Jana nimesafiri na ATCL ndege number TC 106 Bomberdier toka Dar kuja Mbeya. Hii ndege tairi moja ni kipara mpaka nyuzi zinaonekana kabisa. Hii ni hatari sana.
Nilikaa dirishani mkabala na hizi tairi. Jana tulitoka Dar na mvua, na mipira ikiloa si rahisi kuona jinsi mpira ulivyolika. Tunafika, mipira imekauka. Ilivyotoa tairi nikaona jinsi ilivyoisha. Nilikosa amani mpaka ilipo simama.
Hata kama ni tubeless, nadhani kuna kiwango kinacho ruhusiwa cha tairi kulika. Kwa namna zilivyo hapo, hata uwiano wa kubeba mzigo wakati wa kutua ni tofauti. Sababu hiyo tairi isiyolika sana ndio inaanza kugusa chini na kubebe mzigo mkubwa. Hebu fikiria ndege imetua na hiyo tairi inapiga mzinga wakati iko kwenye speed. Au iko kwente speed ya kuruka halafu ndiyo ina piga mzinga. ATCL mtatuuwa kizembe.
View attachment 2197854
View attachment 2197855