jpg
    491.8 KB · Views: 16
  • DSC_0187.JPG
    1.9 MB · Views: 17
  • DSC_0029.JPG
    2.4 MB · Views: 14
  • IMG_20210727_123134.jpg
    238.2 KB · Views: 14
  • DSC_0195.JPG
    1.6 MB · Views: 14
Ahsante sana
 
Ndege John wakati flani unakuwa na akili.
 
Good idea ila sijaona chakula cha asili hapo.vikorokoro vyote hivyo siku hizi unavipata january mpaka disemba.
 
bonge la idea aseeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…