Ndege mpya ya kivita ya Kituruki Model tf-x iko katika hatua ya mwisho kuundwa

Inatisha.
pamoja na kutisha kote, haifui dagu kwa Mwisrael, anawachapa wapalestina pale na uturuki kafyata mkia hawezi kupiga hata chafya. dege au uwezo kama huo angekuwa nao Iran, angeshajilipua though hawezi kushindana na Mungu wa Israel, atafyekwa.
 
pamoja na kutisha kote, haifui dagu kwa Mwisrael, anawachapa wapalestina pale na uturuki kafyata mkia hawezi kupiga hata chafya. dege au uwezo kama huo angekuwa nao Iran, angeshajilipua though hawezi kushindana na Mungu wa Israel, atafyekwa.
You're right.
 
Vipi kuhusu Japan mkuu najua technically wapo advanced sana ila kwenye hizi marathon za kijeshi hatuwaoni kabisa kwenye chart wenyewe hawajaanza development ya hizi fifth generation?
 
Huko kwenye military ntakua mwanafunzi kila Siku!
 
Kwani mpaka wa ulaya uko wapi?
 
Sasa Cyprus na turkey Kuna tofauti gani!?..wanagombea Hadi mipaka
 
Sasa Cyprus na turkey Kuna tofauti gani!?..wanagombea Hadi mipaka
cyprus ugomvi uliopo wewe hauujui. ndani ya cyprus kuna asilimia karibia 80 ya watu wenye asili ya ugiriki, hao wamekuwa supporten na ugiriki tangu enzi kama urusi anavyosapoti watu wa kabila lake kule ukraine. upande wa juu wa kisiwa cha cyprus kuna kipande kidogo kuna raia wenye asili ya uturuki, na hao ni waislam. hao wamekuwa supported na turkey for years. ndio maana ugiriki na uturuki wamekuwa wakipigana vita miaka mingi ila kwenye ardhi ya cyprus. ile pande ya cyprus ambayo ni ya ugiriki, inatambuliwa kuwa ni european union tangu 2004, ile pande yenye waturuki haitambuliki hadi kesho ni watu wasio na taifa. cyprus ipo EU na wanatumia euro. although, kijiografia, cyprus ni technically europe, kiuhalisia ipo upande wa Eurasia (Asia) lakini kwasababu ni kama wagiriki, imeunganishwa na ugiriki.
 
Watu wanajua hadi mishahara ya wachezaji 😂
Jamaa ana vitu vichache kichwani vya maana hvy anadhani na wengine pia wapo kama yeye.
 
Haiondoi hoja kwamba wanagombea mipaka
 
Huko kwenye military ntakua mwanafunzi kila Siku!
Sasa kule usiwe mzembe sababu taarifa hutokumbana nazo bali utazitafuta, kwenye mpira unaweza enda stand asubuhi kila mtu anajua Yanga wamesaini nani jana ila kuna mambo hayajulikani kijiweni. Baada ya muda fulani utakuwa ushaelewa. Kama kwenye mpira unakuwa na shauku kujua matokeo ya Bundesliga, La Liga, Serie A. Kwenye ulinzi utajua MAKS Airshow ya Urusi ni lini na inatarajiwa wataonyesha nini, utajua Zhuhai Airshow ya China ni lini, utajua Paris Arms Expo kumeonekana nini kipya, Turkey kwenye expo yao, Falme za Kiarabu nao. Utajua makampuni ya silaha makubwa kama unavyojua timu za mpira.
Nafollow waandishi wa ulinzi Twitter, nasoma articles zao, nasoma magazines kama 1945, The Drive, War is Boring, Bulgarian Military, National Interest. YouTube baadhi ya channels za uhakika.
Ukishaanza hivyo algorithm ya mtandao itakusaidia kukuletea habari unazopendelea. Google haiwezi niletea mambo ya Zuchu maana kupitia cookies inajua huwa siyasomi, nikifungua nakutana na hivi na vitu vingine navyopenda
 
Vipi kuhusu Japan mkuu najua technically wapo advanced sana ila kwenye hizi marathon za kijeshi hatuwaoni kabisa kwenye chart wenyewe hawajaanza development ya hizi fifth generation?
Mitsubishi wana project ya F-X na ni serious project.
Ndege nyingi prototype zinaitwa something-X then zikikamilika ndio zinaitwa something-suffix ya version inayofuata, hata experimental aircrafts zinakuwa na -X mwishoni hasa NASA wanazo nyingi wanaweza lipia hela zitengenezwe ndege mbili tu watest concept kisha wazibe mdomo na hizi ndio zinakuwa za siri.
Ni Western culture ambayo Russia na China hawafuati.

Russia wao wana mfumo mgumu sana ambao kuna jopo sijui taasisi inatoa namba kwa kila silaha. Mfano Akula class submarine ni Project 971, na hizi namba hazina mtiririko maalum ni namna jopo litakavyoamua. Kisha project ina jina la prototype na jina la type (kama ni prototype ya kitu muhimu kama frontline fighter, kifaru, etc). Su-57 prototype name yake ni PAK-FA. Pia kuna sababu nyingine inachangia kama jina halina bahati labda prototype ilipata crashes nyingi wanaona lina gundu. Kwenye military aviation mambo ya bahati, mkosi, fate, gundu, nyota wanayazingatia.
NATO wanazidisha ugumu kwa kuita kila silaha ya Urusi jina lake (NATO reporting name). Mfano NATO reporting name ya Mig-29 ni Fulcrum.

Tukirudi kwenye next generation fighter ya Japan. Inajulikana itakuwa F-3, watatoa -X waweke -3 sababu inaenda retire Mitsubishi F-2 ambayo ni licence production ya F-16 ya Marekani na zinafanana sana ukiziona bila camouflage na missiles za nchi hizo mbili tofauti.

Sababu kubwa ya kutojua silaha za Japan ni kuwa katiba yao inazuia kuuza silaha nje, wala kutuma jeshi nje ya mipaka yao. Hivyo silaha zao hazisikiki ila ziko vizuri ingawa ni ghali sana kutokana na economies of scale.
 
Ngoja niendelee kujifunza lakini Sasa kama hizi taarifa zote zinakua exposed usalama upo wapi? Mfano Leo Israel pale middle east anauhasama na mataifa mengi ya kiarabu na unakuta haya mataifa yanajua zana za kivita za Israel, huoni kama Israel anakua kwenye risk kubwa🧐🧐

Kwa sababu upo na uelewa na hv vitu Kuna mambo natamani unisaidie;

1. Kwanini kunakua na masharti kwenye matumizi ya baadhi ya zana za vita mfano juzi Kati BBC waliripoti kwamba Biden kuna silaha Fulani sizikumbuki vizuri jina alikua anataka kuwapa Ukraine lakini akawa anataka kuungwa Mkono na mataifa kama France,German & UK, wanadai haziruhusiwi kutumika 🤔kama tunapigana si tupigane tu tusichaguliane namna Wala zzana za kutumia

2. Wakati wa mgogoro Kati ya Russia Vs Ukraine kuna kipind waliingia mkataba wa kusafirisha nafaka kupitia bahari nyeusi, Sasa pale mataifa makubwa yamemuwekea vikwazo Urusi na bado wanasaidia Ukraine silaha inakuaje wanaingia makubaliano 🤔🤔mengine hadi kubadilishana wafungwa

🙏🙏Naomba kuwasilisha
 
Japan walitaka kununua F-35B za kutumika kwenye Carrie yake 'Izumo' kama njia ya kukabiliana na China.


Ila Japan inaweza ikawa military power hasa kwenye naval na air force ikiamua kulegeza sera zake na kupunguza kuitegemea US .

....natamani kuona project yao ya 6th gen. (watakayoifanya binafsi au kushirikiana na Washirika hasa Australia) nione italeta matokeo gani hasa kwenye ushindani na makampuni ya US.
 
Safi hapo nimekusoma vizuri kiongozi we ni mnoma.
NIlikua curious sana kuhusu Japan kumbe policy zao ndio nimekanza nitaanza kufatilia kiundani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…