Ndege ya kijeshi ya usafiri ya Colombia iliyokuwa imebeba wanajeshi 80 imeanguka muda mfupi baada ya kuruka angani

Ndege ya kijeshi ya usafiri ya Colombia iliyokuwa imebeba wanajeshi 80 imeanguka muda mfupi baada ya kuruka angani

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Jeshi la Colombia limesema leo kuwa takriban wanajeshi 80 wanahofiwa kufariki dunia baada ya ajali ya ndege ya usafiri kusini mwa nchi hiyo. Kulingana na shirika la habari la AFP, likinukuu chanzo cha kijeshi, angalau vikosi viwili (platoons) vilikuwa ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Lockheed C-130 Hercules, inayotumika kwa usafiri wa kijeshi.

Ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka Puerto Leguizamo, karibu na mpaka wa kusini wa Colombia unaopakana na Ecuador. Waziri wa ulinzi wa Colombia amesema wengi wanahofiwa kupoteza maisha.

Televisheni ya taifa ya RCN ilirusha picha zikionyesha mabaki ya ndege yakiwa yameharibika vibaya na kuwaka moto ndani ya eneo la msitu. Kwa kawaida, ndege ya aina hiyo inaweza kubeba takriban wanajeshi 100.
=============
Colombia's military said today some 80 troops were believed to be dead after a transport plane crash in the south of the country. There were at least two platoons on the plane, news agency AFP reported quoting a military source. The plane was a C-130 Hercules tactical transport aircraft.

It crashed on takeoff from Puerto Leguizamo, near the southern border with Ecuador. Colombia's defence minister said many are feared dead.


State broadcaster RCN ran images of a badly damaged fuselage aflame in a forest clearing. This aircraft can typically carry about 100 troops.

"Military units are already at the scene. However, the number of victims and the causes of the crash have not yet been confirmed," the defence minister posted on social media.

"It is a deeply painful event for the country. May our prayers bring some measure of comfort."

With inputs from agencies
 
1774287144606.png
 
Back
Top Bottom