Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki je wamejipanga kufika huko kiushindani?
Duh mama kaupiga mwingi hapo. Rais wa zanzibar kupokea ndege za air tanzania jambo jema sana. Zanzibar kwa utalii wa tanzania kazi iendelee.
 
mashirika haya yalitakiwa yaendeshwe na wataalam bila kuingiliwa na siasa , hivi mnakumbuka bomba la kutoka kibamba hadi kisarawe ,halikua na sababu kabisaaaa kisa tu kimada wa mtu yuko kule , hapo kwembe tu na msumi watu wanakunywa maji pamoja na mifugo. walishaambiwa wasikubali akili ndogo kutawala akili kubwa hawaelewi.
Yaani taifa linaangamia kisa mawazo ya mtu mmoja tu kaamua kufanya hivyo.

Ndiyo maana tunapigania kupata katiba mpya itakayo ondoa ukiritimba wa madaraka kutoka kwa mtawala.

Mwl JK Nyerere alisha wahi kusema kuwa kulungana na madhaifu ya katiba yetu tuliyo nayo.

Akitokea rais kichaaa basi anaweza akafanya madhara makubwa kwani katiba inamlinda.

Lkn kuna watu wakisikia habari za katiba mpya wanaogopa utadhani wamekutana na msafara wa wadudu wa korona.
 
Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki je wamejipanga kufika huko kiushindani?
1. Kwanini zipokelewe Zanzibar?
2. Serikali ya sasa isingeweza kuendelea kununua ndege kwa mtindo wao wa kiuendeshaji
3.Hayati JPM ndio aliacha tayari ziko kiwandani zinatengenezwa
4. Hawa wa sasa hawawezi kununua kwa pesa taslimu zaidi ya mikopo
 
Mashirika makubwa ya ndege kama SAA, KQ hata Emirates na KLM yamekuwa na changamoto kubwa za kibiashara na hata kufilisika. Angalia SAA ya Afrika Kusini inajitahidi kufufuka kwa taabu kubwa, hili ni shirika lenye ndege zaidi ya 120 na hufanya safari zake popote duniani!

Isitoshe linamilikiwa kwa ubia na wazungu na serikali tajiri ya Africa Kusini. Sijui itakuwaje na ATCL yetu kama tu tunshindwa hapa nyumbani kuendesha TTCL na TANESCO kibiashara.
Kwa hivyo unataka kusema tajiri fulani mtoto wake mwanaume ni baradhuli wewe masikini usizee kwa kuhofia kuwa mwanao kuja kuwa baradhuli
 
Ukinunua bus la abiria, arafu Nauli ikawa juu, watoto wako wakashindwa kupanda bus la baba yao, wakaenda kupanda mabus mengine ya bei nafuu, unadhan watakuelewa??

Maoni yangu, serikali itafute namna ya kupunguza Nauli za ndege hili watu wapande wengi na root ziwe nyingi.

Sasa hv unakuta ndege inaenda safar moja arafu kwa kukosa abiria inalala yooooo mpaka next day. Safar hiyo hiyo moja operation costs ziko juu balaa!

Jambo lingine, haswa safar za ndan, waruhusuni wawekezaji wa ndege za ndan wawe wengi ndo ushindan utakuwepo. Nadhan mlio ishi nchi Kama India mtakubaliana na mm ile nchi ilivyo na demostic flight nyingi Sana na hivyo naul ndogo na hivyo wasafir wanakuwa wengi!

Sasa apa kwetu..... , Ata Fast jet sijui ilikufia wap! .Juz nilikuwa Tunduma naenda kukata tiketi ya ATCL kutokea Songwe to Mwanza. Naambiwa hapa mzee unalipia Nauli ya root ya dar, then unalipia Nauli ya dar to mwz. Gharama walizo nipa root nzima inafikia milion na point .
Baada ya kuona hiyo gharama nikasema hapa kweli Shikamoo ATCL na Kaz iendelee.!!!

Serikali, ongezeeni wafanyakaz mishahara mizuri, punguzeni au kufuta kabisa vimatumizi vya kijinga arafu hela zipelekeni kweye mishahara ya watumishi..

Mfano wa vimatumizi vya kijinga ni Kama gharama za kukimbiza mwenge nchi nzima ukiwa chini ya ulinzi mkali wa police na bunduki n.k. inatusaidia nn kwa mfano?????

Wafanya biashara wapunguzien makodi..arafu muone Kama ATCL haitajaza abiria mpaka faida nono. Si nyie mnao tuambia Tanzania ni nchi Tajiri? Sasa ndugu Yetu Mwigulu mtaalam wa uchumi, mshaurin raisi wetu vizuri, mambo ya kutwambia Tozo Tozo zitajenga vituo vya afya kwan kikwete, Magufur walivijengaje? Na walipovijenga vilibomoka lini au vip jaman!!!!!

Ndege nunueni tu hata zifike 1000 lakin Kama hazipat abiria na root ku ongozeka ,hv kweli shirika letu litaepuka maden hapo jaman?
 

Attachments

  • VID_20210312_122425~3.mp4
    13.7 MB
Back
Top Bottom