Sasa kule usiwe mzembe sababu taarifa hutokumbana nazo bali utazitafuta, kwenye mpira unaweza enda stand asubuhi kila mtu anajua Yanga wamesaini nani jana ila kuna mambo hayajulikani kijiweni. Baada ya muda fulani utakuwa ushaelewa. Kama kwenye mpira unakuwa na shauku kujua matokeo ya Bundesliga, La Liga, Serie A. Kwenye ulinzi utajua MAKS Airshow ya Urusi ni lini na inatarajiwa wataonyesha nini, utajua Zhuhai Airshow ya China ni lini, utajua Paris Arms Expo kumeonekana nini kipya, Turkey kwenye expo yao, Falme za Kiarabu nao. Utajua makampuni ya silaha makubwa kama unavyojua timu za mpira.
Nafollow waandishi wa ulinzi Twitter, nasoma articles zao, nasoma magazines kama 1945, The Drive, War is Boring, Bulgarian Military, National Interest. YouTube baadhi ya channels za uhakika.
Ukishaanza hivyo algorithm ya mtandao itakusaidia kukuletea habari unazopendelea. Google haiwezi niletea mambo ya Zuchu maana kupitia cookies inajua huwa siyasomi, nikifungua nakutana na hivi na vitu vingine navyopenda
View attachment 2702437