Probably ishu ni Ukraine na Iran...Zipo Kila dalili zinazoonesha sasa Russia anakwenda kufanya mass mobilization ya Jeshi kwaajili ya kazi au operation Kali kabisa na ishu ya Iran kuhusu biashara na Russia, US anataka kumbana Russia aachane na Iran, kumbuka Trump tayari kashaweka zuio Kwa Iran la kufanya biashara Kwa partners zake wote...
Mwaka 2021 Nakumbuka CIA director alimtahadharisha Putin asivamie Ukraine but Putin aliivamia kama kawaida...
Kumbuka Putin anataka ahakikishiwe kuwa Ukraine inakuwa neutral, kinyume na hapo hakuna neno atakalolielewa so maybe CIA boss amekwenda na dili zuri mezani,kama ni maneno matupu basi Putin hawezi kukubali lazima safari hii atatumia nguvu kubwa Sana kwenye field maana Ukraine wamekuwa wakipiga sehemu muhimu za Russia siku hizi Kwa msaada wa NATO hasa UK, Germany...NATO kuna kitu wanakitafuta.
Watu wanaamini Russia yuko vibaya na mobilization lakini ikumbukwe North Korea yuko anajiandaa kuipelekea wanajeshi hata 300,000 atatoa makubaliano yakiwa mazuri kwake.
Bado North Korea anaongezea high caliber rockets, shells za mizinga maana wanatumia caliber sawa na Urusi, na makombora ya masafa mafupi. Kwa sasa Iran hana uwezo wa kuisaidia Urusi ila North Korea anao.
Kwa hiyo kama utaratibu wao ule ule utaendelea kwamba N. Korea atoe wapiganaji na silaha, kisha Russia atoe critical minerals na energy kwa China, kisha China atoe resources na fedha kwa N. Korea kwa niaba ya Urusi (maana kuna ugumu wa kufanya exchange baina ya Rus na N.K). Kwahiyo iwe barter trade, Urusi anadaiwa na North Korea ila China anadaiwa na Urusi. Kwahiyo China angemlipa Urusi, ili Urusi amlipe North Korea. Badala yake China anamlipa North Korea.
Pia China aongeze kutoa critical components kama small jet engines direct kwa Urusi.
Hapo Urusi anaongezea na mobilization ya kwake na strikes nyingi bila kuzingatia makazi ya watu. Ukraine haina interceptors nyingi na haina uwezo wa kufanya mobilization kubwa na hata ikifanya kidogo haiwezi fanya training nzuri ndani ya muda mfupi.
NATO kwa sasa hawana motivation kubwa ya kuisaidia Ukraine. Sana sana Ukraine itazidisha mashambulizi ya masafa marefu ambayo Putin atakwepa kulaumiwa hivyo hatotaka yatokee mara nyingi. Atataka vita iishe haraka.
Suala la Iran sioni kama ni la kumpeleka CIA Chief. Hilo sio la ghafla ingeenda delegation nyingine ya juu na ya kufanya maamuzi taratibu.
Marekani pale naamini imeenda na ultimatum ya kuifanya Urusi ama wakubali kutokubaliana, ama waumizane. Urusi kihistoria ikifika makubaliano na Marekani huwa inaachwa ifanye bluff, US haina cha kupoteza hata ikionekana imekaripiwa viongozi wake mara nyingi sio machismo.
Ikifanikiwa Russia watapiga blah blah, then huku nyuma wamekubaliana na masharti waliyowekeana na US ya kutovunjiana heshima na kuvuka mipaka. Mwishowe ni stalemate na hali inarudi ilivyokuwa mwanzo kuheshimiana.
Kinyume na hapo, vita inaendelea kwa muda kidogo wakati kila mtu ameishachoka. Ila matokeo ni yale yale ama suluhu ama Russia ashinde.