Kwa ninavyoona TF-X inahitaji miaka isiyopungua 10 mpaka iwe deployable, tena hapo nimekuwa optimistic. Haijapata firts flight nadhani, mwaka huu ilikuwa na taxiing.
Uturuki inatafuta ndege kama stopgap ya kusubiri TF-X ikamilike. F-16 zake zinakaribia kuwa retired na Turkey iliondolewa kwenye project ya F-35. Possible stopgap inaweza kuwa F-16 tranche mpya kama walizonunua Qatar, kwa mbali sana ilikuwa inatajwa J-10 ya China.
TF-X inatumia General Electric F110 mojawapo ya very successful fighter engines available ila hii sio injini ya stealth fighter. Imetumika kama powerplant ya F-16, F-15 (ambako zinakuwa twin), Saab Jas-39 Gripen ya Sweden na nadhani hata F-14 Tomcat ilitumia hii au previous type yake.
Baadae wanaweza fikiria kufanya upgrade ya injini iliyo stealth, ni endapo watakuwa wamefanya design inayoficha injini kama hiyo design hamna basi hakuna haja na stealth capabilities will be compromised sababu ya heat inayotolewa na injini. Chinese nao J-20 yao haina injini yake halisi ya WS-15 bado iko kwenye testing, inawatesa sana injini hii.
Na Russia vilevile Su-57 haina injini yake halisi ya Izdeliye 30, bado inatumia AL-41.
F-22 na F-35 zinatumia injini zake zenyewe mahususi kwa stealth.
Wengine wenye projects za stealth fighters ni Uingereza hawa walikuwa kwenye hatihati ya kutoa 6th generation. South Korea wana Boramae, wanataka kushirikiana na UK. Japan nao kama sikosei wana yao. Ufaransa hataki 5th generation anafanya modernization ya Dassault Rafale anasubiri aende direct kwa 6th gen.
Ujerumani, Italy na Spain inawezekana watatengeneza consortium kama ile iliyotoa Eurofighter Typhoon, ila this time haitokuwa na UK. Na F-35 imeharibu hapo katikati wameinunua kasoro Ufaransa ambaye anapenda sana kukuza arms industry yake.