Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Ndege zenyewe zinaenda Arusha,Kigoma na Mwanza zikitoka nje ya nchi ni India na China au mpaka zikodishwe na Yanga iende Nigeria.

Hizo hela zipelekeni kutengeneza barabara za vijijini wananchi wasafirishaji mizigo kwa unafuu,pelekeni zikajenge madaraja au kama zipo nyingi sana wakopesheni SUMA JKT,Magereza na Shirika la maendeleo la taifa(NDC) ili waanzishe mashamba ya michikichi na waanzishe viwanda vya kukamua mafuta ya mawese .Nchi ina mamilioni ya hekari lakini mafuta ya kupikia yanatoka Malaysia aibu sana hii.
 
Siku hizi zitafanya kazi kwa kupokezana kwenda dodoma maana trip zimeongezwa thamani
 
Tungerudi zaidi kwenye kukamilisha ujenzi wa reli ya SGR. Safari za treni nzuri zikianza zitachangamsha sana uchumi. Safari mbili za treni ya SGR kwa siku kati ya Nairobi na Mombasa zimechangamsha shughuli nyingi za kiuchumi. Tujifunze huko.

Let us do the right thing. Consolidate on the planes for now (buy no more for now) na tuelekeze nguvu zote kwenye SGR. Please. Itawashangaza jinsi itakavyochangamsha shughuli nyingi za kiuchumi. Work on it as if our economy depended on it, for it does.
 
mimi nafikiri wangeanza kwa kuangalia gharama za uendeshaji ziwe realistic/competitive, then waweke bei rafiki kabisa mfano Arusha/dar 70,000shs flat rate; ili ndege ijae kila siku. Mbona ulaya wana hizo bei ($20/$30) na ndege kubwa zinaruka kila siku kati ya mji na mji na husikii wakilalamika kuwa wamepata hasara?
Huku kwetu ndege inafanywa anasa na hivyo kuwekwa bei isiyo rafiki hivyo route nyingi hazijai na kufanya ziende kwa hasara.
Unatoa ndege mpanda to Dar shs 300,000pp unapata abiria 35; Je ungechaji 100,000 ukapata abiria 170? kila siku
badala yake tunafuta route kuwa hailipi bila kuangalia kipato cha soko husika
Ni mtazamo tu
 
Hivi hizi ndege zinafanya operations kama kawaida kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…